Uchaguzi 2020 Uwasilishaji wa sera za CHADEMA umeshiba na ndio unaoleta kizaazaa Lumumba

Lissu ananadi sera au anatoa MASIMANGO??!
107530571_3426505757394230_3375537061730439151_o.jpg
 
😂 😂 😂 lissu amesoma HKL magu amesoma PCM (PHD), ushawahi ona wap mtu wa pcm anahangaika na kuandika IMLA? magufuli knows how to handle a crisis scientifically i.e corona, lissu anajua kuandika IMLA ya corona! ni sawa na useme doctor ajifunze kuandika, who has time for that?

- viongozi wengi wa chadema hawajaenda shule, mfano mwenyekiti, lema! wnajua kuongea kihuni for that i agree but they can never handle anything as simple as economics
 
Katika hawa watatu uliowataja Dr Slaa alikuwa na uwasilishaji bora kabisa wa hoja na kwa kiasi fulani alifanikiwa kwenda deep hasa kwenye masuala ya chakula, maji na sera ya mambo ya nje.
Ila kwa sasa huyu Tundu Lissu anapiga vizuri sana tena kwa mazingira halisi zaidi kulingana na mahitaji ya kisiasa na kimkakati ya sasa.

Cheers to TL

nkismama katika ukweli then lissu has nothing cha maaana kinachotoka kwenye hizo lipstick zake! mbowe na kutkojua kusoma kwake but he has wisdom, mara nyingi sana anakua hakubaliana na magufuli lakini anajua how to present his ideas!
- For lissu kati ya kopo la cdm kuwahi kutokea ndo lissu sasa to the extent hata mwanzilishi wa chadema mwenyewe edwin mtei hakubaliana nae, such a waste for chadema! uchaguzi umepotea kihovyo kabisa
 
Yuko vizuri sana. Leo akiwa Mbozi katoa somo la katiba mpya akieleza jinsi katiba iliyopo inavyompa madarakka makubwa rais wa nchi na baadaye akaeleza kuwa yeye hataki kuongoza kwa katiba hii, anataka ndani ya siku 100 za kwanza afufue mchakato wa katiba mpya ambapo madaraka yatagatuliwa kwenda chini ili wananchi wawe na mamlaka ya kuwachagua viongozi wao na kupanga maendeleo yao katika maeneo waliyopo. Utapenda anapo anzisha swala hilo na kuwaeleza wananchi....kama yupo darasani.
 
Kuna tofauti kati ya fasihi Andishi na Simulizi. Sera za vyama zimeandikwa na kuchambuliwa kwenye vitabu. Ukiachilia mbali kwamba sio wote wanaweza kupata vitabu hivyo lakini pia sio wote wanaoweza kusoma wakaelewa.

Tundu LISU anatumia muda wake mwingi wa kampeni kunadi sera zake kwa njia ya UHALISIA " Realities " .Jambo hili linawakera sana CCM kwa sababu anachofanya ni kama mwalimu anavyofundisha darasani.

Anaanza kueleza tatizo kwa kulitaja ..Kwa mfano ugomvi wa wakulima na wafugaji. Baada ya hapo anaeleza chanzo cha tatizo hilo..Mfano" Ardhi kubwa kumilikiwa na viongozi wakubwa au kampuni kadhaa na hapa anawataja kwa majina.

Baada ya hapo anaeleza jinsi walivyopata ardhi hiyo,kama ni kwa minajili ya vyeo vyao au kuuziwa isivyo halali au halali. Pia hueleza faida au hasara ya watu hao kujimilikisha ardhi hiyo.

Mwisho anarudi kwenye suluhisho kwa mujibu wa SERA za Chadema au kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuonyesha UDHAIFU na kutowajibika kwa viongozi waliopo.

Huu ni uwasilishaji BORA kabisa wa SERA mpya na ambazo wananchi hawajazizoea au kuzielewa vizuri.

CCM na Tume (CCM) hawakutegemea kuona uwasilishaji huu. Walitamani awe anasoma kama ilivyoandikwa kwenye kitabu. Lakini pia walipenda waone uwasilishaji huo uwe kama alivyofanya Lowasa(2015) ,Dr Slaa(2010) au Freeman Mbowe (2005) ambao walikua wanazisema juu juu bila mifano hai inayowagusa wananchi wa eneo husika.

Hongera Tundu Lissu! shikilia hapohapo watu wanakuelewa sana na pia unawavuruga watu wa Lumumba. Hawana uwezo wa kujibu hoja zako,wanaishia kuandika "Magufuli 5 Tena".
kimenuka bukoba ! kumbe hawakusahau !
 
Attachments

  • Haya Maneno Magufuli aliyasema kagera mwaka 2017.. . . Leo anaenda kuwaomba kura ( 352 X 640 ).mp4
    1.6 MB
Uchaguzi wa urais Chadema wanaweza kushinda - in fact it's theirs to lose but the following must be done first and foremost:

1. Umati wa wahudhuriaji wa mikutano wahamasishwe kupiga kura:
Hili sijaliona Lissu akilisisitiza kwenye speeches zake. inabidi awe akiwahamasisha watu wote wenye kadi wazinyooshe juu au ambaye kaacha home anyooshe kidole. hii itakuwa inawakumbusha wapigaji kura wajibu wao # 1.

