Uwekezaji binafsi wa umeme una faida kwa TANESCO na Watanzania?

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,730
520
Rais leo amepokea wageni,Kampuni ya Siemens na Wachina wanaotaka kuzalisha umeme mwingi na kuunganisha mikoa yote kwenye gridi ya taifa.Uwekezaj huu na mwingine wowote unaopangwa kufanyika unanipa mashaka makubwa kwenye maana Unapoka jukumu la TANESCO kuzalisha umeme na kuathiri uwezo wa kifedha wa shirika hilo la umma
na itaongeza gharama za umeme na mwananchi atabeba mzigo mzito kwa TANESCO watakuwa wakala wa makampuni hayo, itabidi waongeze tariff waweze kujiendesha na kuwalipa wawekezaji hao.
 

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
5,355
6,379
Uwekezaji si kitu kibaya ndugu!. Kama uwekezaji unafanywa na rate ni nzuri hakuna tatizo lolote kwani badala yake ni kuwafanya Tanesco wafanye hizo shughuli ambazo kila mtu anafahamu kuwa hawawezi na Tanesco yenyewe inawashinda. Wananchi hawawezi kuingia kwenye mipango ya kusaidiwa na goverment kila siku imefika wakati wa makampuni binafsi kusambaza umeme vijijini na mikoani na kuweka umeme wa uhakika kwa wawekezaji hasa wa viwanda. Wananchi sasa wanalipa zaidi kwani inabidi watu watumie majenereta, vibatari, biashara zinazotegemea umeme zimefungwa, gharama ya uendeshaji wa biashara umeongezeka, kuna biashara ambazo zimesimama mpaka swala la umeme lieleweke .n.k Kwani Tanzania tuna tofauti gani na nchi zingine kila siku tunalalamika umasikini lakini tumekuwa watu wa kupenda kila kitu kifanywe na serikali. Tatizo la umeme sio uwekezaji bali ni Tanesco na serikali!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom