Uwazi na uwajibikaji wa Rais Samia unafurahisha

Maryam Malya

Senior Member
Nov 29, 2021
115
258
FedhazaUviko19. Hadi Desemba 31, 2021, jumla ya shilingi bilion 774.67 zilikuwa zimeshatolewa kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali kutokana na fedha za UVIKO-19.

Mchanganuo;

Sekta ya Maji ilipata shilingi bilioni 139.4,
Sekta ya Afya ilitengewa shilingi bilioni 466.8, Sekta ya Elimu ilipata shilingi bilioni 368.9, mfuko wa wajasiriamali shilingi bilioni 5,
Hifadhi ya Jamii bilioni 5.5, Maliasili
Utalii shilingi bilioni 90.2.

Kati ya fedha zilizotolewa , shilingi bilioni 304 zilitengwa kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa madarasa 15,000 ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, pamoja na mabweni 50 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili kupunguza msongamano kwa wanafunzi.

Mpaka sasa Wizara ya Elimu imeshapokea shilingi bilioni 47.7 na kuzipeleka katika taasisi ambazo wanazisimamia ikiwemo VETA. Shilingi bilioni 28.7 ni kwa ajili ya ujenzi wa vyuo 25 vya VETA vya Wilaya na shilingi bilioni 19 ni kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyuo vinne vya VETA ngazi ya Mkoa.

Sekta ya Afya ilitengewa jumla ya shilingi bilioni 466.8. Fedha zilizopokelewa hadi sasa ni shilingi bilioni 86.6. Katika Sekta ya Afya shilingi bilioni 39 zimelipwa kwa ajili ya vifaa vya usimikaji wa tiba mtandao, tafiti na ujenzi wa ICU na EMD, kiasi kingine kilichobaki ni kwa ajili ya ununuzi wa magari 96.

Wizara ya Maji ambayo ilitengewa kiasi cha shilingi bilioni 139.4, utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya vijijini hususan taratibu za manunuzi kwa miradi yote 172 zimekamilika na ujenzi upo katika hatua za awali katika baadhi ya maeneo.

Utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya mijini umeanza katika miradi 44 na mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ikiwemo kukamilisha taratibu za manunuzi. Mwenyezi Mungu ampe nguvu Rais Samia aendelee kuijenga nchi yetu(Takwimu zinatokana na Hotuba ya Waziri wa Fedha siku ya 04 Januari 2022).

#SisiTumekubali #kaziinafanyika
 
Hela za makato ya tozo za simu, mpaka sasa zimekusanywa kiasi gani na zimetumika vipi.
 
Zimekusanywa kiasi cha Bilioni 161.59, na Bilioni 91.66 kwenye mikopo ya Elimu ya Juu, Bilioni 58.2 kwenye Sekta ya Afya, Bilioni 7 kwenye sekta elimu
 
Mama ndie ana haki ya kuongezewa miaka ya kuongoza badala ya miaka mitano iwe miaka saba sio yule mwanakwenda
 
FedhazaUviko19. Hadi Desemba 31, 2021, jumla ya shilingi bilion 774.67 zilikuwa zimeshatolewa kwaajili ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika sekta mbalimbali kutokana na fedha za UVIKO-19.

Mchanganuo;

Sekta ya Maji ilipata shilingi bilioni 139.4,
Sekta ya Afya ilitengewa shilingi bilioni 466.8, Sekta ya Elimu ilipata shilingi bilioni 368.9, mfuko wa wajasiriamali shilingi bilioni 5,
Hifadhi ya Jamii bilioni 5.5, Maliasili
Utalii shilingi bilioni 90.2.

Kati ya fedha zilizotolewa , shilingi bilioni 304 zilitengwa kwa ajili ya kugharamia ujenzi wa madarasa 15,000 ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, pamoja na mabweni 50 ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu ili kupunguza msongamano kwa wanafunzi.

Mpaka sasa Wizara ya Elimu imeshapokea shilingi bilioni 47.7 na kuzipeleka katika taasisi ambazo wanazisimamia ikiwemo VETA. Shilingi bilioni 28.7 ni kwa ajili ya ujenzi wa vyuo 25 vya VETA vya Wilaya na shilingi bilioni 19 ni kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa vyuo vinne vya VETA ngazi ya Mkoa.

Sekta ya Afya ilitengewa jumla ya shilingi bilioni 466.8. Fedha zilizopokelewa hadi sasa ni shilingi bilioni 86.6. Katika Sekta ya Afya shilingi bilioni 39 zimelipwa kwa ajili ya vifaa vya usimikaji wa tiba mtandao, tafiti na ujenzi wa ICU na EMD, kiasi kingine kilichobaki ni kwa ajili ya ununuzi wa magari 96.

Wizara ya Maji ambayo ilitengewa kiasi cha shilingi bilioni 139.4, utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya vijijini hususan taratibu za manunuzi kwa miradi yote 172 zimekamilika na ujenzi upo katika hatua za awali katika baadhi ya maeneo.

Utekelezaji wa miradi ya maji katika maeneo ya mijini umeanza katika miradi 44 na mingine ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ikiwemo kukamilisha taratibu za manunuzi. Mwenyezi Mungu ampe nguvu Rais Samia aendelee kuijenga nchi yetu(Takwimu zinatokana na Hotuba ya Waziri wa Fedha siku ya 04 Januari 2022).

#SisiTumekubali #kaziinafanyika
mtoto mzr sana wewe, unafaa kuolewa, ndo mwanamke wa kwanza kuona unamtetea samiah

unafaa ujengewe sanamu lako pale posta, tukupe na viti maalumu pale bungeni alafu tukupeleke ikulu ukawe mshauri wa mama.
 
Back
Top Bottom