Uwepo wa waandishi wa habari makanjanja ni hatari ndani ya jamii/ nchi

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,330
51,836
WAANDISHI MAKANJANJA NI HATARI NDANI YA NCHI.

Anaandika Robert Heriel.

Leo nitatumia lugha ngumu kidogo, nafahamu nazungumzia kazi za watu ambazo zinawaingizia kipato. Hata hivyo Nia yangu sio kuonyesha ubinafsi, kuwaonea kijicho, isipokuwa kuwataka wabadilike, ili tujenge jamii Bora na taifa bora kabisa.
Nafahamu wapo waandishi WA habari(watangazaji nikiwahusisha), ambao ni wapumbavu na ambao watajifanya kutoa povu hapa. Hawa sitawajali na wala hawatabadili lolote Katika andiko hili. Nafahaku hata wapumbavu wanahaki ya kutoa maoni Yao.

Watangazaji wengi ambao nitawajumuisha katika kundi moja la waandishi WA habari ni makanjanja, watu wa hovyo kabisa,
Taifa au jamii lolote future yake inabebwa na mambo makuu mawili, Mosi, elimu itolewayo shuleni, lapili, ni Media(vyombo vya habari), serikali makini lazima izingatie Maeneo hayo mawili Kwa mustakabali WA kizazi kinachokuja.

Yametokea mapinduzi makubwa katika sekta ya habari, uwepo wa mitandao ya kijamii, ongezeko la vyombo vya habari vya luningani na Redioni vimechochea Kasi ya kusambaa Kwa habari Kwa wepesi na Kwa watu wengi zaidi. Hii inaweza kuwa faida Kwa kizazi hiki lakini pia Kama tahadhari hazitachukuliwa inaweza kuwa hatari Kwa maadili ya jamii.

Watangazaji wengi uwezo wao wa kiakili na elimu upo chini Sana, ninayomifano dhahiri yakutosha Kwa hili nilisemalo, wapo marafiki zangu ambao elimu zao ni Tia maji Tia maji, elimu za kuunga Unga, elimu viraka.
Uwezo wao mdogo wakufikiri hawawezi kuleta Jambo lenye tija ya maana katika jamii.

Mtu yeyote atagundua kuwa Waandishi WA habari wengi siku hizi wamejikuta wakiandaa content nyepesi na zenye maudhui zaidi ya ngono, matusi, umbeya, Kick za kitoto miongoni mwa mambo mengine.

Siwalaumu Kwa kujikita huko kwani uwezo wao ndipo ulipoishia, siku zote waandishi makanjanja hujikita katika mambo mepesi Kwa kisingizio ati ni burudani.

Wao hujaribu kuieleza jamii na kizazi kijacho kuwa Umbeya ni burudani,

Watangazaji karibu wengi sasa, ni hovyo! Hovyo! Hopeless kabisa.

Wao ngono zembe kuielezea kwenye interview kwao ati ni burudani,😥😥
Unakuta liandishi la hovyo linauliza swali Kama hili; Mpaka sasa umetembea na wanaume wangapi?
Shenzi kabisa!!
Na linaloulizwa Kwa vile ni zwazwa linajibu badala ya kumchapa hata kibao kimoja huyo mwandishi Kwa kuuliza maswali ya kipuuzi.
Lengo la kuuliza maswali ya ngono zembe ni nini Kama sio kufanya Kwa kukusudia kuiharibu jamii. Swali hilo kunafanya Vijana wanaokua kuona ngono zembe ni Jambo la kawaida. Serikali nayo imezubaa zubaa haioni Hilo.
Nataka kusema, tunaowajibu WA kulinda jamii yetu Sisi wenyewe. Hatuwezi kuendelea hivi.

Niliwahi kusikia mtu mmoja akihojiwa kuwa aliwahi kutoa mimba, muuliza swali zwazwa na anayeulizwa naye zwazwa likajibu ndio. Yaani mambo mengine ni Fedheha.

