mzushi
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 3,094
- 4,251
Kutokana na kashfa kubwa ya Escrow kuitafuna Serikali na Vigogo wengi kuhusika mfupa huu ni mgumu sana Kwa Jk kuumeza :mosi JK hatokubali tena Serikali ianguke mikononi mwake na kwa kuwa muda wake wa kukaa madarakani umefikia kikomo,Kitakachofanyika ripoti haitasomwa kwa zengwe la mahakama na hiyo moja kwa moja itasababisha Mizengo Pinda kukosa makali ya kuwa Waziri mkuu na wengi wa wasaidizi wake hasa mawaziri watakuwa wazito kupokea maelekezo toka kwake .kitakachofuata ni Ripoti ya Daktari itakayomwelekeza Rais apumzike kutokana na Afya yake na yeye ataomba bunge liridhie na madaraka yake yatakaimishwa kwa makamu wa Rais na hapo ndipo utaratibu wa kisheria unasema miezi 3 baada ya hapo ni uchaguzi mkuu .mtaniona mzushi lakini hakika nawaambia mtanipigia salute