Uwaziri na ubunge mwisho uwe miaka kumi(10)tu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uwaziri na ubunge mwisho uwe miaka kumi(10)tu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fungu la kukosa, Feb 11, 2011.

 1. F

  Fungu la kukosa Member

  #1
  Feb 11, 2011
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu wana JF, ufisadi wa malizi za umma umekisiri hapa nchini ketu. Wabunge na Mawaziri wamekuwa wakijifanyia mambo kiholela na kuwaibia wa tanzania mchana kweupe. Wizi kama ule wa RICHMUD, EPA na LOLIONDO ni mifano hai ya matendo ya kifisadi iliyofanywa na viongozi wetu.Hii inatokana na wao kuona nafasi hizo walizopewa na wananchi kama ngozi ya miili yao. Yaani watakuwa nazo hadi siku ya wao kuingia makaburini mwao. Nina shauri muda wa wao kuwa madarakani upunguzwe na uwe miaka kumi tu kama ilivyo kwa maraisi. Hakuna haja ya mtu kama Kingunge, Mzindakaya, Malekela na Luwasa kugombea ubunge na hataimaye kuchaguliwa tena kuwa mawaziri wakati tuna damu changa wasomim kibao.Hiyo katiba itakayoundwa siku zijazoi iwe na kifungu kitakacho tamka wazi wazi kuhusu nafasi za wabunge na mawaziri na muda wao wa kulitumikia Taifa.Nchi ni yetu wote wazee kwa vijana,hivyo, kila mtu anafursa na haki sawa ya kulitumikia Taifa letu na si kwa wazee tu kama malekela na Mzindakaya, watu ambao wameshapitwa na wakati. Hima wana JF, fumbueni macho na mlitete swala hilo kwa nguvu zote.
   
 2. bluetooth

  bluetooth JF-Expert Member

  #2
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 3,933
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  kipindi cha uongozi au chaguzi kiwe miaka 4 minne
   
 3. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #3
  Feb 11, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Kaka,

  Amna tatizo la kiongozi kupewa muda wa kusimamia kama analeta mabadiliko na anakubalika, lakini kisicho kubalika ni viongozi wezi kuendelea kushika uongozi. Hapa ndio kwenye matatizo yetu makubwa ya kikatiba kuto wajibishana kiutendaji na uwizi. Tumefanya secta ya sheria hiwe kwa sababu ya kuwalinda viongozi wabadhirifu, mijizi mikubwa katika jamii, wafanya biashara matajiri na kuwa kamata vibaka wa mtaani tu.

  Hawa wanaoliletea taifa hasara kubwa kiasi watu wanakosa huduma muhimu za afya na kufa kwa sababu za umaskini wanapeta. Umaskini unaotokana na viongozi wabadhirifu kuchota utajiri wa nchi au kuugawa kwa wageni bila ya kuadhibiwa japo hata kwa kufukuzwa kazi. Mpaka hapo tutakapo weka kipaumbele kwenye sheria dhaifu amna mabadiliko yatakayo kuja haraka na wezi watapeta wapewe siku au miaka kwenye uongozi wataiba tu kwa kujua sheria ina namna ya kuzungukwa.
   
 4. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #4
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  yes, there should be a time limit , this will motivate them to be more responsible and accountable to the society while fostering the economic development
   
 5. sijuikitu

  sijuikitu JF-Expert Member

  #5
  Feb 11, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sio kwamba itawafanya wachukue chao fasta wale kona?
   
 6. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #6
  Feb 11, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mapendekezo tu:
  Nakubaliana na miaka 10
  Wawe ndio wasimaniaji wakuu wa shughuli za mikoa na wilaya
  Kuwapo na muundo unaoweza kuwawajibisha katika majimbo yao, kabla hata ya hiyo miaka 10.
  Wakuu wa mikoa wafutwe
  Nakuu wa wilaya wafutwe, sijui na wakurugenzi wabaki?
  Kazi zao zichukuliwe na wabunge.
   
Loading...