VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Mabaraza haya ya Wanawake ya CCM na CHADEMA,kwa mujibu wa Rasimu ya Katiba mpya, sasa yamepewa uhai mpya. Yatatakiwa kulea,kukuza na kuimarisha viongozi watarajiwa wa nchi hii. Mabaraza haya yatatutolea mgombea mmoja kwa kila jimbo la Uchaguzi wa Wabunge (Majimbo yote yakiwa 35) Tanzania Bara na Zanzibar. Ni wakati muafaka sasa kwa UWT na BAWACHA kuanza kazi ya kutukuka. Kazi rasmi za kisiasa kutuandalia viongozi. Na kazi ianze sasa! Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam