UWT yafuata nyayo za Umoja wa vijana; yaonya wanaokosoa CCM hadharani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UWT yafuata nyayo za Umoja wa vijana; yaonya wanaokosoa CCM hadharani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 26, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  BARAZA Kuu la Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT), limewaonya baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao wameanza kujipanga na kuweka mikakati binafsi ya kuwania nafasi ya urais 2015 kwa kuwa jambo hilo ni hatari kwa chama.

  Mbali na hilo, pia UWT imeonya tabia ya baadhi ya viongozi wa chama na serikali kukemeana hadharani na kwenye majukwaa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa badala ya kutumia vikao sahihi vya chama.


  Hayo yanatokana na maazimio ya kikao cha Baraza Kuu ambalo lilikutana Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo lilijadili mambo mbalimbali likiwemo la kutathimini changamoto zilizokikabili chama katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana.


  Hivi katibuni, Umoja wa Vijana wa CCM ulifanya kikao cha Baraza Kuu mkoani Dodoma na kutoa maazimio mbalimbali, likiwamo la kuwakemea na kuwatisha wanachama wa CCM wanaokikosoa hadharani badala ya kwenye vikao, na kuweka bayana kuwa chama kisiwateue kuwania nyadhifa mbalimbali baadaye.


  Akizungumza na Majira, Katibu Mkuu wa UWT, Bi. Amina Makilagi alisema mbali na kukemea tabia hiyo, pia jumuiya hiyo imewataka wanachama wote wa CCM kurejea utamaduni wa kujitolea kwa moyo ndani ya chama na kuachana na tabia iliyojengeka miongoni mwa wanachama wake ya kudai malipo wakati wa shughuli za kujenga chama.


  Pia UWT iliazimia suala la kuimarisha uhai wake na wa CCM kwa ujumla ambapo iliwahimiza wanachama kuendelea kuimarisha uhai wa jumuiya na chama kwa kuingiza wanachama wapya na kulipa ada kwa mujibu wa katiba na pia iliazimia kuandaa mpango utakaowajengea wanawake uwezo wa kuchangia maoni katika mabadiliko ya katiba ya nchi yanayotarajiwa kufanyika.


  "Mbali na hayo, UWT na chama ni lazima viendelee kujiimarisha kiuchumi kwa kuboresha rasilimali na miradi yake ili kuondokana na tabia ya utegemezi...na katika kujiimarisha zaidi UWT itaweka utaratibu maalumu wenye msingi thabiti wa kuajiri kulingana na mahitaji ya soko la sasa la ajira na kwa kuzingatia maendeleo ya sayansi na teknolojia," alisema Bi. Makilagi.


  Katika suala la kulinda amani na utulivu, baraza hilo lilivitaka vyama vya siasa kuepuka kutumia vibaya fursa na haki za sheria ya vyama vya siasa kufanya maandamano na kuendesha mikutano kwa nia ya kueneza siasa za uchochezi na chuki miongoni mwa wananchi kwa lengo la kuwahamasisha wananchi kuichukia serikali yao.


  "Kwa upande wa wanawake, baraza liliwataka kuepukana na siasa za uchochezi zinazoenezwa na CHADEMA kwani zinawagawa wananchi kisiasa na kiitikadi badala yake wajizatiti kufanya kazi za kujiletea maendeleo," alisema Bi. Makilagi.


  Akizungumzia ilani ya CCM, aliitaka serikali kuendelea kuboresha sekondari za kata kwa kuwa zimepanua fursa ya kupata elimu kwa watoto wengi wa kike na pia kupunguza kwa kiwango kikubwa tatizo la mimba za utotoni.


  Wakati akifungua kikao cha baraza hilo Mwenyekiti wa UWT, Bi. Sophia Simba aliwataka wanawake kuvunja ukimya kwa kujibu mapigo yanayoelekezwa kwa CCM na vyama vya upinzani kwa kuwa siasa zimebadilika kwa kiasi kikubwa.
   