Ninyi mnaomiliki vyombo vya habari lazima muelewe kuwa mmebeba dhamana kubwa ndani ya jamii. Tafuteni watu wenye akili zilizojitosheleza, hata Kama Elimu walikimbia basi walau hata akili wawe nazo.

Sasa mnaokoteza wahuni wahuni huko ambao kwao ngono zembe ni sifa, kwao kuzungumzia ishu zisizojenga jamii ndio wanaona huo ndio ujanja na kuwa maarufu, msiajiri vichaa walioathirika kisaikolojia.
Na Kama mtaajiri basi tafuteni Wataalamu wawa-brash saikolojia zao ziwe Sawa.

Wapo waandishi WA habari ambao wanaheshimu kazi zao, wanazipenda na wanatamani Taaluma ya uandishi wa habari iheshimiwe, lakini wanaharibiwa na Hawa wahuni ambao wanadhani kupiga piga mdomo bila akili ndio uandishi wa habari.

Ndio matokeo yake mnahoji watu wanakuambia Yesu alikuwa Tapeli.
Hivi mpaka unamhoji mtu si ushasoma saikolojia yake na kuona mtu huyu akili hamnazo au zinachaji.
Unamhoji alafu unacheka Cheka Kama Mpumbavu.

WAANDISHI MAKANJANJA mubadilike, msituletee mambo ya kipuuzi, jifunzeni kuiheshimu jamii Kama ninyi mmeshindwa kujiheshimu. Heshimuni kazi.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Morogoro
 
Wengi wanajikomba kusubiri kuwa wakuu was wilaya !!! Hovyo kabisa
 
WAANDISHI MAKANJANJA mubadilike, msituletee mambo ya kipuuzi, jifunzeni kuiheshimu jamii Kama ninyi mmeshindwa kujiheshimu. Heshimuni kazi.

Swali la kizushi, bwana Robert Heriel, mtu akikuuliza (wewe) hivi: 'Unafanya mapenzi mara ngapi kwa siku?' Swali hili unalitafsiri vipi na jibu lake litakuwaje?
 
Huwezi uliza swali hilo Kwa mtu ambaye hajaoa wala kuolewa, ni Dalili ya mtu asiye na akili Sawasawa.

Swali hilo lapaswa kuulizwa mtu ambaye yupo ndoani

Au unakuta mtangazaji anamuuliza mtu aliyendoani kuwa; humkumbuki Ex wako?
Yaani maswali mengine unaweza fikiri aliyeuliza ni mwendawazimu
 
Mkuu ndo maana mimi huwa sina muda na hawa waandishi wa hapo bongo kikukweli wanakera sana hata maswali ya msingi hawana, ila nikwambie kitu habari za kimbea, ushilawadu, uongo ,kiki ngono na mapenzi ndo zina mashabiki wakubwa kwa hapa Tanzania vitu serious huwez kuta watu wako interested navyo kabsa
 
Sikuwa kwenye mlengo huo, lengo na nia ilikuwa kujua upana wa neno mapenzi.
 
Nimekuelewa sana mkuu, ila hapa "wapo marafiki zangu ambao elimu zao ni Tia maji Tia maji, elimu za kuunga Unga, elimu viraka" umechemka sana hapo kwenye ELIMU.

Open University of Tanzania kinatoa elimu kulingana na nafasi, muda wako nadhani hata baadhi ya vyuo, so issue ya kuwa na elimu ya aina hiyo isiwe kero kwako mkuu!.

Utoaji wa cream product hautokani na elimu isiyo ya kuunga unga, mfano kuna watu wamekuwa waandishi nguri pasi vyeti vya habari ila baadae wamesoma kozi fupi na leo media inazowatumia inajivunia.

Jambo la msingi tuongelee media erthics kwa waandishi waliosoma na kufuata zile sheria tano nk. Tofauti na hapo mwandishi yeyote anayefanya au kwenda kinyume huyo ni mantanange.
 
