Uwekezaji wa Mwingereza hapa Tanzania

goroko77

JF-Expert Member
Jul 9, 2019
8,803
12,850
Wakuu hbr za jioni

Napenda. Kujuwa na Kuuliza juu ya suala la uwekezaji wa huyu mzungu muingireza hapa bongo kama nilivyosikia katika hotuba za bajeti zetu kuwa Mwingereza ndio anaongoza zaidi kwa uwekezaji na tunafanya nao biashara sana.

Je, ni maeneo gani muingereza kawekeza zaidi na kuonekana?

Ni kampuni zipi ziko hapa za muingereza ambayo ni kubwa na kufanya kazi hapa bongo na kuzalisha ajira za moja kwa moja ama indirect jobs?

Nawasilisha
 
Njliwahi kwenda mufindi kule, Aisee muingereza ana mashamba makubwa sana ya chai. yani gari inatembea kama dakika 45 hivi mashamba hayaishi tu.

Unaambiwa kule umeme haukatiki aisee, Yes, soma vizuri tena, Umeme haukatiki!! kuna mtoto wa ndugu yangu alisoma shule ya boarding huko inaitwa brooke bond, yani aliniambia hio shule yao katika miaka minne aliyosoma hawajawahi kulala giza, ni mara chache sana kama mara 3 tu umeme unakatika kwa dakika chache mwaka mzima, na pia shule inafaulisha fresh tu.
 
Back
Top Bottom