Uwazi wa Mikataba katika Sekta ya Uziduaji (Mafuta, Gesi na Madini)

Uwakirishi wa mbunge wako sio kupiga kelele bali ni vitendo. Pitapita uone kafanya nini jimboni? This is the best tool to measure his/her perfomance. Unataka umuone kwenye TV live kule Dodoma? Achana na mauzauza amefanya nini? Kama hajafanya chamaana tupa kule 2020.
Unajua kazi ya Mbunge? Mbunge Ana kazi Tatu tu.. Soma elimu ya uraia na katiba ya JMT! Mbunge afanye nini jimboni anakusanya Kodi? Nyie watu aisee..
 
Uwakirishi wa mbunge wako sio kupiga kelele bali ni vitendo. Pitapita uone kafanya nini jimboni? This is the best tool to measure his/her perfomance. Unataka umuone kwenye TV live kule Dodoma? Achana na mauzauza amefanya nini? Kama hajafanya chamaana tupa kule 2020. Muulize pia pesa ya jimbo kaifanyia nini? Kama yote kala mwenyewe na familia yake achana nae.

Yeah... Best response, he needs to understand this from deep of his thinking !!
 
Usiri ni harafu ya unyanganyi,nakumbuka chadema alikuwa mbogo bungeni kuhusu mikataba ya madini na gesi asilia lakini serikali ilishindwa kuiweka wazi.
Tuseme tu huwezi kuwa wewe ni mwizi mzoefu au jambazi sugu na mshtakiwa wewe harafu ukawa ndio hakimu.
Walioweka sahihi mikataba hiyo wengi wao wako hai,kwanini Magu asiwaburuze sehemu usika kama mahakama ya kijeshi wakatupa kilichochetu nasi tukawapa haki yao yaani kitanzi?
Kwanini tunafukuzana na digidigi na kuwaacha tembo mashambani?
 
Serikali inapokubaliana na makampuni binafsi katika kuchimba maliasili wananchi huwa na haki ya kujua kile kilichokubaliwa.

ANGALIA VIDEO:



Meneja wa kampeni Oxfam, Jovita Mlay anasema: “Serikali imeingia kwenye mikataba kadhaa kwenye sekta ya Uziduaji lakini wananchi hawajui ni kitu gani kipo kwenye hiyo mikataba.”

Kikatiba inaelezwa kwamba wananchi wana haki ya kupata taarifa na rasilimali hizi ni mali ya wananchi na Serikali imepewa dhamana ya kuzishika rasilimali hizo, hivyo ni muhimu kwa wananchi kujua na kuelewa ni nini kinafanyika kwenye rasilimali zao na Serikali yao imeingia kwenye mikataba ya aina gani.

Pia upepo wa kiuchumi unaonesha kwamba sekta ya Uziduaji inakua na kuendelea kutokana na teknolojia mpya na makampuni ya uwekezaji yanazidi kuja nchini kwa wingi. Hivyo kutokana na ukuaji huo ni vizuri kuelewa ni mikataba ya aina gani Serikali ya Tanzania inaingia na makampuni hayo ya uwekezaji.

Meneja wa Programu kwenye chama cha wanasheria Tanganyika (TLS), Steven Msechu anasema: “Uwazi wa mikataba kwenye sekta ya Uziduaji ni kitu ambacho wananchi wamekuwa wakidai kwa muda mrefu na tumeona ni kitu muhimu kuwepo kutokana na sababu kadhaa.”

Sekta ya uziduaji ni sekta yenye rasilimali ambazo zinakwisha na ni sekta ambayo katika utekelezaji wake huharibu sana mazingira hivyo ni vizuri kuweka tozo stahiki itakayosaidia baadaye na ili wananchi waifahamu tozo iliyopo ni lazima kuufahamu mkataba unasemaje.

Sekta ya uziduaji imekuwa ikiendeshwa kwa usiri mkubwa na pamoja na kuwepo kwa madini na mafuta kwa kiwango kikubwa lakini bado umasikini ni changamoto kubwa sana.

