Uwepo Lengai Ole Sabaya katika wilaya ya Hai ni tishio jipya kwa uhai wa CHADEMA

Feb 7, 2019
41
45
Hodi Jamvini,

Leo baada ya kupitia baadhi ya mitandao ya kijamii Nikiwa nafatilia Mambo ya duniani yanayojiri Kila siku nimebahatika kukutana na sehemu kadhaa Ambazo Kiufupi zimenipa Taswira mpya kichwani

Kwanza Ni Juu ya hofu kubwa iliyotanda vichwani vya wanachadema wengi juu ya hatima ya Ngome kuu ya chama Chao ambayo kiukweli Ni pale Wilaya ya Hai ,Nasema hivo kwa sababu Ndio shina lenyewe kwa kuwa Ni mahali ambao anaedhaniwa kuwa mwamba wa chadema Ndio nyumbani kwake na SI nyumbani tu Bali pia sehemu iliokuwa haitikisiki.

Hofu kubwa niliyoiona Ni Juu ya uwepo wa Mkuu wa Wilaya Ambae wachambuzi wengi wanamtafsiri Kama kijana shupavu,Mbabe wa Vita za Ana kwa Ana ,Kijana aliepita kwenye kashikashi nyingi za kutisha Wanamwita Lengai Ole Sabaya,

Wanachadema wengi wa mitandaoni wamechukua jukumu la kudili na Kijana Huyu kokote ambako either picha yake ama Habari zake zitakapoonekana Basi wanatumia nguvu ya Kila aina kumbeza,Kumchongea,Kumkashifu,Kumzushia na wengine wanaenda mbali zaidi wana mtolea lugha Ambazo Ni chafu,

Nimejiridhisha zaidi kwa kuanagalia hata sehemu ambazo either Kuna taarifa za viongozi was Serikali kwa pamoja basi wanachadema wengi watamshambulia Lengai Ole Sabaya pekee ake kwa tuhuma za Kila namna.

Kiukweli Nimetafakari Sana suala Ilo kupata hitimisho ambalo kwa upande wangu Ni Pumzi ya Ngome kuu ya chadema iko Mahututi au iko rehani Na Kuna Kila haja ya wanachadema kukaa chini watafakari kwa umakini hatima ya ubunge wa Mbowe pale hai either kwa kutafuta Jimbo lingine hata Moshi mjini au Vijijini lakini kwa hasira hizi nilizoziona napata majibu kuwa Pumzi ya Ngome kuu imefikishwa mwisho

Na hii Ni kuona wazi Rais Magufuli anajua kuzichanga karata zake maana Alitambua wazi kuwa Kumpeleka Hai kijana huyu Lengai Ole Sabaya basi Ni kuhamisha pambano la 2020 maana kwa namna yeyote ile Mbowe asipobadili mahala pa kugombea Basi lazima nguvu zote chama kitahamishia kula Kilimanjaro katika wilaya ya Hai ambayo Ina viongozi wanaosemekana Ni Makini,Wanaoelewana na walioiva kiitikadi na itifaka ukianza na Lengai pia Kuna DED Yohana Sintoo na DAS Upendo Wela

Wako Jamvini
Mnazarayo Mushi GODFREY
 
Sabaya kuna mikakati ya siri sana kaipanga kuhusu mbowe...kila mara wazee wanamzungumzia huyu jamaa. Ila sidhani kama ataweza kumtoa mbowe asishinde kweny wilaya hii.

Mbowe hua haonekani mara kwa mara huku kwake ila akija, influence yake bado ipo sana. Changamoto itakuwepo kwa mbowe ila kushinda ni % kubwa zaid.

Kwako Mnazarayo
 
Maneno mengi yasiyo na jipya.. nani amekwambia chadema ni mbowe..

Chadema ni watanzania wote, toka kigoma hadi mtwara, toka mbeya hadi kilindini Tanga.

Acha kutuletea story za abunuwasi.

Ivi lumumba wataacha lini kuwaharibu hawa vijana kwa hizo buku buku?
 
Sabaya kuna mikakati ya siri sana kaipanga kuhusu mbowe...kila mara wazee wanamzungumzia huyu jamaa. Ila sidhani kama ataweza kumtoa mbowe asishinde kweny wilaya hii.
Mbowe hua haonekani mara kwa mara huku kwake ila akija, influence yake bado ipo sana. Changamoto itakuwepo kwa mbowe ila kushinda ni % kubwa zaid.

