Uwazi katika mapato na matumizi tozo mpya za miamala ya simu

aniceth medard

New Member
Jul 17, 2021
0
0
makala na ANICETH MEDARD NHUNGW'A mwanafunzi mwaka wa pili ndaki ya afya na sayansi shirikishi mbeya chuo kikuu cha Dar Es Salaam.

"Umetuma TSh 19,000 kwenda kwa mpokeaji wa Vodacom ANDREW M ANDREW- 0767284813. Jumla ya Makato TSh 1,160. (Ada TSh 550, Tozo TSh 610), VAT TSh 84. Salio jipya ni TSh ****. Muamala: 95868689370. 23/07/21 17:48. Tafadhali subiri."

Huu ni mfano wa ujumbe wa uthibitisho unaotumwa na mtandao wa tigo kuthibitisha muamala uliokamilika. Ujumbe huu huonesha mambo mengi ya msingi lakini cha muhimu hasa huonesha salio jipya lililobaki baada ya muamala, VAT na TOZO mpya za serikali kwenye miamala kama zilivyowasilishwa na waziri wa fedha Dk MWIGULU NCHEMBA tarehe 10 juni wakati akisoma bajeti mpya ya serikali kwa mwaka wa fedha 2021/22 na kuanza kutumika tarehe 15 julai 2021.

Katika hotuba ile WAZIRI NCHEMBA alilieleza bunge na umma wa watanzania kwamba serikali inatarajia kukusanya kiasi cha Tsh trillioni 1.3 kutoka tozo za miamala ya simu ambazo zitatumika kwenye utekelezaji wa UNIVERSAL HEALTH COVERAGE( bima za afya kwa wananchi wote bure), ujenzi wa vituo vya afya na barabara vijijini na kumalizia miradi ambayo serikali ya RAIS MAMA SAMIA imeirithi ikiwemo mradi wa reli ya kisasa SGR.

Haya malengo ni mazuri sana na yanalenga masilahi mapana ya taifa lakini changamoto kubwa imekuwa ni namna gani serikali itahakikisha hakutakuwa na ubadhilifu wa fedha hizi za tozo mpya za miamala ya simu? Hii ndio imefanya niandike makala hii.

Hivi ni mtanzania gani kasahau yale madudu yaliyoainishwa na ripoti ya CAG Kichere tarehe 28 machi mwaka huu?
vipi kuhusu ule Mradi wa reli ya kisasa(SGR) unaoonekana kuisababishia serikali hasara ya zaidi ya bilioni 35 kutokana na kuwa na wafanyakazi zaidi ya 1538 katika mradi huo kutoka nje ya nchi na wote hawana vibali?
vipi kuhusu sekta ya utalii ambayo ripoti ya CAG kuwa kumekuwa na upotevu mkubwa wa fedha hasa kwa kufanya malipo yasiyozingatia taratibu zilizowekwa na serikali?
vipi kuhusu ule ubadhirifu wa zaidi ya bil 3.7 bandari ya Dar es Salaam?? na vipi kuhusu makusanyo billioni 18 katika wilaya 135 ambazo hazikupita benki na hivyo fedha hizi kuna uwezekano zimeingia kwenye mifuko ya watu wachache?
Hapo bado hatujagusa ule ufisadi wa zile expert levy za korosha na mradi wa REA! pamoja na miradi mingi tu ambayo imewekwa wazi kuwa kuna ubadhilifu uliopindukia wa fedha za umma, Hii maana yake kusipokuwa na uwazi katika ukusanyaji wa mapato ya hizi tozo mpya za miamala na zenyewe zitaenda kutumika ndivyo sivyo na kufaidisha baadhi ya watu wachache.


MAPENDEKEZO KWA SERIKALI
serikali iweke mfumo wa uwazi kwenye mapato ya tozo hizi za miamala ambazo zitaonesha kwenye miamala kuwa baada ya kukatwa tozo ya muamala alioufanya, makusanyo ya jumla ya tozo izo mpaka yeye anakatwa ni kiasi fulani mfano;

UMETUMA TSh 19,000 KWENDA KWA MPOKEAJI WA VODACOM DIONIZ MWAKULEGA MWANDUTE- 0767******. JUMLA YA MAKATO TSh 1,160. (ADA TSh 550, TOZO TSh 610 JUMLA YA MAKUSANYO YA.TOZO BAADA YA MUAMALA HUU NI TSH 234.37BIL), VAT TSh 84. SALIO JIPYA TSh *****. Muamala: 95868689370. 23/07/21 17:48


Kwa kuongezea baada ya kuoneshwa wazi kwamba pesa iliyopatikana ni kiasi gani sasa tuambiwe kipindi pesa hizo zitakapotumika mfano:


NDUGU OMARY MABIHYA MZALENI KIASI CHA TSH 24 BIL KITATOLEWA KUTOKA KWENYE MAKUSANYO YA JUMLA YA TOZO ZA MIAMALA NA KITATUMIKA KUKARABATI KITUO CHA AFYA BUZA, ASANTE!

Simple like this, ukweli ni kwamba pamoja na mzigo mkubwa ambao tozo hizi unasababisha kwa wananchi ambazo kimsingi inabidi viwango vya tozo hizi vipunguzwe lakini bado pia wapo viongozi ambao hawatajali wataendelea kuiba fedha hizi.
"1Timotheo 6:10:
Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi. "

Ni wakati sasa wa viongozi wa serikali na taasisi yoyote ile kujifunza kufanya maamuzi kwa kuridhiana na kushirikisha wananchi wa hali ya chini kabisa maana wao ndio waliowaweka wao madarakani kama inavyohimizwa kwenye QURAN TUKUFU:

“ambao uongozi [katika mambo yote muhimu na ya pamoja] ni kwa kushauriana baina yao” (Al-Al-Shuura, 42:38)

NHUNGW'A ANICETH M 0654703492, 0772792099
 
Back
Top Bottom