Kutokana na hali hii ndiyo maana ndiyo maana ni vizuri kujua kwanza mikataba inasemaje na kwa kufanya hivi itakuwa rahisi kuishauri Serikali juu ya nini cha kufanya au kurekebisha.

Thamani ya mkataba haipo kwenye fedha tuu maana yenyewe hubeba fedha na hasara zinazoweza kujitokeza, ikiwemo hatua za kupunguza uharibifu wa mazingira na haki ya uwazi.

Ni msukumo mzuri kwa Serikali kuhakikisha wanaingia kwenye mikataba yenye manufaa kwa wananchi ambao kimsingi ndiyo wamiliki wa rasilimali za taifa.

Uwazi wa mikataba ni njia mojawapo ya kuhakikisha pande zote zinafaidika kwenye shughuli za Uziduaji.

Tanzania ilipitisha sera ya uwazi na uwajibikaji katika sekta ndani ya sheria ya mwaka 2015 na dhumuni kubwa ni kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya Uziduaji.

Sheria inaitaka Serikali kuweka mikataba wazi kupitia Waziri wa madini ambapo kamati ya madini hulazimika kumuhimiza waziri katika kuhakikisha anatekeleza jukumu hilo kwa manufaa ya wananchi.

Mpaka sasa ni miaka takribani 3 tangu sheria ipitishwe lakini mikataba bado haijawekwa wazi. Kutokana na utafiti uliofanywa na HakiRasilimali unaonesha kwamba Wizara ya madini ipo kwenye hatua nzuri ya kuhakikisha mikataba inawekwa wazi.

Asasi za kiraia kupitia mtandao wa HakiRasilimali zinapendekeza kwamba mchakato mzima wa uandaaji wa mikataba uwe wazi, wa haki na wenye ufanisi. Kutokea kwenye hatua za upangaji, utoaji wa zabuni, ugawaji linganifu, na utoaji wa mikataba hadi utekelezaji.

Hivyo wananchi wanashauriwa kuendelea kudai taarifa kuhusu utayarishwaji wa mikataba kwa umma, muundo wa uendeshaji shughuli, mapato, tathmini ya matokeo ya mazingira na mgawanyo wa mapato yanayotokana na shughuli za sekta ya madini, mafuta na gesi.

Raia wa tanzania sio wazalendo wako karibu Sana na mabeberu ,na sasa wanatumia Hadi simu za viganja za mabeberu . Wazalendo wa tanzania ni viongozi tu na hasa wale wa ccm .
 
Mungu aliweka ile mti wa matunda katikati ya bustani ya Eden ili Adam na Hawa wasile wala kugusa matunda yake. Nyie mnataka kujua mkataba wakati ni kama ule mti wa ujuzi. Halafu mkishayajua muanze kuzungusha gurudumu. Mmmm haiwezekani
 
Maoni yangu:

Si kama watanzania ni wajinga kama watunga sera wanavyoweza kuwadhania, ila wanaopewa fursa ya kuendesha nchi wakishapata madaraka wanajisahau sana. Hizi dharau za viongozi wetu ambao wamegeuka watawala ndo zimetufikisha hapa.

Mikataba ikiwa wazi tena kwa lugha yetu ya Taifa (Kiswahili) itapelekea kila mtanzania kutambua ananufaikaje na rasilimali zinazopatikana nchini mwake.

Ni upuuzi mkubwa kwa waliopata mamlaka kutuchukulia poa na kuendelea kuchezea rasilimali zetu kwa kificho na kushibisha matumbo yao na jamaa zao wakidhani mwisho wao wana maamuzi yao!

Kwa leo naishia hapa

Mikataba kwa lugha ya taifa????? Labda mikataba ya nyumba za kupanga. Kwanza hata ikiwa wazi hamtaisoma. Mlivyo wavivu wa kusoma!!!!!!
 
Back
Top Bottom