Uwekezaji Kwenye Mafuta na Gesi - Tuongeze Umakini...

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Nimemsikiliza Rais Kikwete akitoa ufafanuzi juu ya jinsi wawekezaji katika uchimbaji wa gesi na mafuta watakavyolipa gharama zao za uwekezaji.

Hata hivyo, katika maelezo ya Rais kuna jambo halijatolewa ufafanuzi.

Rais anasema, kinachofanywa sasa na serikali ni kujenga uwezo wa kuhakiki mapato ya mwekezaji ili pale kitakapofika kiasi kinacholingana na gharama za uwekezaji tuanze kugawana mapato. Hii inamaanisha kuwa uwezo huo wa uhakiki bado hatuna ila ndio tunaujenga hivi sasa.

Kimsingi dhana ya mwekezaji kurudisha gharama zake haina tatizo.

Hata hivyo, ufafanuzi unatakiwa kutolewa juu ya mambo matatu:

1. Je, katika hatua za awali ambazo zimeshaanza, serikali inafanya uhakiki wa gharama anazoingia mwekezaji ili kuwa na uhakika kuwa gharama anazotaja ni sahihi? Mwekezaji anaweza kununua kifaa kwa shilingi mioni mia mbili halafu akasema amekinunua kifaa hicho kwa shilingi milioni mia sita! Je, tuna uweza na utaratibu wa kuhakiki hili?

2. Kama mwekezaji ataruhusiwa kurudisha gharama zake kwanza, inamaanisha kwamba tumeshirikiana naye kwenye kuwekeza. Je, zile mali zilizopo zitakuwa za nani baada ya gharama zake kurudi? Kwa lugha nyingine ni kwamba, mwekezaji anakuwa ametukopesha sisi katika uwekezaji huo kwa kuwa yeye ametangulia kuingiza fedha lakini na sisi tutachangia baadae wa gesi/mafuta yetu. Kwahiyo, kama mwekezaji alitumia pesa hizo kununua mashine na kujenga nyumba, gharama zile zinaporudi mashine hizo na nyuma zinakuwa zetu wote. Actually sisi ndio tunakuwa tumeingia gharama yote ya kununua vifaa hivyo na gharama nyingine za uwekezaji!

3. Kwavile na sisi tutalipia gharama za uwekezaji kwa njia ya gesi/mafuta yetu, basi sisi pia tuna haki ya kushiriki katika kudhibiti matumizi/gharama za awali za uwekezaji. Kwa mfano, mwekezaji anaweza kuamua kuajiri mwanasheria kutoka Australia ambaye atamlipa shilingi milioni 500. Sisi kama wadau muhimu ambao gharama hiyo tutailipa kwa njia ya gesi, tunapaswa kuwa na nafasi ya kushiriki maamuzi ya kukubaliana na uwekezaji huo iwapo una umuhimu. Pengine kazi hiyo ingeweza kufanywa na mwanasheria wa Tanzania kwa gharama nafuu na hivyo kupunguza kiasi cha gesi/mafuta yetu kitakachopotea bila ulazima. Hivyohivyo kwenye ununuzi wa vifaa.

Haya ni mambo ambayo ufafanuzi wa Rais haukuyagusa, lakini ni mambo muhimu kutolewa ufafanuzi yakinifu.

Mwekezaji anaingiza pesa nyingi, lakini ifahamike kuwa mwekezaji hatufanyii hisani. Tuko kwenye biashara.
 
Wanajamvi Uwekezaji kwenye utafuataji wa mafuta na Gesi ni ghali sana. Haya makampuni yanayokuja kuwekeza yameshajipanga sana na yanapata mikopo kutoka mabenki makubwa ya ulaya na World bank. Kuchimba kisima kimoja tu baharini mtwara ni gharama kubwa mfano kisima kimoja chaweza kuchukua wiki nne hadi kukamilika (inategemea na kina) sasa gharama zote hizo ikiwa kwa siku moja ni US $mil 1.2 je ni kampuni gani ya mzawa au serikali yetu hii itaweza kuwekeza kuchimba visima zaidi ya 20tu kutafuta? Tusijidanganye kuwa tunaweza kuwekeza ni gharama kubwa mno na hapo huna uhakika kuwa hiyo gesi au mafuta yatakuwa economical au non economical kuproduce. Je serikali au wa-TZ tutawezaje uwekezaji huu ikiwa hata kulipa walimu mishahara ni kazi??

