Uwekezaji: Sio Kila Uwekezaji na Kujenga Nchi, Mwingine ni Kuvuna tu, Uwekezaji wa Total Energies kujenga Nchi!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,
Jukwaa la Siasa:
Hapa Jukwaa la Siasa JF, mada nyingi ni mada za politiking, yaani kupiga siasa, lakini sii wengi wanajua kuwa hata mambo ya uchumi mkubwa ni siasa!, hapa tunazungumzia political economy, Siasa Uchumi.

Kila nipatapo fursa, huwaletea zile mada zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Leo nazungumzia mada ya uwekezaji, Tanzania tumefungua milango yetu na kuiacha wazi ikiwemo kuweka vivutio mbalimbali vya uwekezaji ili kuvutia uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Katika uwekezaji huo, kuna uwekezaji na uwekezaji, sio kila uwekezaji ni uwekezaji wa kujenga nchini, kuna uwekezaji mwingine sio uwekezaji wa kujenga nchi ni uwekezaji wa kuvuna nchi, mfano uwekezaji kwenye sekta ya uchimbaji wa madini, gesi, mafuta, au extractive industry, japo huu ni uwekezaji mkubwa, lakini madini yote duniani yanaitwa diminishing resources, ynafika mahali yanakwisha!. Uwekezaji kwenye sekta ya madini, japo ni uwekezaji mkubwa, lakini sio uwekezaji wa kujenga nchi, ni uwekezaji wa kuvuna nchi, mwekezaji anaingiza mtaji ili kupata mavuno, madini yakiisha, gtunaachiwa mashimo and that is it.

Kuhusu hawa TotalEnergies, naomba kuanza kuanza kwa kuweka hizi facts mezani
  1. Japo Tanzania, tangu tupate uhuru, tuna miradi mingi mikubwa ya uwezekazi iliyoanzishwa, na kuna makampuni mengi yamewekeza Tanzania, hakuna uwekezaji wowote mkubwa, zaidi ya uwekezaji wa kampuni ya mafuta ya TotalEnergies, kupitia mradi wake wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani, Tanga nchini Tanzania, huu ndio mradi wenye thamani kubwa kuliko mradi mwingine wowote nchini Tanzania kwa sasa.
  2. Japo kuna makampuni mengi yanayotoa huduma za mafuta, na vituo vingi vya mafuta, kampuni ya mafuta ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, ndio kampuni inayoongoza kwa kuwa na vituo vingi vya mafuta, ambapo mpaka sasa, ina vituo zaidi ya 100 vilivyotapakaa nchi nzima, tena vituo vya TotalEnergies, sio viko maeneo ya mijini tuu, viko hadi vijijini, siku moja nilikuwa maeneo ya vijijini huko Marangu, Moshi, nikashangaa kukutana na kituo cha kisasa cha TotalEnergies, pale kijijini Somanga!.
  3. Japo kuna aina mbalimbambali za mafuta ya petroli na dizeli, kuna Super, Regular, Unleaded, etc, mafuta yanayouzwa kwenye vituo vya TotalEnergies, ndio mafuta yanayoongoza kwa ubora, kutokana ma mafuta ya Total, kuongezwa kiambata cha TotalEnergies Excellium ambacho kinafanya mambo makubwa kwenye
Uwekezaji unaofanywa na kampuni ya TotalEnergies Marketing Tanzania Limited, huu ndio mfano wa uwekezaji mkubwa wa ukweli wenye lengo la kuisaidia nchi, kujenga nchi na sio kuvuna nchi.
Andamana nami katika makala hii.
TotalEnergies News Feature- Nipashe.jpg

Sasa kwa vile kuna wawekezaji wa aina mbili, wawekezaji wachumaji na wavunaji wa rasilimali zetu, na wawekezaji wajenga nchi.
Mnaonaje tukiishauri serikali yetu, wawekezaji wajenga nchi kama TotalEnergies, waongezewe some investment incentives, ili Tanzania tuvutie zaidi wawekezaji wajenga nchi na sio wachuma nchi?.
Paskali.
 
Wanabodi,
Jukwaa la Siasa:
Hapa Jukwaa la Siasa JF, mada nyingi ni mada za politiking, yaani kupiga siasa, lakini sii wengi wanajua kuwa hata mambo ya uchumi mkubwa ni siasa!, hapa tunazungumzia political economy, Siasa Uchumi....

Nina mashaka na makala yako.

Siku zote umekua uki ipigia chapuo hii kampuni.

