Uwepo wa gesti (guest house) hutambulisha tabia na sifa za wanamtaa walivyo. Chukua tahadhari

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
Habari za Jumapili,

Ni furaha sana kuwepo kwa nyumba za kulala wageni. Siyo kila mgeni anastahili kufikishwa home au kulala kwako unapoishi!

Hivyo uwepo wa gesti unasaidia kuwatunza wageni wa namna hiyo. Kwanza ni biashara nzuri na yenye uhakika, pili ni moja ya huduma mhimu sana kwa faragha!

Lakini pamoja na yote hayo, kuna mitaa na mitaa. Kila mtaa una pepo lake!

Kuna mitaa ya viwanda, karakana, Bar, hospitali na makanisa n.k

Taarifa kutoka kwa wanajimu wa nyota na tiba mdadala unaonesha kwamba, uwepo wa gesti house nyingi katika mtaa ni kiashirio kikubwa cha uwepo wa pepo la ngono kwa wakaaji wa mtaa mzima!

Hili huonekana kupitia tabia za mtu mmoja mmoja aishiye mtaa huo kama ifuatavyo!
  • Watoto kwa wakubwa hupenda umbea
  • Mabinti kutoka mitaa hiyo huharibika mapema
  • Wanawake wa mtaa husika hupenda kukaa vibarazani
  • Wake za watu mtaa huska hushawishika kirahisi sana kuchepuka na niwasiri sana
  • Wanaume wa mtaa huska hujidai kama hawajui lolote kuhusu kinachoendelea kwenye nyumba hizo wakati kumbe ......!
Note: Ukihamia mtaa wenye gesti nyingi chunga sana tabia za mkeo na wanao wasilipokee pepo.
 
Lakini wengi wa watumiaji wa guest House hizo kwa upande wa iasherati ni wa kutoka mbali sidhani kama mm natoka na mkeo ntaenda nae guest ya karibu hapana, lazima ntaenda nae mbali ambako hawamjui wala hawanijui.

Kwa mfano nenda Arusha makao mapya kule kuna guest kama zote na wtumiaji wake ni wakutoka mbali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mtaa wa Bachu Tabora mjini, guest kama lote. Alikuwapo binti mrembo mwenye ndugu yake Mtaa huo. Jamaa aliposikia huwa anaenda Bachu kusalimia aliaihirisha Kumtongoza.
 
Miaka yote nimekaa Dsm sikuwahi kujua kwamba Buguruni sokoni kuna chimbo la wahaya hadi mwaka 2020 nilikatiza mtaa ule
😂 😂 😂 😂 😂 nilipona sana miaka flani nilikua nakaa pande zile, lile chimbo limejificha hatari sana, alaf patam ukiingia/ukitoka huonekani
 
Back
Top Bottom