Tupo pamoja Mkuu
 
Mkuu ndo maana mimi huwa sina muda na hawa waandishi wa hapo bongo kikukweli wanakera sana hata maswali ya msingi hawana, ila nikwambie kitu habari za kimbea, ushilawadu, uongo ,kiki ngono na mapenzi ndo zina mashabiki wakubwa kwa hapa Tanzania vitu serious huwez kuta watu wako interested navyo kabsa

Ushabiki ni attitude, na attitude inatengenezwa .

Media inayouwezo wa kufanya hayo yote tulitoyataja watu wasiyapende
 
Mwijaku
Soudy Brown
Kamanda Mtimkavu
Diva
Baba Levo
Mchaga Og
Maimatha wa Jesse

Hawa watu wanatakiwa kuwajibishwa
 
Mkuu ndo maana mimi huwa sina muda na hawa waandishi wa hapo bongo kikukweli wanakera sana hata maswali ya msingi hawana, ila nikwambie kitu habari za kimbea, ushilawadu, uongo ,kiki ngono na mapenzi ndo zina mashabiki wakubwa kwa hapa Tanzania vitu serious huwez kuta watu wako interested navyo kabsa
Huu ndo upuuzi mnaosingizia kua umbea ndio unamashabiki wakati hamna content nyingine mbadala..na toka yalivokuja masuala ya kulipwa kwa kutokana na vieswers wa youtube basi watu wanatengeneza contents mbovu hizo hizo wakitegemea small rewards na kutojali madhara kwenye jamii..hii imepelekea mpaka nyimbo zetu wasanii wanoimba upuuzi puuzi ndio wanapewa promo kutokana na kushindanisha viewers..
 
Au unakuta mtangazaji anamuuliza mtu aliyendoani kuwa; humkumbuki Ex wako?
Yaani maswali mengine unaweza fikiri aliyeuliza ni mwendawazimu
Mkuu nowdays kuna jambo mtu anatakiwa kujiuliza, kwa nini waandishi na media kadhaa kubwa zimekuwa nje ya msingi wake?.

Moja ya sababu ni kuwa wamiliki kupitia wakurugenzi wakuu wanahitaji profit, kila mwisho wa mwaka kimahesabu mmiliki anataka kuona faida siyo hasara.

Kwa mantiki hiyo kwenye postmortem watu wanakuna vichwa kujua walaji wanataka nini, kutokea hapo ndipo unakutana na maajabu as yale waliyofanya "wachafu, oh sorry wasafi".

Mtu anajitoa ufahamu kuongea na chizi kwa kumuuliza swali la kijinga chizi anajibu kulingana na uchizi wake. Baadaye anapelekewa mhariri ambaye anaikagua na kusema haifai, anapewa somo na kuambiwa acha iruke tuone reaction ambayo wao inawabeba sababu on that challenge of fight against their members wanaongeza wadau wapya na kupata profit.
 
Huu ndo upuuzi mnaosingizia kua umbea ndio unamashabiki wakati hamna content nyingine mbadala..na toka yalivokuja masuala ya kulipwa kwa kutokana na vieswers wa youtube basi watu wanatengeneza contents mbovu hizo hizo wakitegemea small rewards na kutojali madhara kwenye jamii..hii imepelekea mpaka nyimbo zetu wasanii wanoimba upuuzi puuzi ndio wanapewa promo kutokana na kushindanisha viewers..
Mkuu mimi pia siyo muumini wa kuunga mkono ujinga na kiukweli ninapenda vitu vinavyofikirisha kidgo siyo vitu simple na hii imepelekea hata taarifa za ndani watu wengi kuzipuuza, tuna mambo mengi na makala nyingi za kufanya ili kuelimisha jamii zetu lakini waandishi wengi hawana huo uwezo
 
Back
Top Bottom