Tutafakari..... Any changes takes time inaweza kuchukua hadi vizazi viwili kuja kufaidi kweli haya matunda ya hii gesi tunayoisikia. Unafikiri kama wanawekeza pesa zote for more that 3 years hizo how long will it take for them to get their money back??
 
Why? Rais wa chama chako kasema humwamini? Kwani sera ya CCM kuhusiana na gesi na mafuta inasemaje?

mwanakijiji nchi yetu inaangamia kwa sababu ya wana siasa walafi, waliwezaje kuingia mikataba wakati hawakuwa na sera ?? mambo yote uliyozungumza ni sera hakuna sera ya kudhibiti gharama anazoweka mwekezaje makosa ambayo tuliyagundua miaka mingi iliyopita lakini kibaya zaidi makosa hayo yanaendelea kujirudia.

mpaka siku tutakabobadilisha mfumo huu wa kuongozwa na wanasiasa people who have never ran any business in their entire lives kutoa maamuzi ya kibiashara hatuwezi kufika kokote mfumo mbaya ambao ni zao la katiba mbaya unaowapa mwanya wahusika kufilisi nchi.
 
Una uwezo mkubwa sana wa kuchanganua mambo tena kwa kina, ndio maana huwa nakushangaa sana na pia unanikera unapoamua kujivika uhayawani. Maswali yako mazuri sana yanahitaji ufafanuzi wa kina toka kwa Kikwete.
 
Wanajamvi Uwekezaji kwenye utafuataji wa mafuta na Gesi ni ghali sana. Haya makampuni yanayokuja kuwekeza yameshajipanga sana na yanapata mikopo kutoka mabenki makubwa ya ulaya na World bank. Kuchimba kisima kimoja tu baharini mtwara ni gharama kubwa mfano kisima kimoja chaweza kuchukua wiki nne hadi kukamilika (inategemea na kina) sasa gharama zote hizo ikiwa kwa siku moja ni US $mil 1.2 je ni kampuni gani ya mzawa au serikali yetu hii itaweza kuwekeza kuchimba visima zaidi ya 20tu kutafuta? Tusijidanganye kuwa tunaweza kuwekeza ni gharama kubwa mno na hapo huna uhakika kuwa hiyo gesi au mafuta yatakuwa economical au non economical kuproduce. Je serikali au wa-TZ tutawezaje uwekezaji huu ikiwa hata kulipa walimu mishahara ni kazi??

Tutafakari..... Any changes takes time inaweza kuchukua hadi vizazi viwili kuja kufaidi kweli haya matunda ya hii gesi tunayoisikia. Unafikiri kama wanawekeza pesa zote for more that 3 years hizo how long will it take for them to get their money back??
maelezo mengi uliyoyatoa ni propoganda zinatolewa na serikali ya CCM ili kuwaziba masikio wazawa kwa kutumia vigezo vya fedha huo ni uongo wa wazi. kuhusu gharama hesabu yako sijui umeipta wapi kwani kuna variable nyingi zinajumuisha kupata gharama na bahati mbaya ukusema gharama zako zinazingatia nini? ushirikishwaji wa wananchi hauishii ktk kuwezeshwa tu bali kutengeneza sera ambazo zitawazesha wazawa kuwa service industry ya kuhudumia makampuni makubwa ambavyo viwanda hivi vidogo ndivyo vinavyotoa ajira nyingi kwa wazawa leo hii utashangaa hata hizo drill rig canteen yao utasikia wafanyakazi wametoka ulaya na hata udongo wa kusaidia kuchimba mafuta au gesi una supplied na kampuni kutoka ulaya. wise up my friend jiulize watu hawa leo wanaoubiri gharama wakijiona wao ni smart ilikuwaje wasaini mikataba huku hawana sera ???
 
Why? Rais wa chama chako kasema humwamini? Kwani sera ya CCM kuhusiana na gesi na mafuta inasemaje?

