Uwekezaji, mikakati na mapinduzi makubwa ktk kukuza utalii. Tunaweza

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
887
705
Ufaransa (France) inapokea watalii si chini ya milioni 80 kila mwaka toka kote duniani. Paris ikiwa kitovu cha kupokea watalii husika. Lakini pamoja na wingi huo wa watalii, Ufaransa haina vivutio vya utalii kwa wingi kama ilivyo Tanzania, Kenya ama Afrika ya Kusini.

Msingi mkubwa wa watalii wengi kutembelea Paris (Ufaransa) ni hospitality, huduma nafuu za mahotel, ukarimu wa wageni na makumbusho mbalimbali katika nchi. Lakini wengi wa watalii hurudi kutembelea tena na tena.

Hapa kwetu tuna vivutio vya kila aina kuanzia mbuga, hifadhi, milima, maporomoko, mapango, fukwe na mengineyo, lakini idadi ya watalii inakuwa kidogo kila mwaka. Na pia kuna jitihada kubwa za Mh Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Royal Tour.

Tunakwama wapi? Na nini kifanyike?


Elimu ya kina itolewe kwa wananchi wadau wa utalii kwa kuanza na taxi drivers, hotel operators, viongozi wa viwanja vya ndege, mamlaka za uhifadhi, maafisa uhamiaji, wadau wa afya, wakazi jirani na maeneo ya vivutio na mijini.

Makundi haya yaelimishwe kuhusu uhalisia na saikolojia ya watalii wengi wanaokuja, kwamba si wote ni matajiri, hivyo kasumba ya kuwapiga bei na kuwakomoa ni sawa na uhujumu taifa/uchumi.

Kwa mfano, taxi drivers wa airport zetu za kimataifa wamekuwa wakichaji wageni kati ya dola 35 mpaka 80 kwa safari ya kilomita 10 mpaka 15. Sidhani kama ina afya, huku pia baadhi ya wenye hotel wakichaji zaidi watalii au wageni katika mazingira ambayo wangeweza kuweka gharama za chini, hivyo kuchochea utalii zaidi.

Kwa kuwa sekta ya utalii inaweza liingizia taifa mabilioni ya fedha kila mwaka, hivyo kupunguza utegemezi katika mikopo na misaada, hakuna budi kufanya uwekezaji katika ulinzi wa wageni. Jeshi letu la polisi liwe na kitengo maalumu cha kulinda watalii ili kuongeza usalama wao, kitu ambacho ni chachu kuu ya mipango ya watalii kutembelea au kututembelea mataifa fulani (mataifa yenye usalama mdogo yana nafasi ndogo sana kupata watalii) ukilinganisha na yenye usalama mkubwa.

Vitendo vya watalii kuporwa, kufanyiwa vitendo vya ulaghai na kudhalilishwa havipaswi kutetewa hata kidogo, hivyo vinapaswa kuwa sawa na uhujumu taifa/uchumi.

Ikumbukwe wawekezaji wengi katika nchi zinazoendelea, wengi wao huvutiwa kuwekeza baada ya kuridhishwa na mazingira wakiwa watalii. Hivyo, upo uwezekano mkubwa wa kuunganisha utalii na uwekezaji na kupanua wigo wa mapato kiuchumi na maendeleo ya nchi.

Serikali iruhusu uwekezaji wa vivutio vya kisasa katika fukwe zetu, visiwa vyetu, mapango yetu na milima yetu. Tumethubutu, tumejaribu, tunaweza.

Vyombo vya habari ndani na nje vinapaswa kuwa na vipindi maalumu vinavyohusiana na kuhamasisha utalii wa ndani, kwa mfano, katika mainstream media zote pamoja na media za kidigitali.

Vyombo vya usafiri (Anga, ardhini, nchi kavu) navyo vihusike kuwa na maudhui yaliyoandaliwa maalumu kuhusu utalii.

Utalii ni zaidi ya madini, utalii ni zaidi ya mafuta na gesi. Tunaweza kuendesha taifa letu kwa mapato ya utalii.
 