 2. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #2
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mungu isaidie tz
   
 3. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #3
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Unajua Mwenyekiti wao ni Mama Sophia Simba na Unajua ni kibaraka wa Rais Kikwete unajua tena Meya wa Jiji la Dar ndie aliyemshauri Rais Mwinyi kumtafuta Kikwete na kumpa Madaraka... Mama Simba kazaa na huyo Meya wa Jiji la Dar... Domino Effect!!!
   
 4. Domhome

  Domhome JF-Expert Member

  #4
  Mar 26, 2011
  Joined: Jun 28, 2010
  Messages: 1,986
  Likes Received: 1,043
  Trophy Points: 280

  .....KK.....
   
 5. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #5
  Mar 26, 2011
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Angalau shangazi sofie ameonyesha umahiri wa hoja ... Amebalance wito wake kwa wana ccm na pia kuihadhari ccm na cdm.... Ni vema home work ifanyike ndani yetu ccm hasa nyie wenye mamlaka na siyo sisi wenye kadi maalum kwa kura za maoni......
   
 6. G

  Godwine JF-Expert Member

  #6
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  duh kazi 2012 makamba naye out, kinana out, membe out,lowasa out,rostam out,chenge out, sofia ou, makinda out,
   
 7. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #7
  Mar 26, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,036
  Likes Received: 3,067
  Trophy Points: 280
  hata wakazindike hii CCM haifiki 2015...warejee kauli zote za Nyerere enzi za uhai wake Vs CCM ..
   
 8. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #8
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Ila sio ccm
   
 9. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #9
  Mar 26, 2011
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  CCM out of power
   
 10. G

  Godwine JF-Expert Member

  #10
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  lakini tukiombee kiondoke kwa amani na tuwe tayari kukiunga mkono kikiwa chama cha upinzani sio tukiue moja kwa moja sawa?
   
 11. M

  Makiyuve Member

  #11
  Mar 26, 2011
  Joined: Sep 7, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi jamani huu ni umoja wa wanawake Tanzania au ni UMoja wa wanawake wa CCM Tanzania?
   
 12. m

  mbongopopo JF-Expert Member

  #12
  Mar 26, 2011
  Joined: Jan 24, 2008
  Messages: 1,112
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hadi raha wakome sasa wao kwa wao
  Wana ccm mnalo
  Bora mie nisie na chama
   
 13. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #13
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  That will never happen by talking and writing some abuse language
  out of power kirahisi rahisi kama upo kitandani na mke,kuwa out of power kuna hitaji nguvu ya hoja watu wakuelewe nini unataka na pia wakusapoti kwa kile utakacho,la sivyo utakauwa kila siku unaliandika hilo OUT OF POWER HADI unaingia kaburini
  unachotakiwa kufanya kwanza wewe mwenyewe ukubali kubadilika then usafilishe hicho hayo kwa jamii inayo kuzunguka

  labda itawezekana lakini si kwa kukaaaaaa na kuongea na kuandika na kutukana
  badilika wakati ndio huuu
   
 14. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #14
  Mar 26, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Nadhani huzijui vyema siasa za ccm,hiyo ni mikakati madhubuti ya kukiweka chama ktk hali ya kujulikana na kusikika masikioni mwa watu na wanachama wake,ili muweze kuelewa usafi uliopo na mwisho wa siku kuingia ktk mtego wa kukitambuwa na kukisapoti chama
   
 15. Sabasaba

  Sabasaba Member

  #15
  Mar 26, 2011
  Joined: Jul 12, 2007
  Messages: 88
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15  Hii ni issue!!! sijui katiba ya Tanzania inasemaje kuhusu hili, naona kuna conflict of interest kwenye hili jina kwani kuna wanawake wengine sio lazima wawe CCM, kuna watu wamenyimwa haki zao hapa, ivi mwanasheria anaweza kushtaki kuwazuia kutumia hili jina!, sheria inasemaje kuhusu hili?
   
 16. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #16
  Mar 26, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mwenyekiti wa ccm ..atakiangamiza chama na taifa ...Where is he to give FIRM statements and directives which water downs all the pate stories everybody is giving???????
   
Loading...