Uwenyekiti CCM na hadithi ya nani atamfunga paka kengele

Mtini

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
1,486
2,332
Kwa muda mrefu panya walikuwa wakiteswa na ukatili wa paka. Vikao vingi vilifanyika vya kujadili jinsi ya kumalizana na paka ili waishi kwa amani. Mawazo mengi yalitolewa lakini hapakupatikana jawabu la tatizo lao. Siku moja wakiwa kwenye vikao vyao, panya mmoja akatoa wazo, akasema "kwa kuwa hatuna uwezo wa kumuua paka, kwanini tusimfunge kengele ili akiwa anakuja tumsikie ili tuwahi kukimbia?".

Wazo hili lilishangiliwa sana na kikao kikaishia hapo na kufuatiwa na tafrija kubwa sana ya kujipongeza.
Siku iliyofuata wahunzi wakaitwa waje kutengeneza kengele mbele ya mkutano mkuu wa panya wote. Naam, kengele ikatengenezwa kwa ustadi mkubwa sana. Ilikuwa na uwezo wa kutoa sauti ya kumfanya hata aliye mbali aweze kuisikia inapotingishika.

Kengele hii ilitengenezwa kwa mfumo wa chuma ambacho katikati kina kirungu cha chuma kizito kiasi, kirungu hiki hucheza cheza na kujigonga kwenye chuma cha pembeni na kutoa sauti kinapotikitiswa.
Baada ya wahunzi wale kuimaliza kazi na kufanya majaribio wakaikabidhi kwa uongozi. Ikumbukwe tu kuwa muda wote huu panya wengine walikuwa wanashuhudia wahunzi wakifanya kazi huku wao wakiwa na gilasi za mvinyo wakijipongeza.

Kengele ilipokabidhiwa kwa uongozi kwa miluzi, nderemo na vigelegele, panya yulee aliyetoa wazo la kumfunga paka kengele akagonga glasi ili papatikane ukimya, panya waliponyamaza huku wakiwa na Sura za bashasha kwa kulimaliza tatizo la miaka mingi, panya yule akauliza..."tumekubaliana tumfunge paka kengele, je ni nani atakayeifanya shughuli hiyo ya kumsogelea pakashume yule na kumfunga hiyo kengele?". Panya wote wakatazamana, kisha kikapita kimya cha dakika karibu kumi na baada ya hapo panya wote wakatawanyika kimyakimya..

Huko mitaani minong'ono ikawa inazagaa kwamba kuliko 'kurisk' maisha ya panya kwa kumsogelea paka kumfunga kengele, ni bora waendelee kuishi hivihivi na paka. Ingawa vifo na kuumia kwingi kulikuwa kunatokea lakini ni Afadhali ya hali hiyo kuliko kujipeleka mwenyewe kwa paka. Na wengine wakasema kwanza paka akijua kuwa tunafanya mipango, atapata hasira atumalize wote!

Maisha yakaendelea.

Pamoja na kukubaliana kuendelea kuishi na paka, mara kadhaa walitokea panya na kuibeba kengele kwenda kumfunga paka akiwa amelala lakini waliishia kupoteza maisha yao. Panya wengi sana waliendelea kufa kwa jaribio la kuutaka ushujaa wa kumfunga paka kengele. Na mbaya zaidi jaribio la mwisho lilisababisha panya wote tisa wafe na kengele kubaki mikononi mwa paka!

Siku moja, akatokea panya mmoja ambaye hakuwa na marafiki wengi katika jamii ile ya panya...
WINO UMEISHA!

JK KABLA HUJAKABIDHI JARIBU KUKUMBUKA HAKA KAHADITHI BABA
 
Hadithi tamu sana hii
 
Tafsiri yake ni kuwa wanaCCM woote ni "panya" na Mwenyekiti wao mpya ajaye JPM ni paka tena pakashume lililotayari kuwatafuna panya woote kwa kasi kubwa sana!!

Na bahati mbaya ni kuwa pakashume huyu alishagundua kuwa mipanya imekaa kikao na kukubaliana kutengeneza kengele ya kuja kumfunga pakashume huyu ili anapowajia kutaka kuwakamata awale, wamsikie haraka na kukikimbia kifo.

Kengele iko mikononi mwa pakashume, panya hawana namna maisha yanaendelea na kila mmoja akijihami kivyake!!
 
Hahahaja kila mmoja ataibuka na tafsiri ya kwake
 
Back
Top Bottom