Tuongeze umakini katika Uwekezaji wa Mafuta na Gesi

ZeMarcopolo

Platinum Member
May 11, 2008
14,017
7,220
Nimemsikiliza Rais Kikwete akitoa ufafanuzi juu ya jinsi wawekezaji katika uchimbaji wa gesi na mafuta watakavyolipa gharama zao za uwekezaji.

Hata hivyo, katika maelezo ya Rais kuna jambo halijatolewa ufafanuzi.

Rais anasema, kinachofanywa sasa na serikali ni kujenga uwezo wa kuhakiki mapato ya mwekezaji ili pale kitakapofika kiasi kinacholingana na gharama za uwekezaji tuanze kugawana mapato. Hii inamaanisha kuwa uwezo huo wa uhakiki bado hatuna ila ndio tunaujenga hivi sasa.

Kimsingi dhana ya mwekezaji kurudisha gharama zake haina tatizo.

Hata hivyo, ufafanuzi unatakiwa kutolewa juu ya mambo matatu:

1. Je, katika hatua za awali ambazo zimeshaanza, serikali inafanya uhakiki wa gharama anazoingia mwekezaji ili kuwa na uhakika kuwa gharama anazotaja ni sahihi? Mwekezaji anaweza kununua kifaa kwa shilingi mioni mia mbili halafu akasema amekinunua kifaa hicho kwa shilingi milioni mia sita! Je, tuna uweza na utaratibu wa kuhakiki hili?

2. Kama mwekezaji ataruhusiwa kurudisha gharama zake kwanza, inamaanisha kwamba tumeshirikiana naye kwenye kuwekeza. Je, zile mali zilizopo zitakuwa za nani baada ya gharama zake kurudi? Kwa lugha nyingine ni kwamba, mwekezaji anakuwa ametukopesha sisi katika uwekezaji huo kwa kuwa yeye ametangulia kuingiza fedha lakini na sisi tutachangia baadae wa gesi/mafuta yetu. Kwahiyo, kama mwekezaji alitumia pesa hizo kununua mashine na kujenga nyumba, gharama zile zinaporudi mashine hizo na nyuma zinakuwa zetu wote. Actually sisi ndio tunakuwa tumeingia gharama yote ya kununua vifaa hivyo na gharama nyingine za uwekezaji!

3. Kwavile na sisi tutalipia gharama za uwekezaji kwa njia ya gesi/mafuta yetu, basi sisi pia tuna haki ya kushiriki katika kudhibiti matumizi/gharama za awali za uwekezaji. Kwa mfano, mwekezaji anaweza kuamua kuajiri mwanasheria kutoka Australia ambaye atamlipa shilingi milioni 500. Sisi kama wadau muhimu ambao gharama hiyo tutailipa kwa njia ya gesi, tunapaswa kuwa na nafasi ya kushiriki maamuzi ya kukubaliana na uwekezaji huo iwapo una umuhimu. Pengine kazi hiyo ingeweza kufanywa na mwanasheria wa Tanzania kwa gharama nafuu na hivyo kupunguza kiasi cha gesi/mafuta yetu kitakachopotea bila ulazima. Hivyohivyo kwenye ununuzi wa vifaa.

Haya ni mambo ambayo ufafanuzi wa Rais haukuyagusa, lakini ni mambo muhimu kutolewa ufafanuzi yakinifu.

Mwekezaji anaingiza pesa nyingi, lakini ifahamike kuwa mwekezaji hatufanyii hisani. Tuko kwenye biashara.
 
Back
Top Bottom