Naona hii mada sio kwa maslai ya taifa, bali maslai ya Pascal.
 
Nina mashaka na makala yako....
Siku zote umekua uki ipigia chapuo hii kampuni...

Naona hii mada sio kwa maslai ya taifa, bali maslai ya Pascal....
... Kuna wimbo mmoja wa dansi kwa sisi watu wa zamani wimbo huo uliimbwa na Marehemu Nico Zengekala bwana huyu alikua kipofu ... jina la wimbo huo limekuwa ni neno maarufu sana katika lugha ya leo hasa mpaka mwishoni mwa myaka ya 90 na 2,000 wakati mataa ya barabarani yakishamiri ...
 
Nina mashaka na makala yako....
Siku zote umekua uki ipigia chapuo hii kampuni...

Naona hii mada sio kwa maslai ya taifa, bali maslai ya Pascal....
Mkuu General Mangi , tujifunze kusoma mada kwa kuangalia contents na sio mtoa mada.

Understanding ya Watanzania wengi kwenye mambo ya serious investments ni mdogo sana, hivyo sishangai mtu badala ya kujadili mada iliyopo mezani, wewe unamjadili mtoa mada. Tujadili mada iliyopo mezani.
P
 
Paskali tusaidie ajira wadogo zako. Wewe upo kwenye channel ya hela saizi maana unawajua wakuu huko, siunajua safari hii kama hakuna wa kukushika mkono hutoboi.

Mambo yamerudi kwenye mstari mwendazake alikua anawabania.

Nina kikampuni changu cha marketing hizi propaganda za kuwapgia debe mabeberu sitashindwa niamini mkuu wangu
 
Mkuu Pasko Mayala hongera kwa makala nzuri ambayo umeiandika kwa msukumo mkubwa wa uzalendo kwa Nchi yako .Samahani mkuu vipi hizi makala zako zinapatikana gazeti gani .
 
Paskali tusaidie ajira wadogo zako. Wewe upo kwenye channel ya hela saizi maana unawajua wakuu huko, siunajua safari hii kama hakuna wa kukushika mkono hutoboi.
Mambo yamerudi kwenye mstari mwendazake alikua anawabania.
Nina kikampuni changu cha marketing hizi propaganda za kuwapgia debe mabeberu sitashindwa niamini mkuu wangu
Sasa tuko kwenye ulimwengu wa kidigitali, yaani digital world, or cyber world, kila kitu kinafanywa kidigitali, this is the age of information science, to be informed.

Unachotakiwa kufanya ni ku digitize hiyo kampuni yako, tenda zote za maana zinatangazwa kidigitali, unaomba online, ushindi unapatikana kwa technical know how na sio technical know who.

Kitu muhimu sana kwa sasa ni Just be connected ili uwe Informed.
P
 
... Kuna wimbo mmoja wa dansi kwa sisi watu wa zamani wimbo huo uliimbwa na Marehemu Nico Zengekala bwana huyu alikua kipofu ... jina la wimbo huo limekuwa ni neno maarufu sana katika lugha ya leo hasa mpaka mwishoni mwa myaka ya 90 na 2,000 wakati mataa ya barabarani yakishamiri ...
Naomba nikumbushe ni wimbo gani huo, au ni solemba?.
P
 
Total kawasome vizuri hawa jamaa huko west africa na miradi yao kule Chad na Congo brazzavile... Total from france, kaisome kitu inaitwa french Africa na makampuni kama total influence yake....Moja ya project ya french Africa ni Gabon na Burkin faso..

Total amemnunua Anadarko pale Msumbiji, yuko na project kuubwa sana ya LNG....tayari RPF vijana wa PK wako pale...

Mengine magumu bwana Pasco nenda kayachimbe...
 
Mkuu General Mangi , tujifunze kusoma mada kwa kuangalia contents na sio mtoa mada.

Understanding ya Watanzania wengi kwenye mambo ya serious investments ni mdogo sana, hivyo sishangai mtu badala ya kujadili mada iliyopo mezani, wewe unamjadili mtoa mada. Tujadili mada iliyopo mezani.
P
Sasa unaachaje kumjadili mtoa mada ambaye ni wakala, mwenye maslahi na mada aliyoitoa? Yaani unajadili embe ukaacha kujadili mwembe? Kwani hilo embe limetokana na mpapai? Wanakulipa tsh ngapi Total? Basi vijana wanakwambia uwatafutie kazi na wao muwe wengi.
 
Back
Top Bottom