Uwekezaji hati fungani BOT

Dit000

JF-Expert Member
Apr 21, 2017
656
856
Habari ndugu zangu naomba wanauchumi wanisaidie vitu hivi
  1. Nimejalibu kupitia bond investment calculator ya BOT, nimejalibu kuweka tsh mil 500,000,000 kwa muda wa miaka 25 na nikabofya calculate nimeletewa kama picha inavyooenesha, sasa hio faida ya kila mwaka wameipata kwa kuzingatia bid ya shingapi katika kila mia unayoinunua?
MMM.PNG


2. hivi unatumia mbinu gani kushinda tender za hizi mikataba, nimejalibu kuangalia majibu ya mnada watu ni wengi sanaa , je upatikanaji wake ni sawa na tenda za barabara yaani unaweza honga ukapewa BOQ ukajaza kama ilvyo then mmoja wa member kwenye procurement anakusaidia hadi unapata kazi sasa sijajua kwa upande wa hizi BONDS

3. Nimeona kuna watu wamejaza bid za 99 kwenye shiling 100 sasa nawaza anapata kweli faida?? yaani hesabu nazoletewa kwenye calculator ni tofauti kabisa majibu yanakuja namba kubwakubwa sasa sijui wao kwenye mahesabu yao wanatumia bid ya shingapi kwa kila tsh 100 kupata hizi figure kubwa kwenye calculator yao.

4. Je, kati ya competitive na non competitive auction ipi ni nzuri? Nimeangalia naona kwenye competitive serikali imetenga pesa ndefu na kwenye non competitive auction pametengewa pesa ndogo sijajua kwa nini

5. Mwisho baada ya kupitia video moja ya BOT wakiongelea haya mambo nimejifunza kwamba , hii mikopo ama bonds zinatolewa na BOT kwa lengo la kutoa fedha kwenye mzunguko kama kuna wingi wa fedha kwenye mzunguko kunaweza leta mfumuko wa bei pia wanatoa bond ili kufanikisha fedha iliyopelea kwenye miradi ya maendeleo

Karibuni ndugu tubadilishane mawazo yaani mi mweupe kabisa kichwani kwenye haya mambo
 
Back
Top Bottom