Elections 2010 'Uwongo wa Dr Slaa' na maslahi ya taifa

Magobe T

JF-Expert Member
Mar 19, 2008
4,621
2,567
Wakati Dr Slaa anaibua hoja za Richmond na EPA bungeni Dodoma aliitwa mwongo na mara kadhaa Spika wa Bunge alimwambia afute kauli yake. Sisi wote ni mashahidi. Lakini baada ya ukweli kugundulika kuwa Richmond na EPA ulikuwa ufisadi, vigogo kadhaa wa CCM wakasema hoja hizo ziliibuliwa na wao na si kutoka vyama vya upinzani. Walidai vyama vya upinzani vilidakia hoja yao ya ufisadi.

Hili la uchakachuaji wa kura za uchaguzi, Dr Slaa amekuwa akitajwa na vigogo fulanifulani kuwa ni mwongo na mchochezi (sedicious) na kwa sheria za Tanzania mwongo na mchochezi ni mhalifu. Kujua kuwa haya makosa mawili ni uvunjaji wa sheria za nchi, wewe au mimi ongopa juu ya serikali au chochea na na utakiona cha moto! Dr Slaa amekuwa akisisitiza kuwa ana ushahidi wa yale anayoyasema na anadai vyombo husika kuliko kukanusha vichunguze tuhuma hizo. Anasema yuko tayari kutoa ushahidi mahakamani endapo mtu yeyote anayeshtumiwa kuhusika kwake kwenye ufisadi au uchakachuaji wa kura atamshitaki.

Lakini mpaka sasa hatuoni huyu 'mwongo' na 'mchochezi' akikamatwa na vyombo vya dola. Je, inatufundisha nini sisi Watanzania? Binafsi najifunza mambo manne:

1. Dr Slaa siyo mwongo bali ni mkweli na anapigania haki inayoonekana ikipindishwa waziwazi kwa maslahi binafsi. Anaweka maslahi ya taifa mbele kwa yale anayotaka yatendeke!

2. Serikali yetu haina utashi wa kisiasa kushughulikia matatizo au changamoto zinazoikabili hasa pale wananchi wanapoelezea kero zao na kuhoji kwa nini hazishughulikiwi ipasavyo.

3. Wanaotaka na kutetea mabadiliko siku zote wanakumbana na matatizo kama anayokutana nayo Dr Slaa. Waliozoea njia za mkato wanaona kile wanachokifanya ndio sahihi na yule anayetaka haki itendeke anaonekana ndiye mbaya. Baadhi yetu tumekuwa tukiweka mbele ushabiki wa vyama kuliko maslahi ya taifa. Tukiendelea hivi, demokrasia Tanzania itabakia nadharia na maendeleo yatachelewa sana.

4. Kama Dr Slaa aliibua hoja za ufisadi kuhusu mikataba mibovu ya madini, Richmond, EPA nk na kuambiwa mwongo, sitegemei kama akiibua uchakachuaji wa matokeo ya kura za uchaguzi asiambiwe mwongo!
 
Hata mimi nilikuwa najiuliza swali hilo hilo, kama kweli Dr. Slaa ni muongo, mzushi, mchochezi na anahatarisha usalama wa taifa, mbona hachukuliwi hatua za kisheria?

Mimi nilitegemea badala ya TISS kuongea kinadharia tu, wangemchukulia hatua za kisheria kama inavyofanyika kwa wengine. Kuendelea kutomgusa Dr. Slaa ina maanisha kitu kimoja tu, wao ndio waongo, wazushi, wachochezi na ndio wanaohatarisha usalama wa taifa.
 
Usije ukashangaa siku CCM wakidai suala la wizi wa kura wao ndo walianzisha na Dr Slaa alidandia hoja yao:tape:
 
Hilo inawezekana hao waliomjibu walijibu kwa kukurupuka na kujibu bila kujuwa hayo masuala undani wake.

Lakini Dkt Slaa bado ni muongo, kwani mwaka jana kwenye kampeni alichakachua barua ya kusema JK alikuwa anafanya Mkutano wa Siri mwanza, na RA, EL na wengine walikuwepo. Ikabainika kuwa ni Muongo

Sasa tusimtetee sana hata kama tunampenda; huwa anachemka sana tu.
 
Hilo inawezekana hao waliomjibu walijibu kwa kukurupuka na kujibu bila kujuwa hayo masuala undani wake.

Lakini Dkt Slaa bado ni muongo, kwani mwaka jana kwenye kampeni alichakachua barua ya kusema JK alikuwa anafanya Mkutano wa Siri mwanza, na RA, EL na wengine walikuwepo. Ikabainika kuwa ni Muongo

Sasa tusimtetee sana hata kama tunampenda; huwa anachemka sana tu.

Dr Slaa alisema akina kikwete walikaa kikao mwanza, akina kikwete na kundi lake wakakanusha. Wewe unamwamini yupi kati ya hao bila ushahidi. Mahakamani wangecheck hisotoria yao ya nyuma na kufanya uamuzi. Dr Slaa anajulikana kwa kusema ukweli - mifano michache imetajwa na mleta mada. Kikwete ni mwongo. Hajaleta maisha bora kwa kila mtanzania. idaidi ya watoto wake anatudanganya. - eti watoto kadhaa. Kwa hiyo, hata ktk sakata la mwanza mimi naamini Dr Slaa yuko sahihi. Na wewe je?
 
Back
Top Bottom