UWIZI WA VIONGOZI WA AFRIKA HUANZIA KWENYE SANDUKU LA KURA

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Nov 7, 2012
1,970
2,000
Uzalendo wautoe wapi?? Waliowengi uwizi wao huanzia kwenye sanduku la kura sasa tunatarajia wawe ni watu wenye kutenda haki au kutetea maslahi ya taifa ??
Uzalendo hukosekana tangu kwenye kipiga, kuhesabu na kutangaza matokeo ambayo mostly chama kilicho madarakani hushinda sasa tunategemea tuwe na viongozi wazalendo na wenye kupenda haki?? Uzalendo wanaojitangaza nao ni koti tu lakini ndani wamevaa mashati yenye ubinafsi, chuki, udikteta nk.

Wanapenda kujihalalishia maovu yao kwa kigezo cha uzalendo na kuleta maendeleo, nchi nyingi za Afrika kiongozi anaongoza kwa fikra zake ndo maana lisemwalo baya leo kesho akija kiongozi mwingine laweza kuwa zuri na wafuasi wakashangilia.....uzalendo wa wanaAfrika waliondoka nao akina Mandela, Nyerere, Nkrumah nk. Haiwezeka eti unakuwa raisi kwa mfano toka 1994 na una uhakika wa kuwa madarakani hadi 2034 kwa kubadili katiba. Mtu yeyote mwenye kuja na hoja ya kuongezewa kiongozi muda ni mchochezi mkubwa anajaribu kuwasha moto ambao hata yeye utamuunguza, uzalendo si kukaa madarakani muda mrefu, si kuwa na chuki dhidi ya wakupingao....by the way kutaka kudhibiti mitandao ni dalili nyingine ya kuja giza, watafanya watakalo huku sauti za wanyonge zikiwa zimezimwa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom