GRAMAA
JF-Expert Member
- Nov 1, 2014
- 1,155
- 3,399
Kitendo cha kuwa nimelala usiku mmoja na nikawa naota ndoto na ndani ya ndoto hiyo nikawa nazungumzia matendo niliyofanya miaka mingi iliyopita huko huko ndotoni wakati matendo hayo sijawahi kuyafanya duniani. Kitendo hiki huwa kinanifikilisha sana.
Na baada ya kushituka kutoka ndotoni huwa najiuliza sana kwamba inamaana maisha ya ndotoni huwa ni marefu sana sawa na maisha ya duniani kiasi kwamba yamebeba nyakati zote za maisha yaani wakati uliopita,wasasa na wakati ujao?
Ngoja niweke mfano ili tuweze kuelewana namaanisha nini.
MAZUNGUMZO YAKO UKIWA NDOTONI.
Unaweza ukawa ndotoni na ukawa unaongea na mwenzako huko huko ndotoni mambo yaliyokutokea miaka mingi huko huko ndotoni na ukawa unayakumbuka vizuri tu ila chakushangaza mambo hayo hayajawahi kukutokea katika maisha yako ya duniani.
MFANO UNAOTA UNAONGELEA MAMBO YALIYOPITA UKIWA NDOTONI NA WENZAKO KAMA VILE:-
i/ MUOTAJI: mwaka juzi nilidondokewa na mti mpaka nikalazwa hospitali miezi sita.
Yaani hapa ukiwa ndotoni unakuwa na uhakika kabisa kuwa mwaka juzi ulidondokewa na mti mpaka ukalazwa hospitali na ikiwezekana hata makovu ya kuchubuka unakuwa nayo na unakumbuka tukio zima lilivyokuwa na huwezi kujua kama ndoto mpaka ushituke. Na wakati maisha yako ya duniani hujawahi kutokewa na tukio hilo.
Huo ni mfano tu Ila yapo matukio mengi sana ambayo umewahi kuyaota umefanya ndotoni miaka mingi huku duniani hujawahi hata kuyafanya.
Kitendo hiki kinamaanisha maisha ya ndotoni yamekamilika ndiyo maana yana past,present na future?
Ipi tofauti kati ya maisha ya ndotoni na haya tuliyonayo kama yote yamekamilika kwa nyakati zote muhimu?
Kipi kinachosababisha unaota dakika chache ila ndani ya ndoto unakuwa umeishi maisha marefu sana?
Kipi husababisha kutokea kwa matukio ndotoni ambayo hayajawahi kukutokea duniani?
Au kwenye ndoto napo kuna muda( masaa)?
Karibuni wajuzi wa mambo.