Hakuna mtu niliyesema simwamini. Nilichosema ni kwamba ufafanuzi wa Rais haujazungumza kuhusu vipengele hivyo ambavyo kwa hakika watu wengi wangependa kupata ufafanuzi wake...
 
maelezo mengi uliyoyatoa ni propoganda zinatolewa na serikali ya CCM ili kuwaziba masikio wazawa kwa kutumia vigezo vya fedha huo ni uongo wa wazi. kuhusu gharama hesabu yako sijui umeipta wapi kwani kuna variable nyingi zinajumuisha kupata gharama na bahati mbaya ukusema gharama zako zinazingatia nini? ushirikishwaji wa wananchi hauishii ktk kuwezeshwa tu bali kutengeneza sera ambazo zitawazesha wazawa kuwa service industry ya kuhudumia makampuni makubwa ambavyo viwanda hivi vidogo ndivyo vinavyotoa ajira nyingi kwa wazawa leo hii utashangaa hata hizo drill rig canteen yao utasikia wafanyakazi wametoka ulaya na hata udongo wa kusaidia kuchimba
mafuta au gesi una supplied na kampuni kutoka ulaya. wise up my friend jiulize watu hawa leo wanaoubiri gharama wakijiona wao ni smart ilikuwaje wasaini mikataba huku hawana sera ???

Dont get me wrong my friend na usifikiri kila mtu anayekujamkuandika kitu humu basi ni Mwanasiasa. Am not the politician and I never dream to be. Naongea fact kwa sababu nina experience ya kutosha kwenye hii Industry and still in the same industry. Nakupa fact kuwa kwenye project ya BG mtwara gharama zote kwa siku ni US $1.4 mil kataa au kubali. there are more than five international companies there working for the same client. ndio maana kwa wenzetu hawa muda ni mali.
Kuhusu swala la wazawa kuwa suppliers mbona lipo tu. Mbona hata huko Mtwara Kampuni za kutoka nje zimeajiri wazawa wengi na wanafanya kazi huko? mbona maji tunayokunywa huko ni ya Kilimanjaro na juice ni Azam? unataka kampuni gani ya kitanzania ipewe tenda ya kudrill wakati haina hata watu walioko trained kuwa oilwell roughnecks? grow up man hizi kazi ni very proffesional na zinzhitaji kufanya kwa mara moja tu bila kukosea kwa sababu there is no room to correct a mistake for free. Hazihitaji siasa wala propaganda mkuu
 
Wanajamvi Uwekezaji kwenye utafuataji wa mafuta na Gesi ni ghali sana. Haya makampuni yanayokuja kuwekeza yameshajipanga sana na yanapata mikopo kutoka mabenki makubwa ya ulaya na World bank. Kuchimba kisima kimoja tu baharini mtwara ni gharama kubwa mfano kisima kimoja chaweza kuchukua wiki nne hadi kukamilika (inategemea na kina) sasa gharama zote hizo ikiwa kwa siku moja ni US $mil 1.2 je ni kampuni gani ya mzawa au serikali yetu hii itaweza kuwekeza kuchimba visima zaidi ya 20tu kutafuta? Tusijidanganye kuwa tunaweza kuwekeza ni gharama kubwa mno na hapo huna uhakika kuwa hiyo gesi au mafuta yatakuwa economical au non economical kuproduce. Je serikali au wa-TZ tutawezaje uwekezaji huu ikiwa hata kulipa walimu mishahara ni kazi??

Tutafakari..... Any changes takes time inaweza kuchukua hadi vizazi viwili kuja kufaidi kweli haya matunda ya hii gesi tunayoisikia. Unafikiri kama wanawekeza pesa zote for more that 3 years hizo how long will it take for them to get their money back??

Mkuu,

Maelezo yako ni sahihi, lakini mada haijadili ushirikishwaji wa wazawa.

Mada inajadi udhibiti na uhakiki wa matumizi ya mwekezaji na umiliki wa mali iliyowekezwa.
 
Dont get me wrong my friend na usifikiri kila mtu anayekujamkuandika kitu humu basi ni Mwanasiasa. Am not the politician and I never dream to be. Naongea fact kwa sababu nina experience ya kutosha kwenye hii Industry and still in the same industry. Nakupa fact kuwa kwenye project ya BG mtwara gharama zote kwa siku ni US $1.4 mil kataa au kubali. there are more than five international companies there working for the same client. ndio maana kwa wenzetu hawa muda ni mali.
Kuhusu swala la wazawa kuwa suppliers mbona lipo tu. Mbona hata huko Mtwara Kampuni za kutoka nje zimeajiri wazawa wengi na wanafanya kazi huko? mbona maji tunayokunywa huko ni ya Kilimanjaro na juice ni Azam? unataka kampuni gani ya kitanzania ipewe tenda ya kudrill wakati haina hata watu walioko trained kuwa oilwell roughnecks? grow up man hizi kazi ni very proffesional na zinzhitaji kufanya kwa mara moja tu bila kukosea kwa sababu there is no room to correct a mistake for free. Hazihitaji siasa wala propaganda mkuu
my friend you are part of the problem kwa bahati mbaya kwani unaonekana ku argue kama wana ccm kwa sababu hizi.

