Uwazi wa Mikataba katika Sekta ya Uziduaji (Mafuta, Gesi na Madini)

Mikataba sisi tunapenda kufanya kificho

Ova



Kwani umesahau mkuu, si wale wahenga wetu waliotufundisha ile kauli kwamba "" ukila na kipofu usimguse mkono"". Sisi wananchi tumekuwa vipofu kwa muda mrefu sana.
 
Inafaa pia kwa wanasheria wa Tanzania kujikita kuwapa wananchi uelewa wa sheria mbalimbali za nchi kuliko kukalia kuwachafua viongozi na kuwalaumu pindi wanapokosea katika sheria
 
Tatizo ni utayari wa kuisoma na kuielewa.

Ukweli ni kwamba kama kuna upigaji ni wakati wa kusainishana hiyo mikataba

Wengi mnajua mambo yalivyokua huko nyuma mfano mtu anainflate gharama za ujenzi wa miundo mbinu ili apewe cha juu

Vivyo hivyo ndio imekua kwenye mikataba mingine kama ya madini

ndio maana leo Magufuli analia kila kukicha anajua kilichofanyika na tiyari mikataba imeshasainiwa.
 
Sikubaliana ya kusema watz ni mambugila!

Waweke hiyo mikataba wazi wananchi waisome na kuielewa!

Lkn kama sasa hv mikataba mingi inayoingia serikali jumba kule dom kwenyewe hawashirikishwi sembuse sisi wananchi tutaletewa!

Ova
 
Ni msukumo mzuri kwa wananchi kudai uwazi wa mikataba.

Lakini changamoto kubwa zaidi ni ya kisheria. Kanuni za kimataifa zinasisitiza juu ya usiri wa wanaoingia mikataba. Na mara nyingi wawekezaji hawapendi uwazi huu (kwa nia njema au mbaya). Hivyo ni hatua yenye kupata ukinzani mkubwa wa kisheria. Ila ni hatua muhimu ya kupongezwa.
 
Kama wananchi! Kuna kitu tunapaswa kuwafunza hawa viongozi, nacho ni "UWAJIBIKAJI" vinginevyo wataendelea kuvunja katiba wapendavyo na watakavyo ila vunja wewe raia sasa!! Jasho litakutoka!
Wananchi wanaweza kuwafutilia watumishi wa serikali kama hao wananchi nao ni wanaajibika kwa nafasi zao. Umeshasikia walipa kodi hii nchi ni 2.2m tu. Unadhani tungekuwa tunawalipa kodi 30m tungeruhusu pesa zitumike bila uwajibika? Watu kusoma ni shida, Nchi hii library nzuri hazifiki hata 3? watakwambia wanasoma online ukiwauliza apps za vitabu hawajui Zaidi ya facebook na insta.
 
Uwazi bila kusahau uwezeshaji (capacity building ) kwa wale maofisa / viongozi tunaowatuma kusaini mikataba kwa niaba yetu ni muhimu ili mikataba hiyo iwe ya manufaa.

Tumeona kelele nyingi kuwa kumeshasaini mikataba mingi ambayo ni mibovu, sababu mojawapo ni kukosekana kuwa na wataalamu wenye uzoefu wa kuendesha mazungumzo, maelewano na hatimaye mwishoni kupelekea utiaji saini mkataba mzuri na wawekezaji toka pande yeyote ya dunia.
 
hahahaha...inaonekana baadhi yetu raia tuna maneno ya "kichochezi" ndio maana tunafichwa
Ukisema hivi unatukosea kwani lengo la jf ni kusaidia kujenga hoja mbadala kulingana na uelewa wetu juu ya jambo fulani na huenda wengine ni wataalam katika jambo hilo ambao wapo nje ya mfumo husika na wengine ni wadadisi ambao wana maarifa zaidi kushinda watendaji waliopo kwenye mfumo! Kusema ni uchochezi ili hali mmetofautiana kimtazamo ni makosa!
 
In principle, all official documents za serikali zinatakiwa ziwe open to public kuanzia ngazi za kijiji hadi Ikulu.

Wafanyakazi wa serikali na wote wanaoshika nafasi za kisiasa wanawajibika kwa wananchi. Jamii ikielewa hili mbona mambo mengi yangekuwa rahisi sana.
 
Sikubaliana ya kusema watz ni mambugila!

Waweke hiyo mikataba wazi wananchi waisome na kuielewa!

Lkn kama sasa hv mikataba mingi inayoingia serikali jumba kule dom kwenyewe hawashirikishwi sembuse sisi wananchi tutaletewa!

Ova
Wameona hatuhoji sasa wameamua kutudharau kabisa na ukihoji unatishiwa jele.
Wacha wawaamshe waliolala then tutaelewana tu.
 
Kwanini tumelazimishwa kusoma huu uzi?
Kuna wakati lazima mtu alazimishwe kufanya jambo la msingi na faida kwake na jamii nzima.

JF imetaka watu wengi watambue uwepo wa hii sheria na udhaifu wa mamalaka husika kuitekeleza kama zilivyo sheria zingine kama za uhalifu wa mitandaoni au sheria mpya ya posta na simu au ile ya vyombo vya habari.

Kawanini sheria hii haijapewa kipaumbele na serikali yetu ya awamu ya 5 inayojipambanua kupinga ufisadi, kusimamia uwajibikaji, kukomesha rushwa na kusimamia uvunaji mzuri wa maliasili zetu.

Kuna faida gani kuwa na mahakama ya kushughulikia makosa ya ufisadi huku hatutekelezi sheria itakayowezesha kuwaaanika hadharani na kuwabaini mafisadi na wabadhirifu wa mali za umma kama maliasili?

Mwisho naomba tu niimbe kobwagizo cha wimbo maarufu unaosema "SIRI YA NINIII...?"
 
Kwani muswada umekwisha andaliwa au uko bunge tayari?! Kama itakuwa hivyo, ndiyo tutakuwa wa kweli tofauti na hivyo tutakuwa tutakuwa tunapiga story maskani.
Mwenye kujua hilo naomba anijuze ili tuangalie utaratibu wa kuanza kusifiana na kupongezana.
 
Saratani komavu nyingine tuliyonayo ni wanasheria.

Tanganyika Law Society wanatutoa wasiwasi kwamba wizara iko mahala pazuri katika hatua za uwekaji wazi mkataba, japo huu ni mwaka wa tatu tangu sheria ya kutaka uwazi ipitishwe na hakuna mkataba uliowekwa wazi.

Nilikuwa nasubiri mwanasheria huyu atuambia walichomwambia huko wizarani wako katika hatua nzuri maana yake nini, kuna mkandarasi wa IT anamalizia malizia kupandisha document kwenye website mwaka wa tatu?

Karatasi ikishasainiwa aidha inawekwa kabatini milele au nakala zinasambazwa kwa waandishi hapo hapo. Tupo hatua nzuri maana yake makaratasi yamepelekwa jeshini kwa kazi ya kutolewa nakala? Sidhani kama TLS ya Tundu Lissu ingepozwa kwa hadaa kama hii na kuja kutughilibu kwa maneno matamu ya "wako katika hatua nzuri." Especially baada ya serikali kutangaza wazi wazi kwamba imejuta kuweka wazi makubaliano yao na Accacia-Barrick. TLS ya Fatma Karume wanatuambia serikali iko katika hatua nzuri!
 
Back
Top Bottom