Kazi kweli kweli kwanza usiongopewe kwamba royal tour imeleta au italeta watalii. Ile ilikuwa ni biashara tu ya bwana Tony. Pili, kuwa na maporomoko, milima, mbuga, hifadhi, mapango, na fukwe sio vigezo pekee vya kuvutia watalii. Mfano, Kenya na Afrika Kusini hawana vitu vingi ulivyotaja kuizidi Tanzania, lakini bado wanapokea watalii wengi kuliko Tanzania. Kuna nchi moja inaitwa Austria, inapokea mamilioni ya watalii kila mwaka. Kivutio chao kikubwa ni mji wa Salzburg, nyumbani kwa Mozart, mwanamuziki mahiri wa classical music, ambaye alifariki miaka mingi iliyopita.

Lakini watalii kutoka nchi mbalimbali na Marekani hawakauki pale. Vivutio vyao vingine ni makanisa ya kale, nyumbani kwa Adolf Hitler, na vyakula na wines. Kuna wiki ya kuonja wines mpya, watalii wanafurika pale. Ufaransa, watalii wengi wanafurika kwa sababu ya chakula na pombe, matanuzi na gambling. Angalia, Ufaransa inapokea watalii wengi kutoka nchi za Uarabu kwa sababu tu Ufaransa wana tolerance kubwa juu ya Uislamu.

Sisi Tanzania tungeweza kupokea watalii wengi kupitia Butiama kwa Mwalimu kuliko hata hizo mbuga za wanyama. Kama tungeweza kutengeneza mazingira mazuri ya Educational tour, sababu Mwalimu alitambuliwa na vyuo vingi duniani ambavyo vilimtunuku degree za heshima ya Udaktari. Kwa hiyo, labda tutengeneze royal tour nyingine ya upande wa elimu. Japokuwa haitafanikiwa kama jina litabaki royal tour.

Mwalimu alikuwa mjamaa, hakushabikia utawala wa Royal. Ningefurahi sana kama siku moja ningepata darasa na mimi nikatoa elimu yangu japo ni ndogo kuhusu utalii Tanzania. Nini kifanyike? Kwa sababu hii ni fani yangu, tourism and hospitality. Kuna aina nyingi za utalii tunaweza kuzitumia na zikatutoa kuliko kushikilia wanyama tu. Sasa na huo mlima, wanataka kufunga cable car. Swali kati ya Kilimanjaro na mlima Everest upi mrefu kuliko mwingine? Jee, Everest wamefunga cable cars ili kuupanda?

Tunayo milima ya Usambara, hakuna hata mtu anayeizungumzia. Pia, tushikamane na
UNESCO watusaidie kuitangaza na kufufua magofu ya kule Kilwa Kivinje, Kipatimu, Mkoani, Masoko. Kuna historia kubwa kuielezea Kilwa kabla ya Tanganyika kuwepo ikiwa dola na fedha yake.
 
Ufaransa (France) inapokea watalii si Chini ya milioni 80 kila mwaka toka ktk pembe zote Za dunia.Paris ikiwa kitovu kupokea watalii husika..Lakini pamoja na wingi huo wa watalii Ufaransa haina vivutio vya utalii Kwa wingi kama ilivyo Tanzania,Kenya ama Afrika ya kusini..
Kivutio ni nini ?
Msingi mkubwa wa watalii wengi kutembelea Paris (Ufaransa) ni hospitality,Huduma nafuu Za mahotel,Ukarimu wa wageni na makumbusho mbalimbali ktk nchi..Lakini wengi wa watalii urudi kutembelea tena na tena..
Je hivyo sio vivutio ?


To put it mildly hizi ni baadhi ya sababu courtesy of CNBC

On top of that, France is easily accessible from neighboring European countries, is relatively small and has a certain "je ne sais quoi" — something that you can't quite put your finger on
"People are drawn to France for the exquisite cuisine, culture, pure beauty of the country and, ultimately, the way they feel when there. There is a certain romance to France,"
 
Acha na wao wazipige

Wasipofanya hivyo watalii wataongezeka na mapato yataongezeka halafu WANASIASA watapiga

Hii nchi kila mtu akipata kanafas anapiga ni nchi ya KIPIGAJI PIGAJI
 
Back
Top Bottom