Uwindaji haramu Tanzania: Ni nani yupo nyuma ya waarabu hawa?

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,007
2,675
Wakuu,

Kuna mambo yanashangaza kidogo ila yanasikitisha sana ukiyaangalia.

Tunazo mamlaka zetu, tumeziamini na zinatakiwa kuwajibika kwetu kama watanzania na kulinda rasilimali zetu.

Kampuni ya Green Mile ilifungiwa lakini ajabu ni kuwa wanaendelea kutamba Tanzania yetu.

Kinachosikitisha, mawakili/watetezi wa wauaji hawa ni watanzania.

Kifupi, habari kuhusu kampuni hii hazijaanza leo na nakumbuka Msigwa alipiga sana kelele 2014. Ni nani aliwarudishia leseni waarabu hawa?

aa2a78f06871e4d22b2221acb664e36b.jpg

VIDEO inayosikitisha:

Mataifa mengine yanatushangaa, soma: Leaked Animal Abuse Video Shows Everything That's Wrong with Big Game Hunting

Aidha, SHERIA YA UHIFADHI WA WANYAMAPORI NAMBA 5 YA MWAKA 2009 ina ufafanuzi wa wazi kabisa juu ya vitendo vya kihalifu kama hivi (nimeambatanisha PDF version yake).

Wanaua hadi ndege ambao wanapatikana Tanzania pekee, wanataka tuwaachie nini wajukuu zetu?

Kumgonga mnyama na gari ni uwindaji huu?

1408119624282525.png

===

The video is apparently a promotional tool for Green Mile and features “highlights” from the United Arab Emirates-based company’s 2012 hunting season. Highlights include shooting wildlife from moving jeeps, running over a baby gazelle with a jeep, letting young children shoot at animals and capturing a baby zebra and holding it while it cries. The hunters regularly watch animals writhe and slowly die, and animals are chased with trucks and shot at from close range.

These abuses were revealed in March 2014, but being well-connected politically, Green Mile kept its hunting license until July when Tanzania’s Minister of Natural Resources and Tourism, Lazaro Nyalandu finally revoked the company’s permission to hunt.

===

Magufuli tusaidie, nani aliwarudishia leseni watu hawa?

Serikali iliyopita ilipigwa dongo kuwa imefumba macho Tanzania ikipoteza idadi kubwa na wanyama na gazeti la Guardian la UK - Tanzania turns a blind eye to poaching as elephant populations tumble

Ni matumaini yangu kuwa tunazinusuru mbuga zetu na wawindaji majangili kama hawa.
 
Attachments

  • Infringements - Swahili Version.pdf
    86.2 KB · Views: 617
Mh Magufuli naomba sasa tulipe jeshi jukumu la kulinda wanyama wetu vinginevyo wanyama watatoweka kabisa.
 
Hawa waarabu HAWAFANYI hivyo bila ya sheria. Wanalipia malipo ya kuwinda kila aina ya mnyama. Sheria yetu ya nchi inaruhusu, kuna kitu kinaitwa ANIMAL CULING ( kupunguza idadi ya wanyama kwa kuwawinda) ndio hapo serekali inatoa vibali na kuruhusu uwindaji.

Hebu angalia hiyo link hapo juu utawaona wamarekani nao wanawinda. Idadi kubwa ya wauwaji wanyama wetu wanaokuja kujinufaisha na uuwaji wa wanyama ni waz unguarded, na wamekuwa wakifanya hivyo zaidi ya miaka 100 na hakuna anayewasema, lakini akifanya mtu mwingine tunawasakama.

Ni bora tukalipinga hili jambo kwa wote wanao kuja kuuwa wanyama wetu kama starehe. Kama ni upunguzaji nasimama waruhusiwe watanzania wenye shida ya kitoweo.
 
Nonsense! Kuwinda ili kupunguza wa nyama una kikomo na unalenga wa nyama fulani. Hapa tunaona wanyama wanauawa bila kujali ni mnyama gani na hata vitoto. Hili halikubaliki kwa wawindaji waarabu au wamarekani. Hapa kuna ushahidi tosha kuhusu jinsi hawa waarabu wanavyo abuse wanyama wetu kama unao ushahidi wa wamarekani kufanya hivyo weka hapa na sio kutoa utetezi usio na hoja. Huwezi kumpiga mkeo kwa sababu jirani anafanya hivyo.
 
Back
Top Bottom