1.gharama za $1.4m per day ni according to who ??? it is accord. to them or independent observer ??

2. unasema wataalamu hakuna hilo ni kosa la nani ?? shouldn't we make sure the boat is there before we jump off the cliff ??

3. umesema kuna local wana supply huduma umeshindwa kuzitaja hizo kampuni locals zinazotoa huduma ?? unataja
maji ya azam je kununua maji ya azam kunaitaji mwekezaji ?? mimi nanunua maji nami si investor , think outside the
box na si kuhubiri kile wanachikiimba CCM na seriakli yao kwamba watanzania hatuwezi
 
Mi nafikiri hapa si malumbano ya sera za vyama, anachokizungumza hapo juu huyu mwana-jamvi ni suala la muhimu ili kuja msitakabali wa watanzania juu ya rasilimali tulizopewa na Mungu. nafikiri ni muhimu kufikiri masilahi ya nchi kabla hatujaanza malumbano ya itikadi za vyama.
 
Mkuu,

Maelezo yako ni sahihi, lakini mada haijadili ushirikishwaji wa wazawa.

Mada inajadi udhibiti na uhakiki wa matumizi ya mwekezaji na umiliki wa mali iliyowekezwa.

May be am out of topic but not the whole ngoja niishie hapa.
 
Ni kweli kuwa umakini unahitajika zaidi kwenye suala hili, ndio maana JK kasema wanazidi kujenga uwezo. Lazima tufahamu kuwa Tanzania haijawahi kuwa na visima vya mafuta wala gesi hivyo jambo hli lililloko mbele yetu si la kukurupukia au kurumbana, ni wakati sasa tutulie, tutafakari tuone ni kwa jinsi gani Tanzania itanufaika na rasilimali hii. Tusilaumu uwekezaji na kujidai eti kampuni zetu za ndani zinauwezo wa kuchimba, mbona hizo kampuni za ndani zilikua hazijagundua rasilimali hii kwa miaka yote, halafu leo ndo wasemee eti ooooooooh.....
 
Mi nafikiri hapa si malumbano ya sera za vyama, anachokizungumza hapo juu huyu mwana-jamvi ni suala la muhimu ili kuja msitakabali wa watanzania juu ya rasilimali tulizopewa na Mungu. nafikiri ni muhimu kufikiri masilahi ya nchi kabla hatujaanza malumbano ya itikadi za vyama.

Ni kweli.

Kuna watu wanajisahau, wakati tunajadili specific issues wao wanaleta general assumptions.

Matokeo yake mpaka giza linazama tunakuta hatuna common resolutions.
 
Nimemsikiliza Rais Kikwete akitoa ufafanuzi juu ya jinsi wawekezaji katika uchimbaji wa gesi na mafuta watakavyolipa gharama zao za uwekezaji.

Hata hivyo, katika maelezo ya Rais kuna jambo halijatolewa ufafanuzi.

Rais anasema, kinachofanywa sasa na serikali ni kujenga uwezo wa kuhakiki mapato ya mwekezaji ili pale kitakapofika kiasi kinacholingana na gharama za uwekezaji tuanze kugawana mapato. Hii inamaanisha kuwa uwezo huo wa uhakiki bado hatuna ila ndio tunaujenga hivi sasa.

Kimsingi dhana ya mwekezaji kurudisha gharama zake haina tatizo.

Hata hivyo, ufafanuzi unatakiwa kutolewa juu ya mambo matatu:

1. Je, katika hatua za awali ambazo zimeshaanza, serikali inafanya uhakiki wa gharama anazoingia mwekezaji ili kuwa na uhakika kuwa gharama anazotaja ni sahihi? Mwekezaji anaweza kununua kifaa kwa shilingi mioni mia mbili halafu akasema amekinunua kifaa hicho kwa shilingi milioni mia sita! Je, tuna uweza na utaratibu wa kuhakiki hili?

