Uwepo wa ATCL haujaleta unafuu wowote kwa Mtanzania

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,702
71,013
Nimeshtuka sana leo hii nilipofanya booking online (tena tarehe ya mbali) kwenda Mwanza na nilishikwa na taharuki kuona bei ikiwa ni zaidi ya laki sita.

Kweli nia ya kufufua (na wakati mwingine kuyadhibiti mashirika binafsi) ilikuwa kutuumiza kiasi hiki? Yale masifa ya nyimbo na mapambio kweli waimbaji walikuwa wanajua wanachoshangilia au ni mkumbo tuu? Bila kuingilia kati ATCL itaushindwa ushindani wa biashara.

Nimewaza si bora kutumia gari binafsi au kutafuta basi bora kabisa na kusafiri siku moja kabla ili kuwahi shughuli hata kama ratiba itaharibika?

Screenshot_20191111-084501.jpeg
 
Bei haiwezi kupungua kama serikali inaua competition kwenye biashara, inajenga monopoly kwa nguvu, na inatafuta faida ili ionekane imefanya jambo la maana kisiasa.

Katika kanuni za classical economics, monopoly ni adui wa kushuka kwa bei.

Shirika la usafiri wa ndege likiwa moja, litakuwa na incentive gani ya kupunguza bei za tiketi?
 
Mimi nimeumizwa sana kuiua fast jet. Dar to Mbeya tulikuwa tunaenda kwa laki 150,muda mwingine walikuwa wanatoa promotion mpaka elfu 80 for one trip. Siku nakumbuka nilisafirisha familia nzima wa-enjoy mwewe.

Siku hizi watu kibao wamerudi kwenye mabasi wakati walishaanza kusahau mabasi. Kuia fast jet ilipaswa kuendane basi na shirika letu kuwa nafuu zaidi ya fast jet. Lakini ATCL gharama ni kubwa mara 3 ya fast jet.
 
I see hawa jamaa ATCL wana gharama karibia mara 3 ya fast jet. Watu walishaanza kusahau mabasi baada ya fast jet kuja. Lakini sasa wamerudi kwa kasi kwenye mabasi
Hiyo bei ni karibu nusu ya bei ya tiketi za nafuu kabisa za New York to London.

Wakati umbali wa New York to London ni kama mara nne ya umbali wa Dar to Mwanza.

Sababu?

Competition.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom