Uwezo wa kuongea kiingereza utumike kuwakata wabunge na madiwani

HUO NI UTUMWA.
iwe ni lugha ya nyongeza.
wote tukiongea kiingereza kiswahili ataongea nani?.
Sikijui kiingereza na wala sikipendi.
Ila "HAUWEZI KUNISEMA KIINGEREZA"

Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Lakini enzi zetu English ilianza kufundiswa shuleni darasa la tatu.Ukiingia Darasa la tano masomo yote ni katika English isipokuwa somo la kiswahili
Alieua English ni Mwl.Nyerere, japo masomo ya secondary schools hadi vyuoni ni English.
Hakuna utashi wa kisiasa,lakini ukisubiri hao wanasiasa watakuchelewesha wakati watoto wao wapo shule bomba ndani na nje ya nchi.
Kama kuna ka uwezo wekeza katika elimu ya watoto wako.
Kutokana na ulichoeleza je,uwezo wenu wa kumudu kuzungumza hiyo lugha ulikuaje katika enzi zenu.
 
Kwasasa Tanzania yetu ukienda kwenye interview hata Kama nafasi ya wahitimu wa darasa la saba mnachujwa kwa kufaham kiingereza inakuaje uko kwa madiwani na wabunge interview zao zinakua za kiswahili wakati ni nafasi muhimu sana.
tuanzie U-Rais, asiyejua aenguliwe
 
Kwasasa Tanzania yetu ukienda kwenye interview hata Kama nafasi ya wahitimu wa darasa la saba mnachujwa kwa kufaham kiingereza inakuaje uko kwa madiwani na wabunge interview zao zinakua za kiswahili wakati ni nafasi muhimu sana.
Kwani tunatafuta viongozi wa Uingereza?
 
Kutokana na ulichoeleza je,uwezo wenu wa kumudu kuzungumza hiyo lugha ulikuaje katika enzi zenu.
Enzi hizo English ilikuwa inatumika ktk mazungumzo shuleni na pahala pa kazi,ni wazi tulikuwa na mazoea ya kutumia lugha hiyo hadi grammar.
Lakini kuna watu wengi ambao hawakusoma shule ilikuwa kikwazo.Lakini kijana aliemaliza darasa la nane angeweza kuwa hata translator mahakamani.
Kwenye secondary school majority ya walimu walikuwa wazungu tena waingereza au Marekani na Canada ,India na ilikuwa ni marufuku kuzungumza lugha nyingine kwa muda mwingi wa masomo na prep.
 
But Kiingereza si kama suti ambayo mtu aweze kuacha kuvaa isiwe tatizo.
Kiingereza ni kama almasi kwenye ncha ya mtaimbo iwezayo kupenya miamba kupata madini muhimu. Hakikwepeki kwa kisingizio chochote. Kiswahili ni chetu pia...

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
Umeisema kweli ndivyo ilivyo kiingereza hakikwepeki tena hata wachina na wafaransa wanaangaika kujifunza
 
Enzi hizo English ilikuwa inatumika ktk mazungumzo shuleni na pahala pa kazi,ni wazi tulikuwa na mazoea ya kutumia lugha hiyo hadi grammar.
Lakini kuna watu wengi ambao hawakusoma shule ilikuwa kikwazo.Lakini kijana aliemaliza darasa la nane angeweza kuwa hata translator mahakamani.
Kwenye secondary school majority ya walimu walikuwa wazungu tena waingereza au Marekani na Canada ,India na ilikuwa ni marufuku kuzungumza lugha nyingine kwa muda mwingi wa masomo na prep.
Kwahiyo tunaweza kusema mliyosoma kipindi hicho mnamudu kuonge kiingereza vizuri?
 
Ili iweje! Wananchi wote wanazungumza kiswahili sisi tuwapitishe viongozi wetu kwa kizungu?

..nadhani ni lazima tuelewe kwamba Kiingereza ni fursa.

..it is an added advantage ktk soko la ajira la ndani na nje ya Tz.

..tatizo ni kwamba SIASA imeingilia mjadala huu, lakini tukiweka siasa pembeni Kiingereza hakiepukiki.

..kuna nchi kama INDIA wamefaidika sana kwa wasomi wao kuimudu lugha ya Kiingereza.

..kwa mfano hapa Tz tuna mkongo wa taifa, sasa tungekuwa na vijana wanaoweza kuongea kiingereza vizuri tungeweza kufungua call centers ambazo zinafanya kazi za customer services kwa makampuni yaliyoko nchi za mabeberu. Na call center haihusishi wapokea simu tu inahusisha na wahandisi wa mambo ya tehama.

..mimi nimekutana na wanasayansi wa Kichina na Kihindi ktk kongamano moja nje ya nchi. Wale wachina walikuwa very knowlegeable lakini walikwazwa na lugha ktk kuwasilisha mada yao. Wahindi wao walipeta tu kwasababu ya kukimanya Kiingereza. Hata scientists wa Kijerumani walikuwa wanabonga Kiingereza.

..Kwa kifupi Kiingereza ndiyo SARAFU ya elimu na maarifa ulimwenguni. Kama unataka kupambana ktk dunia ya utandawazi lazima ujue Kiingereza.

NB:

..hata Kiswahili, pamoja na kuwa ni lugha ya taifa letu, lakini hatukiheshimu na kukizungumza kwa ufasaha.

cc MK254
 
Back
Top Bottom