Uwekaji wa stampu maalum za kodi katika bidhaa za filamu na muziki nchini tanzania

sulphadoxine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
2,257
644
Serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania,kupitia mamlaka ya mapato tanzania(TRA),kwa kushirikiana na BASATA,Bodi ya Filamu Tanzania(TFCB),chama cha hakimiliki na hakishiriki Tanzania (COSOTA) na wizara ya habari,vijana,utamaduni na michezo inapenda kutoa taarifa kwa wasanii wote hapa nchini hasa wale wa tasnia za filamu na muziki,wakuzaji sanaa(promoters)wazalishaji(producers),waagizaji (importers),wasambazaji(distributors) na umma wote kwa ujumla kuhusu kuazishwa kwa utaratibu mpya wa uwekaji wa stampu maalum kwenye bidhaa za filamu na muziki kuanzia mwezi januari,2013.
 
Utaratibu wenyewe upoje? Stamp zitapatikana wapi? Kwa gharama ipi? Vipi kuhusu bidhaa za muziki na filamu ambazo tayari zipo sokoni na hazina stamp?
 
Utaratibu wenyewe upoje? Stamp zitapatikana wapi? Kwa gharama ipi? Vipi kuhusu bidhaa za muziki na filamu ambazo tayari zipo sokoni na hazina stamp?

Wasanii wote wa tasnia ya filamu na muziki hapa nchini,waagizaji,waingizaji wa kazi za sanaa za filamu na muzki kutoka nje ya nchi,wahamasishaji,wazalishaji na wasambazaji wa kazi za sanaa hapa nchini wamnatakiwa kujisajili katika mamlaka ya mapato tanzania kwa ajili ya kupatiwa namba ya utambulisho wa mlipa kodi(TIN) ikiwa bado hawana namba hiyo na kisha kusajili kazi zao mpya ambazo hazijainginzwa sokoni. Kuanzia januari 3/2013 hakuna kazi yoyote ya filamu na muziki itakayoruhusiwa kuzalishwa ,kuyingizwa kutoka nje ya nchi kibiashara au kusambazwa na mtu yeyote au kikundi chochote bila kupata usajili rasmi katika mfumo mpya wa urasimishaji wa kazi za tasnia za filamu na muziki ikiwa ni pamoja na uwekaji wa stampu maalumu za kodi zitakazo tolewa na TRA.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kwa upande wa kazi zote za filamu na muziki ambazo tayari zimeishaingizwa sokoni ni wajibu wa msanii(au mrithi wake anayetambulika kisheria) pamoja na msambazaji wake kuhakikisha kuwa kazi hizo zinakusanywa ili ziweze kuwekewa stampu kanla ya tarehe 1/7/2013. Baada ya kipindi hicho hakuna kazi yoyote ya filamu au muziki itakayoruhusiwa kuzalishwa au kurushwa katika vyombo vya habari au kutumiwa na kampuni yoyote ya kibiashara kama vile kampuni za simu au vikundi vya burudani bila kazi hiyo kuwa awali imesajiliwa rasmi katika vyombo husika na kuwekewa stampu maalumu za kodi.
 
Lakini bado na wasiwasi kidogo kama kuna elimu imetolewa kuhusu hili swala.
 
Back
Top Bottom