Uwaziri wa Kitwanga ni kashfa nyingine inayojitegemea

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Hivi sasa sehemu nyingi za vijiwe katika jiji la Mwanza kuna mijadala isiyo rasmi imezagaa kuhusu Rais Magufuli kukengeuka kauli yake kwamba katika suala la rushwa hatamtazama mtu yeyote usoni.

Mjadala mkubwa unahusu kashfa wanayoiita 'Lugumigate' inayomhusu Said Lugumi, kijana ambaye ktk jiji hili maisha yake ni ya kupigiwa mfano kwa jinsi alivyonyanyuka toka mburashi viatu hadi kufikia hatua ya kuitikisa serikali ya Magufuli na kumfanya Rais akiuke kauli yake hiyo na kuamua kuwatazama usoni wahusika wakubwa wa kashfa hiyo Said Lugumi na Charles Kitwanga bila kuwa na hatua ya kuchukua.

Mashaka hayo yanapelekea kufikiria kwamba kutokana na urafiki wa mheshimiwa Rais na Kitwanga, huenda fedha iliyotokana na malipo ya kazi iliyofanywa na kampuni za Infosys na Lugumi ndizo zilizotumika katika kampeni za JPM, Kitwanga akimchangia kama rafiki na si kama mfanya biashara maana Rais aliishakanusha kwamba hakuna mfanya biashara aliyemchangia.

Mjadala huu pia unagusa hisia kwamba inawezekana nafasi ya uwaziri wa Charles Kitwanga ya wizara ya mambo ya ndani ulikuwa mpango uliopangwa makusudi wa kumpa wizara hiyo ili kupitia wizara hiyo inayohusika na polisi maslahi yake na wenzie yalindwe.

Wanywa kahawa hao wanaendelea kulonga pia kwamba kuchelewa kuchukua hatua kali kama zilivyochukuliwa kwa wengine wa Bandari na TRA ni kuwapa mwanya watuhumiwa wa kashfa hii wajipange, wafiche mazonge zonge yote hatarishi. Na kwamba ndiyo maana jambo hili haliguswi na Takukuru kwa nguvu eti zimeachiwa kamati za bunge ambazo hazina ujuzi wowote wa kupeleleza ila kuhoji tu kwa kawaida.

Katika mijadala hiyo kuna uongo uongo pia kwamba siri ya jambo hili ilipenyezwa kwa wajumbe wa kamati ya PAC na imekomaliwa na wakwasi wa mtandao wa wafanya biashara ya madawa ya kulevya waliokamatwa na waziri Kitwanga kama kulipiza kisasi vinginevyo suala hili lisingefika mbali.

Kuna vichakubimbi vingine navyo vimekomaa vikidai kwamba hata kufutwa kuonyeshwa live mijadala ya bunge kumetokana na nguvu ya pesa iliyopenyezwa na mafisadi hawa ili kuficha jambo hili na mengine kama haya yasionyeshwe kwa wenye nchi ili wasione jinsi kodi yao inavyopigwa na wajanja wachache.

Kama haya mawazo yao yana chembe ya ukweli basi tuna safari ndefu ya kwenda hata kuifikia vita halisi ya rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.
 
Sasa wanywa kahawa wana weledi gani wa mambo ya uchunguzi kuhusu rushwa?wacha vyombo vyenye dhamana kuhusianana mambo ya rushwa pamoja na bunge vifanye kazi zao,Kitwanga ndio kaanza kazi zamazaawamu ya 5 wakati Lugumi ipo wakati hata Kitwanga hajakuwa waziri wa mambo ya ndani
 
Mafisadi watajenga urafiki wa karibu sasa hivi watamtumia Kitwanga kama daraja kufika ngambo ya pili! Wameshaona jamaa hagusiki
 
Sasa wanywa kahawa wana weledi gani wa mambo ya uchunguzi kuhusu rushwa?wacha vyombo vyenye dhamana kuhusianana mambo ya rushwa pamoja na bunge vifanye kazi zao,Kitwanga ndio kaanza kazi zamazaawamu ya 5 wakati Lugumi ipo wakati hata Kitwanga hajakuwa waziri wa mambo ya ndani
Lugumi si keshakwambia kampuni ambayo kitwanga ni mkurugenzi ilipewa tendar?
 
Back
Top Bottom