Uwezo wa kuongea kiingereza utumike kuwakata wabunge na madiwani

Big Eagle

JF-Expert Member
May 3, 2020
592
623
Kwasasa Tanzania yetu ukienda kwenye interview hata Kama nafasi ya wahitimu wa darasa la saba mnachujwa kwa kufaham kiingereza inakuaje uko kwa madiwani na wabunge interview zao zinakua za kiswahili wakati ni nafasi muhimu sana.
 
Serikali ijayo Wiele shule za maalum kila kata kwa watoto wanaopata alama za juu. Shule hizi zianze kuongea Kiingereza kama lugha uingiapo shuleni. Na kuwe na maabara za sayansi kuanzia sekondari.

Si uhamie uingereza ili uwe na kiingereza, nyie ndo watumwa wa fikra, miaka yote tunasema kiswahilinkitumike kuwafundisha wanafunzi lakini nyie na kiingereza tu, hicho kiingereza si ukisome kwa muda wake ukikitaka?

Mbona kuna waRusi hawajui kiingereza na wafaransa pia waeshia lakini wameendelea,
Nyie masikini wa africa ndo mnashebedua viuno eti kiingereza,
 
Mimi Mkenya hapa, napita kimya nikisoma nyuzi zenu hizi kila siku mnatuponda kwa kuwazidi uwezo wa kuongea kingereza, naona taratibu mumeanza kutia akili na kuelewa umuhimu wa hii lugha ya malkia hapa duniani.

Wachina, Wajapani, Warusi n.k. kote kote wanahangaika wakikeshea kusoma kingereza, mwafrika umekwama kisa uzembe huku ukijiliwaza eti ni lugha ya mkoloni, ilhali kila ulicho nacho hapo kimeandikwa kwa kingereza, simu, tarakilishi, na bidhaa zote unazoagiza na hata unazozalisha.

Mikataba ya madini na kila aina ya raslimali yote imeandikwa kwa kingereza, na ulivyo mzembe kwenye kusoma mikataba ya kingereza huwa unaomba uonyeshwe wapi pa kutia saini tu basi.
 
Ukizingatia kwamba Jumuia ya Madola ilitawala 3/4 ya dunia. Kiingereza ni muhimu kwa mawasiliano duniani. Unahitaji mawasiliano katika biashara na uchumi uanategemea biashara.
 
Kwasasa Tanzania yetu ukienda kwenye interview hata Kama nafasi ya wahitimu wa darasa la saba mnachujwa kwa kufaham kiingereza inakuaje uko kwa madiwani na wabunge interview zao zinakua za kiswahili wakati ni nafasi muhimu sana.
Sisi hapa kwetu tunatumia kinyasa na kiwemba, hicho kiinglishi tupa kuleeee

Sasa tutapiga kampeni kwa kiingereza kwamba diwani wetu awe anauwezo wakutusikiliza na kutuletea maendeleao lakini tusimchagua tu kwasababu hajui kiingereza ambacho hata wananchi wa Kata yake hatukijui.
 
Jamani kutumia kingereza kama chujio kunamtia kwenye hatihati mgombea urais kwa tiketi ya CCM.
Kwa Rais ni rahisi manake kazungukwa na wataalamu lukuki, anaweza pata msaada, mashaka yangu siku zote uwa ni Kwa madiwani ambao wao ndio wanakaa kwenye tender boards za local governments.. tender documents nyingi zinajazwa Kwa kimombo,wasipojua lugha si ni rahisi kuingizwa chaka!?
 
Serikali ijayo Wiele shule za maalum kila kata kwa watoto wanaopata alama za juu. Shule hizi zianze kuongea Kiingereza kama lugha uingiapo shuleni. Na kuwe na maabara za sayansi kuanzia sekondari.
Hii nimeichukua pamoja na tehama.Ni mambo muhimu sana.Kuwekeza katika elimu ya utotoni-Early childhood education.
 
Kwasasa Tanzania yetu ukienda kwenye interview hata Kama nafasi ya wahitimu wa darasa la saba mnachujwa kwa kufaham kiingereza inakuaje uko kwa madiwani na wabunge interview zao zinakua za kiswahili wakati ni nafasi muhimu sana.

Kwa sababu wewe unajua kuongea kiingereza?

Ondoa hii "colonial mentality" yako, haifai...

Vikao vya Mabaraza ya madiwani (Full Council & Committees) huendeshwa kwa lugha ya kiswahili...

Tusiwanyime watu haki ya kuchagua na kuchaguliwa kwa kigezo cha lugha ya kigeni - Kiingereza.

Wewe pambana, unaweza kushinda tu
 
Si uhamie uingereza ili uwe na kiingereza, nyie ndo watumwa wa fikra, miaka yote tunasema kiswahilinkitumike kuwafundisha wanafunzi lakini nyie na kiingereza tu, hicho kiingereza si ukisome kwa muda wake ukikitaka?

Mbona kuna waRusi hawajui kiingereza na wafaransa pia waeshia lakini wameendelea,
Nyie masikini wa africa ndo mnashebedua viuno eti kiingereza,
Huna ufahamu maana hizi nchi zote ulizotaja wanakijua kiingereza mpaka marais wao!! Fanya research utoke gizani.
 
Kama huku Bungeni wangekuwa wanatumia kiswahili sawa.. Ila uswahili kibao na matusi yake...waacheni watu
 
Huna ufahamu maana hizi nchi zote ulizotaja wanakijua kiingereza mpaka marais wao!! Fanya research utoke gizani.

Acha ujinga si lazima wananchi wote wajue, unayoyasema ninkma nilivyosema ni lugha ya kujifunza lakini sio kugha ya taifa lao au ya kufundishia.
Hao maraisi kujua kiingereza ni somo la lugha tu, kuna mainginia wachina na wasomi wengi lakini hawajui kiingereza, kwa hiyo usikariri na wanaendesha uchumi wa nchi zao.
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom