Nimeona 'Tweet' ya Ansbert Ngurumo akikosoa hatua ya mtuhumiwa Wa uhujumu uchumi kurudisha pesa zikiwa kwenye maboksi na utaratibu wa rais Magufuli kuwasaidia wananchi mbalimbali anapokuwa katika ziara mbalimbali za kikazi.
Kinachowasumbua NGURUMO na watu wengine Wa aina hiyo ni uwazi Wa Rais Magufuli. Watanzania hawakuzoea kuona mambo yakifanyika kwa uwazi namna hii.
Watuhumiwa wa uhujumu uchumi waliorejesha fedha ni wengi lakini aliyerudhisha fedha kwa njia ya maboksi ni mmoja, ni yule aliyekuwa akipokea mil.7 kwa dakika. Fedha hizo zimerudi kwa mtindo huo kwa vile zilikuwa zimefishwa kwenye maboksi hivyo hivyo, hazikuwa benki. Labda kosa la Serikali ni kuzionesha waziwazi. Ansbert alizoea mambo ya gizani gizani. Lakini mbona hakuhoji pesa zilizorudishwa kwenye maboksi na Serikali ya Kenya pamoja na Dhahabu baada ya kukamatwa nchini humo?
Rais kuwapa wananchi wenye shida pesa taslimu wakati akiwa kwenye ziara zake eti nalo ni suala la kukosoa! Hivi mtu ambaye anakosa sh. Laki 5 Ansbert anataka awekewe pesa hivyo kwenye akaunti? Kwanza hiyo akaunti ya benki mtu huyo anayo? Mgonjwa anayehitaji msaada wa hapo hapo awekewe pesa benki kwanza?
Malipo ya kuchukua maiti hospitalini pia? Lakini kubwa katika hili bado linabaki kuwa ni uwazi, unajuaje kama Rais akitoa msaada kupitia benki kama pesa hizo zitamfikia mlengwa zote na kwa wakati?
Watanzania wengi wameelewa nia ya dhati ya Rais Magufuli kwa Wananchi wake, hawa akina ANSBERT NGURUMO wanateseka bure
Hongera Taifa Stars kwa kututoa kimaso maso huko Sudan.