Uwekezaji katika shule za awali (chini ya miaka mitano) ni muhimu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,268
Kuna umuhimu wa kuwekeza zaidi katika elimu ya awali. Wana saikolojia wanasema umri huu ndiyo umri wa ku ‘make or break a child’ yaani mtoto akikosa muongozo, mapenzi na malezi katika umri huu ni rahisi kuharibikiwa kabisa huko mbele.

Jamii tunayoishi wakina mama wana mchango mkubwa katika kukuza uchumi na kuleta mkate juu ya meza. Wanawake wako sokoni, mama lishe, uhudumu wa bar, kazi za usafi, mashamba ni, maofisini, ufundi na hata u dereva. Wengi wao hawana uwezo wa kuajiri wasaidizi wa kuwasaidia kulea watoto. Mtoto anaachwa kwa jirani.

Kukiwa na shule za awali za mtaa zinazolea watoto kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa kumi jioni, kutawapa nafasi wamama kufanya shughuli zao kwa amani zaidi. Pia watoto watapata nafasi ya kucheza na kujifunza dunia inayowqzunguka na kupanua maarifa yao.

Watoto wengi hawana hata matoy ya kuchezea. Uwezo wa wqzqzi unatofautiana. Nimemuangalia mtoto Charles Mathias, miaka sita anatembea umbali wa lisaa lizima kufuata elimu ya awali. Nyumbani anakotoka ni mazingira magumu na shule anayosoma pia ina hali duni.

Matoy wa kuchezea watoto China yanauzwa kwa gharama nafuu. Ni kama mbunge na viongozi viongozi wengine wakiorodhesha mahitaji yao na kuagiza mzigo utawanufaisha watoto wetu.

1614771784644.jpeg
 
A. Umri wa mwaka sufuri hadi mitatu.

B. Umri wa miaka mitatu hadi sita.

Pana mbinu tafauti za kutumika.
Kuna kuwa na madarasa ya baby class, na toddler class. Lakini kwa Afrika watoto wengi huanza chekechea baada ya kuacha kunyonyonya.
 
Kuna kuwa na madarasa ya baby class, na toddler class. Lakini kwa Afrika watoto wengi huanza chekechea baada ya kuacha kunyonyonya.
Do not let school interfere with learning, sijui nani alisemaga hiyo.

Mtoto anatakiwa awekewe mazingira ya yeye kujifunza mwenyewe. Rejea zifuatazo ni muhimu:



 
Back
Top Bottom