2. Kama mwekezaji ataruhusiwa kurudisha gharama zake kwanza, inamaanisha kwamba tumeshirikiana naye kwenye kuwekeza. Je, zile mali zilizopo zitakuwa za nani baada ya gharama zake kurudi? Kwa lugha nyingine ni kwamba, mwekezaji anakuwa ametukopesha sisi katika uwekezaji huo kwa kuwa yeye ametangulia kuingiza fedha lakini na sisi tutachangia baadae wa gesi/mafuta yetu. Kwahiyo, kama mwekezaji alitumia pesa hizo kununua mashine na kujenga nyumba, gharama zile zinaporudi mashine hizo na nyuma zinakuwa zetu wote. Actually sisi ndio tunakuwa tumeingia gharama yote ya kununua vifaa hivyo na gharama nyingine za uwekezaji!

3. Kwavile na sisi tutalipia gharama za uwekezaji kwa njia ya gesi/mafuta yetu, basi sisi pia tuna haki ya kushiriki katika kudhibiti matumizi/gharama za awali za uwekezaji. Kwa mfano, mwekezaji anaweza kuamua kuajiri mwanasheria kutoka Australia ambaye atamlipa shilingi milioni 500. Sisi kama wadau muhimu ambao gharama hiyo tutailipa kwa njia ya gesi, tunapaswa kuwa na nafasi ya kushiriki maamuzi ya kukubaliana na uwekezaji huo iwapo una umuhimu. Pengine kazi hiyo ingeweza kufanywa na mwanasheria wa Tanzania kwa gharama nafuu na hivyo kupunguza kiasi cha gesi/mafuta yetu kitakachopotea bila ulazima. Hivyohivyo kwenye ununuzi wa vifaa.

Haya ni mambo ambayo ufafanuzi wa Rais haukuyagusa, lakini ni mambo muhimu kutolewa ufafanuzi yakinifu.

Mwekezaji anaingiza pesa nyingi, lakini ifahamike kuwa mwekezaji hatufanyii hisani. Tuko kwenye biashara.
Mbona leo una mawazo mazuri?!!! Au mtu mwingine kaiba ID yako? Ni wewe kweli?!! Maana siku zote huwa unasifika kwa uharo tu hapa!!!
 
my friend you are part of the problem kwa bahati mbaya kwani unaonekana ku argue kama wana ccm kwa sababu hizi.

1.gharama za $1.4m per day ni according to who ??? it is accord. to them or independent observer ??

2. unasema wataalamu hakuna hilo ni kosa la nani ?? shouldn't we make sure the boat is there before we jump off the cliff ??

3. umesema kuna local wana supply huduma umeshindwa kuzitaja hizo kampuni locals zinazotoa huduma ?? unataja
maji ya azam je kununua maji ya azam kunaitaji mwekezaji ?? mimi nanunua maji nami si investor , think outside the
box na si kuhubiri kile wanachikiimba CCM na seriakli yao kwamba watanzania hatuwezi

Mkuu Hivi unahitaji nini kuamini kuwa the cost is that much high?? Do you really thing Investing in oilwell drilling offshore is same as starting a business in Kariakoo? Anyways hakuna njia ya kukufanya uamini hilo na siku utakuja kujua labda ukipata nafasi ya kujua how Drilling operations Involve Multiple companies with a single Client paying for every single Thing/ a person Involves in an operations ndio maan opreation zikisimama iwe kwa uzembe au vyovyote vile for more that 3 minutes is counted as NPT because of the higher cost per day.

Umesema kuwa kosa la kukosa wataalamu ni la nani. mimi nadhani ni la hayo makampuni yanayotaka kuwekeza pasi na wataalmu wala uwezo wa kutosha. mimi sio kwamba siungi mkono au nasema hawawezi lakini Is there any Local Company which can Invest such money over 3-5 years in Exploration-Development and yet still Invest even more for more tha 3 years to Facilitate production? kama hiyo kampuni ipo basi ipewe kitalu na Iwekeze ili wazawa tunufaike.

Kuhusu hilo la Makampuni kama Local suppliers ni mengi na sio offshore tu hata kwenye operational bases za makampuni yote ambayo yako Involved ni ajira pia hizo products nadhani ni za makmpuni ya ki-Tanzania. It was jus few to mention

Mimi naona niishie hapa nisijeonekana mwanasiasa au natetea ujinga lakini kuna siku nitakuja na uzi humu wa mapendekezo yangu kulingana na ninchokifahamu labda wakubwa serikalini watasikiliza
 
Back
Top Bottom