Je, Uwezo wa mtu kufikiri na kutenda, unaendana na nchi aliyopo?
Kuna mambo ukiyatafakari saana, unaweza kuona kwamba, uhusiano kati ya mtu uwezo wake wa kufikiri na kutenda kunatokana na nchi aliyopo,kuna nchi zina watu wasomi, ambapo mambo yao huendeshwa kitaalamu na kiuweledi wa kutosha, lakini zipo nchi ambazo nazo zinawasomi wa level ileile, lakini kwa jinsi zinavyoendesha mambo yake utadhani hao waliosoma, ni sawa na jamii ya wasiosoma tu na kwamba hawana msaada, msaada wao ni kudhibiti kila anayehoji uwezo wao wa taaluma zao! hii ni mbaya sana
Changamoto nyingine ni kwamba, Zipo nchi ambazo zinajivunia mabadiriko makubwa yanayotokana na matunda ya watu wake kwa kazi nzuri wafanyazo wasomi wake na kunufaisha zaidi watu woke, tofauti kabisa na ilivyo kwa baadhi ya nchi ambazo wasomi wake hawana msaada kabisa kwa watu wao, kazi yao na sifa yao kubwa, hujivunia kwa kujiongezea mishahara tena nyongeza hiyo ya mishahara, haitokani wa weledi na matunda bora ya kazi zao maofisini, ni kuwachangisha tu wananchi na kisha wao kujiongezea mishahara na kupangiana safari mbalimbali nje ya nchi zao na kujlipa posho kubwa kubwa, wakati huohuo nchi utakuta inautajiri mkubwa wa rasilimali asili, Cha kushangaza zaidi, hata wale ambao hawana elimu kubwa kwenye nchi hizo zenye msaada wa wasomi wake, uelewa wao katika mambo mbalimbali juu ya kinachoendelea katika nchi zao, unaweza kudhani elimu zao ndogo, ndiyo uwezo wa watu wenye elimu kubwa kwenye taifa lingine.
Nchi, za watu kama hao, kila jambo hupimwa kwa kutumia vigezo vya leo na miaka mingi ijayo, ikilinganishwa na baadhi ya nchi zenye watu wenye uwezo mdogo wa kufikiri na kutenda, ambapo watu wake hupima mambo yake kwa kutumia vigezo vya leo na kesho tu! elimu ya namna hii hauwezi ukasema imemkomboa mwananchi na kiongozi huyo
katika nchi watu wake ambapo fikra zao na utendaji kazi ulio chini mno, raia wake ni kama kuku broiler, mchinjanji huchukua kuku mmoja baada ya mwingine na hakuna anayepiga kelele, wote ni kimya wakiwa wamepanga foleni zamu kwa zamu
Nchi kama hizo, maendeleo kwao ni magumu saana na hata yakipatikana ni ya maumivu makubwa kwa makundi makubwa ya watu, huku kundi dogo likibadirisha vitu vya anasa kila uchwao na kundi hili kuishi kama liko peponi
Shida zinazotukabiri hasa katika nchi zetu hizi ni uhasama mkubwa uliomo katika vyama na katika suala zima la siasa!
Hatujawahi kabisa kukubali uwezo binafsi wa mtu na tukajivunia watu hao ndani ya chama hata nje ya chama, hiki ndicho kinachotafuna mataifa yenye watu aina hizi, Kwenye mataifa yenye watu wanaokubali uwezo wa mmojammoja, watu wenye uwezo mkubwa hutunzwa kama mboni ya jicho kwa ajili ya mambo ya nchi zao, tofauti na nchi hizi zingine ambapo mwenye uwezo mkubwa anaweza kutafuutwa ikiwezekana apotezwe! Jamani haya mambo yapo mjuwe!
Kwa mantiki hiyo, mataifa yenye watu kama hao, wasiokubali uwezo wa watu wao, huishi kwa mashindano na kwa makundi makundi ya kisiasa ili kusaka madaraka pasina kujali uwezo wao wa kushughurikia kero za wananchi
Na kwa kuwa nchi kama hizo, wananchi wake kulingana na nchi waliopo, huwa kama kuku broiler, muda ukifika wa uchaguzi huletewa pumba tena ili mchinjaji akiwa anachinja, wengine wakiendelea kudonoa pumba mdogomdogo wakisubiri maumivu yao
Je, ni kweli sasa, kuna tofauti ya kufikiri na kutenda kulingana na nchi uliyopo?
Mwingine anaweza kusema, Wa Africa ndivyo tulivyo, lakini kuna waafrica ambao wako nje ya bala la Africa wakifanya mambo makubwa sana, tunayo mifano mingi kwa watu wenye ngozi nyeusi waliowahi kufanya mambo makubwa na yakawa historical mpaka leo!