Uwekezaji soko la nyoka, Serikali isaidie kupunguza kodi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,218
24,078
March 22, 2020

Serikali yaombwa ipunguze bei ya nyoka na viumbe wengine wanaopelekwa nje kuuzwa ili wawekezaji hao wachangie fedha za kigeni nchini. Hayo maombi yamesemwa na Paul Madinda mfugaji na muuzaji wa viumbe nje ya nchi wakati akimfahamisha Naibu waziri Costantine Kanyasu juu ya fursa hiyo adimu kwa nchi kuingiza kipato kupitia maliasili na vilevile ajira.



Moja ya faida za soko la sumu ya nyoka nje ni mahitaji makubwa katika matumizi ya sumu hiyo iliyochakatwa inayoitwa botox ambayo baadaye ikatumika ktk clinics za urembo kuondoa mikunjo kupitia Botox 11 Surprising Uses For Botox katika sura za ma - celebrity wa fani ya movie za Hollywoods, wanamitindo, wanamichezo maarufu na matajiri bara la Marekani ya Kaskazini, Ulaya n.k kubakia na sura zenye muonekano wa ujana.

Pia mbali ya sumu ya nyoka, soko la nje linahitaji za ng'e, tandu, buibui na vyura kwa wingi nje ya nchi kutengeneza madawa mbalimbali ya tiba ya mwili na vipodozi.
Source : Voice of Bongo
 
Nyama ya nyoka husaidia kuifanya ngozi yako nyororo na laini

Jr
Nasikia Wachina wanakula sana vitu vya ajabu kama popo na nyoka. Matokeo yake dunia nzima imepagawa na corona! Sasa hizi tafiti kuhusu urembo unaoletwa na sumu ya nyoka, nazo ni za kuziangalia kwa tahadhari kidogo
 
90% ya nyama ya nyoka haina shida.. Na mwonekano wake hauna tofauti na nyama ya samaki hasa kwenye mchemsho
Nasikia Wachina wanakula sana vitu vya ajabu kama popo na nyoka. Matokeo yake dunia nzima imepagawa na corona! Sasa hizi tafiti kuhusu urembo unaoletwa na sumu ya nyoka, nazo ni za kuziangalia kwa tahadhari. kidogo

Jr
 
Back
Top Bottom