Lole Gwakisa
JF-Expert Member
- Nov 5, 2008
- 4,764
- 2,347
Kati ya mafanikio ya mwanzo kabisa ya Rais Magufuli ni hili alilo ahidi juzi kuwawezesah wakandarasi watanzania kujijenga kiuwezo ili waweze kuchukua kazi kubwa kubwa.
Si wengi, hata huko mawizarani wanaoelewa maana halisi ya msimamo huo.
Wiki iliyopita , akifungua mkutano wa mashauriano kati ya makandarasi na serikali, Rais Magufuli aliahidi kusaidia kuwajengea uwezo makandarasi wa Kitanzania ili si tu wakue kiuwezo bali waweze kutekeleza miradi mikubwa ya kiserikali.
Maana halisi ya msimamo huu abao wakandarasi waekuwa wakielimisha jamii ni kama ifuatavyo:
Tatizo kubwa inaloendekeza waajiri(watoa kazi) kupendelea wakandarasi wa nje ni pamoja na mengineyo,rushwa.
JPM alisema wazi kuwa atakula sahani moja na wakndarasi/waajiri wanaoongeza gharama za kazi kwa kuongeza "cha juu" hivyo kuongeza gharama za ujenzi pasipo sababu ya maana.
Nami nampongea sana Dr John Pombe Joseph Magufuli, matokeo ya uamuzi huu yataonekana katika kipindi cha miaka kumi ijayo, pole pole ndio mwendo.

- Fedha za faida ya makampuni ya ujenzi itabaki nchini. Sasa hivi makampuni makubwa ya kigeni huondoa mara moja salio la fedha zote wanazolipwa na kuzipeleka kwao. Hata hizi kampuni za wenzetu waAsia wakipata fedha huzikimbiza Uingereza na Canada wanakokimbilia mara tu wakistaafu.
- Kampuni za watanzania watawekeza umu humu nchini ikiwa ni pamoja na kuongeza mzunguko wa fedha.
- Kuongeza ajira nchini, ikumbukwe kuwa haya makampuni ya kigeni huajiri wageni katika kuziongoza kampuni zao, jambo ambalo si lazima tukiwa na kampuni zetu za wakandarasi.
- Kupunguza gharama za ujenzi, Kuna kitu kinaitwa overheads, hizi ni gharama za kusimamia kampuni wakati wa ujenzi. Inategemewa kuwa gharama hizi zitapungua kwa kiasi kulingana na kupungua kwa wageni ambao gharama za kuwatunza ni kubwa nchini.
- Nchi kama China , imejenga kada nzuri sana ya wakandarasi wao nchini kwao kiasi ambacho hawahitaji kampuni toka nje ya china kutekeleza miradi mikubwa ya aina yoyote, hivyo kuongeza usalama wa nchi yao.