uwongo huu ni wa nini?

bne

JF-Expert Member
Oct 11, 2016
1,672
2,006
Huwa nasikiliza hotuba za raisi wetu John Pombe Magufuri kuhusu upungufu wa chakula nchi ni hadi najiuliza uwongo ni wa nini?
Kwanini mkuu wa nchi anaingia ktk mtego huu wa kuwadanganya, kuwafokea, kuwakejeri,kuwadharau na hata kuwavunjia ubinadamu wananchi wake waliomchagua kwa kuwasingizia uwongo?
Jamani ni ukweli usiopingika kuwa kunaupungufu mkubwa wa chakula nchini na mahitaji ni makubwa. Lkn si kweli na narudia tena kuwa si kweli ni uwongo mkubwa kuwasingizia wananchi kuwa wanataka vyakula vya bure ,si kweli. Raisi si kweli unawaonea.
Wananchotaka wananchi hawa wanyonge ni kwa serikali kufidia hili gap LA upungufu ili chakula kisipande bei ili waendelee kununua kwa bei nafuu lkn siyo chakula cha bure, huo ni uwongo.
Raisi wasaidizi wako wanakudanganya sana, na Bahati mbaya nawewe unakubaliana nao,naomba ujiongeze na zakwako.
Nakuomba Raisi usishiriki dhambi zao wanaowasingizia kuwa wananchi wanataka bure, na wewe Bahati mbaya umeimba wimbo huo huo wa bure, unawasingizia.
Maana ya maghala ya serikali ya chakula ni nini? Si kutoa bure Bali kufidia pale palipo na upungufu ili kudhibiti bei.
Wananchi hawataki bure, wanachotaka kutoka kwako ni kujazia huo upungufu ili wasiumie lkn wataendelea kununua kwa hela zao, acha kuwasingizia baba kuwa wanataka bure.
Sasa Raisi wasipokuomba wewe wamuombe nani? Si wewe ndiyo walikua kura mbona unawangusha? Imefikia hatua sasa tunajuta kwa nini tulikupa wewe? Mbona wanyonge uliosema uko kwa ajili yao ndio wanataabika huku wewe ukiwakejeri.
Si vema hata kidogo.
 
Hapa tulipofikia kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe-namaanisha suala la njaa kila mtu apambane kuokoa familia yake mwenyewe.
Hali ni mbaya mimi nimechukua hatua naenda sehem kubeba gunia 10 za mahindi zitaipitisha familia yangu hata hadi mwezi kama huu mwakani.
Nikishaleta nitakuwa upande wa bwana yule kupinga vikali uwepo wa njaa kwani nitakuwa nashiba na ndugu zangu kama bwana yule.
 
NADHANI labda ALIZOEA KUPEWA VYA BURE... na majukumu aliyonayo anashindwa kupanga njia madhubuti ya kutatua matatizo ya jamii badala yake anadhani kila mtu ni ombaomba bila sababu anaishia kufoka tu akidhani watu wataogopa!
 
Siku hizi Kauli mbiu yao ya ''HAPA KAZI TU" ni kudeal na wapinzani na wanaoikosoa sirikali. HAMNA KAZI ZINGINE. NDIYO TATIZO LA KUSHINDA KIWIZI. KM MESHINDA KIHALALI KWANN MNAWEWESEKA SANA?
UTAKUTA WA LUMUMBA WAPO BUSY NA UPINZANI TU. Uzuri wa upinzani wao wanadili na vitu vya maana vya kimaendeleo hata kikifanyiwa kazi kinaleta maendeleo. Angalia thread za WanaLumumba ovyo sana, ni zz kujipendekeza ili wapewe vyeo
 
Back
Top Bottom