Nia yangu ni kuhoji matumizi yasiyo na tija ya Halmashauri ya Ilala. Kama uko Dar utakuwa umeyaona mabango ambayo yamegharimiwa na Halmshauri ya Ilala yakiwa na ujumbe wa kumpongeza mwenyeketi, makamu mwenyekiti na viongozi wengine wa chama kwa kuchaguliwa tena.
Kwangu mimi hili ni moja ya matumizi ya kijinga na yasiyo na kichwa wala miguu yanayofanywa na Halamshauri zetu.
Meya Jerry Silaa na madiwani wake wanaonekana bado wanaishi kwenye zama za chama kimoja. Unatumiaje kodi za wanachadema, wanaNCCR, wanaTLP, wanaUDP na hata wengine wasio na vyama kumpongeza mwenyekiti wa CCM?
Hivi inakuwaje hatuna pesa za kununua dawa kwa ajili ya hospitali ya Amana na zahanati ya Mnazimmoja lakini tuna pesa kwa ajili ya mabango ya kumpongeza mwenyekiti kwa kuchaguliwa kitu ambacho kila mtu alikitarajia? Meya Silaa kwanini unatumia pesa zetu kwa ajili ya political mileage?
Kwa style hii ya uongozi tulionao then ndoto za maendeleo zinapaswa kufutwa vichwani mwetu.