Uwezekano wa wewe kupona kwenye ajali ya ndege, huu hapa

JAMII-ASM

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
1,305
524
Mtaalam wa ki-Russia kafanya utafiti na kuibuka na muundo mpya wa ndege..muundo ambao haujawahi kuonekana duniani.Muundo huu kidogo unataka kufanana na Apollo capsule iliyotua katika mwezi.
Lakini hii inatumika wakati wa ajali tu. Chumba cha abiria ''fuselage'' kinajitenga na cockpit...na kuwa vitu viwili tofauti. Halafu ''fuselage'' na abiria ndani yake inatua baharini au ardhini kwa parachute.
https://www.google.co.tz/url?sa=t&r...BoQl0iIv0-d_UVobylT5AQ&bvm=bv.112064104,d.d2s
Kama ataweza kufikia hatua ya kuitengeneza ndege hii basi ataokoa maisha ya wengi. Ajali za ndege ni nadra lakini ikitokea wanaopona wanahesabika.
Hii video hapa chini inaonesha hatua muhimu ...jinsi ndege hii itakavyoweza kuokoa maisha ya abiria baada ya ndege kupata hitilafu angani
VIDEO OF PROTOTYPE

Hawa warusi sasa wameamua kufunguka!hapo awali ilikuwa kila kitu kuzuri ni USA
 
Hawa warusi sasa wameamua kufunguka!hapo awali ilikuwa kila kitu kuzuri ni USA
Kama utakumbuka wao ndio watu wakwanza kurusha chombo angani chenye abiria/mwana anga ndani yake ''VOSTOK I''.
 
Ndege mara nyingi huwa ni more safe mpaka ukiona imeangua huwa ni technical problem mara nyingi mara chache ndiyo inakuwa hujuma/ ugaidi n.k

so wasiwasi wangu ni kuwa kama ni technical problems i dont think kama this kind of evacuation prototype waliyokuja nayo warusi itawork

however lets wait
 
Inawezasaidia hasa inapofikia hatua rubani anaona kabisa sasa ndege inaanguka hapo ata press button ngoma iachane au wanaweza hata wakafanya iwe auto au computerised pindi ionekanapo ndege inaaguka basi inajigawa
 
Hii design sio ''terror proof''. Likitegwa bomu ndani ya hii ndege na likalipuka mid-air hakuna wa kupona.
 
Wenzetu kila problem wanaifanyia utafiti. Sisi ajali za barabaani tu zinatushinda na kila siku watanzania wenzetu wanapoteza maisha
 
Inawezasaidia hasa inapofikia hatua rubani anaona kabisa sasa ndege inaanguka hapo ata press button ngoma iachane au wanaweza hata wakafanya iwe auto au computerised pindi ionekanapo ndege inaaguka basi inajigawa
Design bado ina mapungufu mengi. Kuna uwezekano wa hiyo ''detachable cabin'' kutua katikati ya makazi ya watu au eneo la viwanda.Hiyo cabin inavyoonekana itakuwa inaelea kama puto na kutua popote.
 
Hilo ni bonge la invention aisee..itasaidia kupunguza idadi ya vifo vitokanavyo na ajali za ndege.
 
Design bado ina mapungufu mengi. Kuna uwezekano wa hiyo ''detachable cabin'' kutua katikati ya makazi ya watu au eneo la viwanda.Hiyo cabin inavyoonekana itakuwa inaelea kama puto na kutua popote.
Ni bora kuelea baharini au kuangukia msituni rescue inaweza kufanyika kwa muda muafaka.
 
Ni bora kuelea baharini au kuangukia msituni rescue inaweza kufanyika kwa muda muafaka.
Ndivyo wanavyodhani.kuwa uwezekano mkubwa ni kuangukia sehemu za baharini au msituni...lakini inaweza kuangukia kiwanda cha nyuklia.
 
Kwa mujibu wa video marubani wao hii chocho haiwahusu.au watatoka flight deck??
 
Ndege mara nyingi huwa ni more safe mpaka ukiona imeangua huwa ni technical problem mara nyingi mara chache ndiyo inakuwa hujuma/ ugaidi n.k

so wasiwasi wangu ni kuwa kama ni technical problems i dont think kama this kind of evacuation prototype waliyokuja nayo warusi itawork

however lets wait
marubani wengi wa ndege za kivita wanapona kwa mifumo inayofanana na hiyo.
 
ni wazo zuri..
vp kuhusu vile vipande vengine vikienda kudondokea kwenye makazi ya watu si vinaweza kuleta madhara..
 
Naamini itaongeza gharama kubwa hasa katika ununuzi wa ndege hizo na ticket kwa habiria!.Makampuni ya dunia yanapendelea cheap economy plane. Pia changamoto itakua bado kwa rubani kama tatizo litatokea ghafra maana yake Yeye rubani atakubali kufa ili aponye abiria ,maana Yeye atakwenda na kipande chake na abiria pia wana cha kwao! Ikumbukwe akili ya Dreva yeyote duniani ni kupona Yeye kwanza.
 
Back
Top Bottom