Uwezo tunao, tunahitaji nini zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwezo tunao, tunahitaji nini zaidi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Annina, Jan 3, 2010.

 1. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Inawezekana suala hili limesha ongelewa humu jamvini, mniwie radhi kama ninalirudia katika namna ya kuwarudisha nyuma. Siku zote nimekuwa na wazo la kuunganisha nguvu za kuweza kusaidia kutatua matatizo katika jamii yetu japo kwa kiasi kidogo.

  Kupitia mijadala mbalimbali hapa JF nimeona wengi wanaguswa na hali mbaya ya maisha inayotukabili wananchi wa kawaida. Ni wazi serikali yetu kwa sababu mbalimbali ambazo zimejadiliwa pia humu inashindwa kutimiza majukumu yake ikiwa ni pamoja na huduma za kijamii kama vile afya (mfano wa post ya Mwanakijiji kuhusu ward ya akina mama katika hospitali ya temeke), maji, usafi wa miji yetu nk nk.

  Wazo langu ni kuwa, badala ya kuishia kujadili tu na kuacha hali iendelee kama ilivyo, tunaweza kujipanga tukabadili hali kwa kiasi fulani pamoja na uwezo mdogo tulionao. Tunaweza kupitia mkuu wa kaya, tukajipanga na kuchangia vitanda katika baadhi ya hospitali, au madawati, vitabu katika shule au kufanya usafi katika baadhi ya maeneo, au chochote chenye kugusa maslahi ya umma kadri tutakavyoona inafaa kwa wakati huo. Pia tunaweza kuandaa vijarida (popular version) vya elimu ya uraia katika minajili ya kuelimisha umma.


  Annina
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Umeongea jambo la maana annie....
  Ni hiccho ndo najaribu kukifanya humu..
  Kuwa encourage watu wenye uwezo wa kulipia
  matibabu kwa mfano,walipie ili mzigo upungue kwa serikalii.....

  From history utaona masuala ya harakati na movements huwa
  hayafanikiwi sana kwa sababu binadamu tupo tofauti na common sense
  is not common....

  Ili serikali iweze kutusikiliza ni lazima sisi wananchi ndo tuwe
  na nguvu ya kuilazimisha itusikilize,mfano marekani obama lazima
  awasikilize walimchagua kwa sababu hata pesa za uchaguzi walimchangia
  wakati sisi huku mtu anasubiri pilau ya mgombea halafu unategemea nini???

  Watanzania tukijihamasisha kubeba mizigo yetu wenyewe
  na hata ikibidi ku ignore hiyo serikali then one day kutakuwa
  hakuna jinsi,watatusikiliza tu wapende wasipende.

  But kwanza tuje na solution bila kuihusisha serikali na inawezekana sana tu.
   
 3. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Siku serikali ikiacha kupokea kodi tukawa na local tax pekee kwa ajili ya mambo yetu ndio tutaacha kuihusisha na mambo yanayohusu maisha yetu..kama elimu, afya, maji, barabara etc. period!

  siku tukiacha kuwalipa wabunge kwenda dodoma, mawaziri, PS, nk. tukawalipa madiwani wa mtaani kwetu tu, tukaendesha shule na hospitali zetu mtaani kwetu kwa standard zetu mtaani ndio tutaacha kuihusisha serikali

  As long as wanapokea tax lazima wakubali responsibility..huwezi kuwa unalipwa bila responsibility sijawahi kuona popote mimi

  Nakubaliana na wewe watu kujitegemea lakini serikali ikubali kutopokea chochote kutoka kwetu kwanza au tusiwape chochote ndio tujitegemee.
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kama serikali ingekuwa inatutegemea kwa asilimia mia moja
  hata upuuzi huo wanaoufanya wasingefanya.....
  Serikali inawategemea zaidi wafadhili na ndio inao waogopa
  kwa ssababu wanafadhili sehemu kubwa ya bajeti na upuuzi mwingine....

  Usisahau kuwa watanzania wanaolipa kodi ni milioni moja tu
  au mbili na hilo limeshatamkwa mpaka na mkullo....

  Sasa hapo pata picha.
   
 5. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nashukuru tupo pamoja. Kwa mfano, gharama za wanafunzi kukosa vitabu na mazingira mazuri ya kujifunzia ni kubwa kuliko tunavyoweza kufikiria. Mwanafunzi anaesoma mazingira magumu huku akiona kuna wanaosoma kwenye mazingira mazuri atakata tamaa na kuathirika kisaikologia - hapa ndipo kundi kubwa la watanzania tulipo, tumeaminishwa (kutokana na mazingira) kwamba hatuna cha kufanya mbele ya serikali hivyo tusubiri kudra za Mungu!

  Hatuhitaji pesa nyingi kusafisha mitaro inayotuzunguka, ni kwa manufaa yetu wenyewe maana mwisho wa siku ni sisi tutakaopata magonjwa ya kuambukiza na tunajua huduma za afya zilivyo mbovu kwa mwananchi wa kawaida - ni vyema kuchukua tahadhari. Kuna mtaro upo karibu na TMJ hospital kila nilipokuwa napita nilisikia kizunguzungu - nao wanasubiri serikali iwasafishie!

  Tukikubaliana na wazo hili, tunaweza kuchagua maeneo ya kuanzia - hata tukiiwezesha hospitali moja na shule moja ni hatua kuliko kuendelea kulalamika wakati mama na dada zetu wanateseka, watoto na wadogo zetu wanakaa chini kwenye darasa la vumbi. Tusisubiri kupata kikubwa, tuanze na kidogo tulichonacho.
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2010
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ha! Kama wanategemea wafadhili waache kututoza kodi "Income tax" wafanyakazi wote Tanzania, wafanyabiashara wote, wakulima wote (mauzo ya mazao)...wanatutegemea sana tu ...

  wafadhili wanawategemea wao serikali kwakuwa ni wajinga wanatunyonya bila kufahamu...kwenye mikataba na mauzo ya resources zetu..don't you see!

  Watanzania wanaolipa kodi ni wote...unless umeacha kufanya consumption siku hizi umesahau VAT? kila nguo, machines, nk unayonunua kuna kodi ya VAT sikuelewi ndugu..
   
 7. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nadhani wote tushiriki vizuri uchaguzi ujao kwa uhuru na tupige kura bila unafiki. kama chama fulani hakikuridhishi kiache chagua kingine. sio ukichague kisha uanze kulialia hapa JF. fursa pekee iliopo ni kujitokeze kupigakura na upige mwenyewe sio upigishwe na kanga, kofia nk.
   
 8. Annina

  Annina JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2010
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 437
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mgombea Ubunge,
  Kwa mtazamo wangu suluhu sio kupiga kura pekee, kuna haja ya kueleweshana juu ya umuhimu na utayari wa kuchangia maendeleo yetu. Naona mwenzetu unawaza masanduku ya kura tu - I dont blame you...
   
Loading...