Uwezo wa kufikiri na mafanikio ya kimaisha

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
11,136
19,871
Kufikiri ni utumiaji wa taarifa za ufaham kuhusu jambo fulani ili kufikia hitimisho fulani.
Ni dhahiri kuwa maisha ya kisasa yamemwingiza mwanadam katika ushindani ambao atake asitake, lazima ashiriki ili kujikim kwa kipato na maisha kwa ujumla. Ushindani huu unaelekezwa katika kitu kiitwacho "fursa"
Fursa ni nafasi, eneo au mazingira ambayo huruhusu jambo/kazi fulani kutendeka kiufanisi.
Utumiaji wa fursa hutegemea na ubunifu asilia au wa kujifunza wa mhusika ili kuwa tofauti na wengine ili kuteka soko au huduma fulani
Fursa hizi ni kama:-
1 . kazi (ajira)
2. Biashara
3.utaalam
4. Siasa n.k
Kushindwa kufanikiwa kimaisha ni dhahiri ya uwezo kuwa mdogo kuhimili changamoto husika japo sababu nyinginezo zaweza.
Vijana wengi wamekuwa wakitoa sababu nyingi tegemezi ambazo zimewafanya wawe na ustawi hafifu kimaisha, sababu hizi ndio huwapumbaza kwani huficha udhaifu wao ambao ungeweza kurekebishika badala yake hutupia lawama wengine mfano kuilaumu sana serikali na kusubiri utendewe.
Elewa haya:-
1.pesa ni matokeo ya kazi/shughuli ufanyayo, hivyo usiangalie kwanza pesa angalia kazi/shughuli.
2. Kuiga mambo huziba kipaji/ubunifu wako, tumia ulicho nacho akilini sio alichonacho yule.
3. Kubali kuwa wewe bado unanafasi ya kufanikiwa japo bado hujafanikiwa.
4. Mwangalie kila mtu kama fursa yako, jenga heshima kwa kujali na kusaidia kadri.
5. Usitumie asilimia kubwa ya maamuzi kupitia ushauri wa rafiki yako, hapo ni sawa na kwamba rafiki yako anaamua mambo yako yote.
6. Kiri udhaifu wako.
7. Tathimini uwezo wako.
8. Fanya kazi zako kwa ari.


Usifikiri kuna siku utaombewa kanisani/msikitini ili ufanikiwe. NI WEWE NA FIKRA ZAKO= success or failure.
 
Back
Top Bottom