beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Wizara ya Madini pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) zitakutana hivi karibuni ili kufanyia kazi malalamiko ya wachimbaji wadogo kuhusu tozo mbalimbali.
Hayo yamebainishwa jana na Waziri wa Madini, Doto Biteko, wakati akifunga Mkutano wa Siku Tatu wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania 2021.
Katika mkutano huo, jumla ya maazimio 17 yalifikiwa ambayo wizara iliwahakikishia wachimbaji hao kuwa itayafanyia kazi.
Biteko alisema anakubaliana na hoja ya wachimbaji wadogo kuwa kumekuwa na tozo zisizotabirika katika halmashauri ambazo ni kikwazo kwa ustawi na maendeleo yao.
Kutokana na hilo, alisema atakutana na waziri mwenzake wa Tamisemi, Selemani Jafo na wakurugenzi watendaji wa halmashauri ili walipatie ufumbuzi.
“Unaweza kukuta tozo zote wanazotozwa wachimbaji wadogo kwenye halmashauri moja zinafika 27, hii siyo sawa kwa sababu tuna wajibu wa kuwalea, kuwahudumia na kuwapa maendeleo wachimbaji wadogo, nitakutana na waziri Jafo na wakurugenzi ili tulipatie ufumbuzi,” alisema Biteko.
Pia aliwataka wachimbaji wadogo kubadilika kimtazamo kwa kujiona hawawezi kupiga hatua na kuwa wachimbaji wakubwa badala yake waitumie mikutano hiyo kama fursa ya kukua kibiashara na siyo sehemu ya kulalamika na kutoa changamoto tu.
“Msipotumia fursa ya utawala huu wa Rais John Magufulu kujinufaisha na kujiletea maendeleo kupitia sekta ya madini, itawachukua miaka mingi kupiga hatua, mnachotakiwa kufanya ni kupendana, mthaminiane, msipigane majungu au kuwapiga vita wanaofanikiwa, mnachimba wote lakini siyo wote mtapata, tuone fahari mmoja wetu anapofanikiwa,” alisema Biteko.
Aidha, aliwataka wachimbaji hao kujiepusha na utoroshaji madini au biashara ya madini feki kwa kuwa mambo hayo yanaichafua nchi. Pia alitaka wasiyavunje moyo mabenki ambayo yameanza kuwapatia mikopo baadhi yao.
Alisema ni kweli zamani mabenki yalikuwa hayatoi mikopo kwa wachimbaji wadogo, lakini kwa sasa hali imekuwa tofauti kwa baadhi ya mabenki kama vile NBC, NMB, CRDB, Azania yameanza kutoa mikopo.
Naibu Waziri wa Madini, Profesa Shukrani Manya alisema mpango wa serikali ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha mikutano ya kimataifa siyo ya madini, tu bali ya mambo mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima akizungumza kwa niaba ya wakuu wa mikoa wenzake, aliwataka wachimbaji hao kuacha unyonge na kujiona maskini wakati wana uwezo wa kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Malima aliwataka waache kulalamika kila wanaposhiriki mikutano hiyo badala yake waione kama fursa ya kupiga hatua na kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa ni wachimbaji kutaka kuwa na benki ya madini ili iwapatie mikopo, kuondolewa kwa utitiri wa kodi na tozo zinazotozwa na mamlaka mbalimbali za serikali pamoja na ukosefu wa taarifa za utafiti wa kijiolojia.
Chanzo: Habari Leo