Kwako Mnazarayo
Naam Mimi bado Naamini hii pia Ni mikakati ya kisiasa ya Dkt Magufuli kulihamisha pambano 2020 maana Naamini kwa viongozi damu changa Kama Sabaya,Upendo Wela na Sintoo sidhani Kama watakubali kuipoteza hai hasa ukizingatia Ndio wapya katika system na wanahitaji kwenda juu kisiasa huko mbeleni ,nafasi ya Mbowe Ni finyu sana
 
Wewe Sabaya acha uandishi wa kitoto huu ni mwandiko wako na hii ndiyo mida yako ya kuposti siasa misifa yako Mbowe ni mashine kubwa achana nayo akipata dk 5 tu anapindua meza kmbka kanisani alivyo mchenjia kakayako acha siasa za kinafiki kumdanganya Mkuu
 
seriously Lengai ole Sabaya Ni gonjwa jipya kwa vijana wa chadema maana Kila anapotajwa inakua Ni mayowe,Mimi Naamini Ni vema tukajadili mada na sio hisia Mkuu
 
Na hii Ni kuona wazi Rais Magufuli anajua kuzichanga karata zake maana Alitambua wazi kuwa Kumpeleka Hai kijana huyu Lengai Ole Sabaya basi Ni kuhamisha pambano la 2020 maana kwa namna yeyote ile Mbowe
Nani alikufundisha Hasidi hushinda vita? Nimuda utajibu
 
Huyu kijana ndio jibu la wananchi wa hai na kanda ya kaskazini kwani anapiga kazi na kuleta maendeleo chanya kwenye wilaya ya hai bila kujali itiladi za chama wala dini.

Heko kwa raisi magufuli kuwaona vijana kama hawa wachapa kazi na wenye uchungu na taifa lao.Kongole pia kwa vijana wote wa aina ya lengai wanaosukuma gurudumu la maendeleo kwa kasi ya ajaabu.

Kuhusu jimbo la hai na sia wananchi wamesha hamua hawataki siasa za majitaka na wamechoka kuwachagua wawakilishi ambao hawawatetei bungeni ila wamegeuka wahamasishaji wa vurugu bungeni na kitaifa.

Kiukweli chadema kwa upande wa kaskazini wanahemea pua moja na wako hoi bin taabani.Wanauhakika pia wanajua wananchi wa arusha na kilimanjaro wanataka viongozi wa kiwasemea shida zao sio viongozi wa kufanya vurugu na kupelekwa ndani kwa utomvu wa nidhamu.

Uchaguzi mkuu ujao wananchi wa hai wanamtaka jerry muro na sio mbowe na genge lake kwani wamekuwa wakifanya vurugu badala ya kupiga kazi hadi kufikia hatua lengai nalazimika kumkamata mashinji na kumuweka ndani ili kumnusuru na kipigo cha wananchi wa hai amabao wanataka kupiga kazi wao wanapeleka siasa muda wa kazi.

Arusha mjini imesha hamua hakuna kurudia makosa tena.Vilele vile arumeru wamesha hamua na wameanza na jimbo la arumeru mashariki.Kwa upande wa arumeru magharibi wanamtka kijana wao sabaya achukue jimbo kwani kwa muda mrefu jimbo ni kama halina mwakilishi.
 
Yaani hili lina maana kwamba:
DC, DED, DAS, Katibu wa CCM wa Wilaya, Katibu Mwenezi, Makatibu wa UVCCM, UWT, Wazazi, ongeza na OCD, DSO na wa PCCB, wote hawa wanapambana na mtu mmoja anaitwa Mbowe huko Hai na bado hawana uhakika kama watamshinda!? Kweli CDM ni hali ya hewa si mtu.
 
Nchi hii ina tatizo kubwa sana, badala ya kuhangaika na mambo yenye tija kwa nchi tunahangaika na akina Sabaya kumkomoa Mbowe Hai.
 
Huyu kijana ndio jibu la wananchi wa hai na kanda ya kaskazini kwani anapiga kazi na kuleta maendeleo chanya kwenye wilaya ya hai bila kujali itiladi za chama wala dini.

Heko kwa raisi magufuli kuwaona vijana kama hawa wachapa kazi na wenye uchungu na taifa lao.Kongole pia kwa vijana wote wa aina ya lengai wanaosukuma gurudumu la maendeleo kwa kasi ya ajaabu.

Kuhusu jimbo la hai na sia wananchi wamesha hamua hawataki siasa za majitaka na wamechoka kuwachagua wawakilishi ambao hawawatetei bungeni ila wamegeuka wahamasishaji wa vurugu bungeni na kitaifa.

Kiukweli chadema kwa upande wa kaskazini wanahemea pua moja na wako hoi bin taabani.Wanauhakika pia wanajua wananchi wa arusha na kilimanjaro wanataka viongozi wa kiwasemea shida zao sio viongozi wa kufanya vurugu na kupelekwa ndani kwa utomvu wa nidhamu.

Uchaguzi mkuu ujao wananchi wa hai wanamtaka jerry muro na sio mbowe na genge lake kwani wamekuwa wakifanya vurugu badala ya kupiga kazi hadi kufikia hatua lengai nalazimika kumkamata mashinji na kumuweka ndani ili kumnusuru na kipigo cha wananchi wa hai amabao wanataka kupiga kazi wao wanapeleka siasa muda wa kazi.