2. Kuhakikisha kura zote zinahesabiwa katika vituo vya kupiga kura na kutumwa systematically kwenda kwenye tallying centre(s).

3. Kuhakikisha CREDIBLE representatives wanakuwa deployed wakati wote wa kuhesabu kura na wawe wanapiga picha kurasa zenye matokeo na kuziwasilisha haraka kunakostahili (refer # 2 hapo juu). MUHIMU SANA.
Hizi ni kampeni za urais, sasa kama anafanya vizuri kuwasilisha hoja unadhani wananchi hawajui kwamba kinachopiganiwa ni kura?!

Wananchi watampigia kura Tundu Lissu, ondoa shaka.

Usimamizi ni mgumu sanaa, nchi nzima sio kitu kidogo, hilo jukumu ni la vingozi wa majimbo sasa sio la Tundu Lissu, hawajui watu wa maeneo aendayo, kupata credible people ni jukumu la viongozi wa majimbo ya uchaguzi ,mikoa ,wilaya hadi kata.

Ma ccm majizi lakini tutajitahidi kuyadhibiti.
 
... when it comes to Audience Management, none like Tundu Lissu! Anayekaribiana naye ni Mwl. Nyerere tu.

..anapenda kutumia maneno, "..naomba tusikilizane.."

..halafu akijenga hoja huipa msisitizo kwa kuuliza, " ..si ndio..?"

..au huhakikisha kama ameeleweka kwa kuuliza, "..mmenipata..?"

..ila KIBOKO ni alipokuwa Znz na kusema, "...mimi nikiongea huwa sipendi muziki tafadhali..."

..Tundu Lissu ana mvuto, ana facts, na ana credibility.
 
Kuna tofauti kati ya fasihi Andishi na Simulizi. Sera za vyama zimeandikwa na kuchambuliwa kwenye vitabu. Ukiachilia mbali kwamba sio wote wanaweza kupata vitabu hivyo lakini pia sio wote wanaoweza kusoma wakaelewa.

Tundu LISU anatumia muda wake mwingi wa kampeni kunadi sera zake kwa njia ya UHALISIA " Realities " .Jambo hili linawakera sana CCM kwa sababu anachofanya ni kama mwalimu anavyofundisha darasani.

Anaanza kueleza tatizo kwa kulitaja ..Kwa mfano ugomvi wa wakulima na wafugaji. Baada ya hapo anaeleza chanzo cha tatizo hilo..Mfano" Ardhi kubwa kumilikiwa na viongozi wakubwa au kampuni kadhaa na hapa anawataja kwa majina.

Baada ya hapo anaeleza jinsi walivyopata ardhi hiyo,kama ni kwa minajili ya vyeo vyao au kuuziwa isivyo halali au halali. Pia hueleza faida au hasara ya watu hao kujimilikisha ardhi hiyo.

Mwisho anarudi kwenye suluhisho kwa mujibu wa SERA za Chadema au kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuonyesha UDHAIFU na kutowajibika kwa viongozi waliopo.

Huu ni uwasilishaji BORA kabisa wa SERA mpya na ambazo wananchi hawajazizoea au kuzielewa vizuri.

CCM na Tume (CCM) hawakutegemea kuona uwasilishaji huu. Walitamani awe anasoma kama ilivyoandikwa kwenye kitabu. Lakini pia walipenda waone uwasilishaji huo uwe kama alivyofanya Lowasa(2015) ,Dr Slaa(2010) au Freeman Mbowe (2005) ambao walikua wanazisema juu juu bila mifano hai inayowagusa wananchi wa eneo husika.

Hongera Tundu Lissu! shikilia hapohapo watu wanakuelewa sana na pia unawavuruga watu wa Lumumba. Hawana uwezo wa kujibu hoja zako,wanaishia kuandika "Magufuli 5 Tena".
Porojo tu. Yeye aseme atafanya nini kwa watanzania. Watanzania hata kama hawajui kusoma wanaona picha ya flyover, ndege, hospital, na kadhalika. JPM mbele kwa mbele.
 
Hizi ni kampeni za urais, sasa kama anafanya vizuri kuwasilisha hoja unadhani wananchi hawajui kwamba kinachopiganiwa ni kura?!

Wananchi watampigia kura Tundu Lissu, ondoa shaka.

Usimamizi ni mgumu sanaa, nchi nzima sio kitu kidogo, hilo jukumu ni la vingozi wa majimbo sasa sio la Tundu Lissu, hawajui watu wa maeneo aendayo, kupata credible people ni jukumu la viongozi wa majimbo ya uchaguzi ,mikoa ,wilaya hadi kata.

Ma ccm majizi lakini tutajitahidi kuyadhibiti.
nina uhakika wahusika wameyaona maoni yangu na watayafanyia kazi.

ngoja niongee pointi zangu kwa volume kubwa...

1. kuhamasisha kupiga kura - doable
2. kura zihasebiwe vituoni - doable
3. wawakilishi kuhesabu kura - doable
 
Back
Top Bottom