Arusha mjini imesha hamua hakuna kurudia makosa tena.Vilele vile arumeru wamesha hamua na wameanza na jimbo la arumeru mashariki.Kwa upande wa arumeru magharibi wanamtka kijana wao sabaya achukue jimbo kwani kwa muda mrefu jimbo ni kama halina mwakilishi.

Jerry Muro hana nafasi hata ya kuchungulia ,kwanza hajui shida za wana hai,hajui changamoto Za wana hai,Hafahamiki hai Kwa mchango wowote.Wana Hai ni muda wa kumchagua mtu miongoni mwenu,si wakuja Kwa shabaha ya uongozi na kuondoka
 
Naam Mimi bado Naamini hii pia Ni mikakati ya kisiasa ya Dkt Magufuli kulihamisha pambano 2020 maana Naamini kwa viongozi damu changa Kama Sabaya,Upendo Wela na Sintoo sidhani Kama watakubali kuipoteza hai hasa ukizingatia Ndio wapya katika system na wanahitaji kwenda juu kisiasa huko mbeleni ,nafasi ya Mbowe Ni finyu sana

Kwa mwenendo wa Magufuli kwenye demokrasia ya kutumia ubabe kumtangaza mwanaccm yoyote, hata huyo DC angekuwa ICU mwaka mzima bado angeweza kutuma sms kwa msimamizi wa uchaguzi kumtangaza mgombea wa ccm kuwa mshindi.

Hakuna cha kusifia mahali ambapo maboxi ya kura yanaweza kutolewa vituoni na kwenda kujazwa kura za ccm kwa uratibu wa vyombo vya dola, na bado mkurugenzi akatangaza mgombea aliyeshinda kwa hujuma za wazi hivyo.

Kwa maneno marahisi kwa sasa chini ya Magufuli hakuna uchaguzi, bali zoezi zima la uchaguzi ni picha halisi ya ujinga wa mwafrika linapokuja suala la madaraka.
 
Huyu kijana ndio jibu la wananchi wa hai na kanda ya kaskazini kwani anapiga kazi na kuleta maendeleo chanya kwenye wilaya ya hai bila kujali itiladi za chama wala dini.

Heko kwa raisi magufuli kuwaona vijana kama hawa wachapa kazi na wenye uchungu na taifa lao.Kongole pia kwa vijana wote wa aina ya lengai wanaosukuma gurudumu la maendeleo kwa kasi ya ajaabu.

Kuhusu jimbo la hai na sia wananchi wamesha hamua hawataki siasa za majitaka na wamechoka kuwachagua wawakilishi ambao hawawatetei bungeni ila wamegeuka wahamasishaji wa vurugu bungeni na kitaifa.

Kiukweli chadema kwa upande wa kaskazini wanahemea pua moja na wako hoi bin taabani.Wanauhakika pia wanajua wananchi wa arusha na kilimanjaro wanataka viongozi wa kiwasemea shida zao sio viongozi wa kufanya vurugu na kupelekwa ndani kwa utomvu wa nidhamu.

Uchaguzi mkuu ujao wananchi wa hai wanamtaka jerry muro na sio mbowe na genge lake kwani wamekuwa wakifanya vurugu badala ya kupiga kazi hadi kufikia hatua lengai nalazimika kumkamata mashinji na kumuweka ndani ili kumnusuru na kipigo cha wananchi wa hai amabao wanataka kupiga kazi wao wanapeleka siasa muda wa kazi.

Arusha mjini imesha hamua hakuna kurudia makosa tena.Vilele vile arumeru wamesha hamua na wameanza na jimbo la arumeru mashariki.Kwa upande wa arumeru magharibi wanamtka kijana wao sabaya achukue jimbo kwani kwa muda mrefu jimbo ni kama halina mwakilishi.
Umeongea kweli tupu
 
Kwa mwenendo wa Magufuli kwenye demokrasia ya kutumia ubabe kumtangaza mwanaccm yoyote, hata huyo DC angekuwa ICU mwaka mzima bado angeweza kutuma sms kwa msimamizi wa uchaguzi kumtangaza mgombea wa ccm kuwa mshindi. Hakuna cha kusifia mahali ambapo maboxi ya kura yanaweza kutolewa vituoni na kwenda kujazwa kura za ccm kwa uratibu wa vyombo vya dola, na bado mkurugenzi akatangaza mgombea aliyeshinda kwa hujuma za wazi hivyo. Kwa maneno marahisi kwa sasa chini ya Magufuli hakuna uchaguzi, bali zoezi zima la uchaguzi ni picha halisi ya ujinga wa mwafrika linapokuja suala la madaraka.

Mda,utaongea siasa ni upepo sio hesabu.
 
Back
Top Bottom