Ridhwani Mbaraka
JF-Expert Member
- Jun 18, 2017
- 484
- 1,135
Kuna tofauti kati ya fasihi Andishi na Simulizi. Sera za vyama zimeandikwa na kuchambuliwa kwenye vitabu. Ukiachilia mbali kwamba sio wote wanaweza kupata vitabu hivyo lakini pia sio wote wanaoweza kusoma wakaelewa.
Tundu LISU anatumia muda wake mwingi wa kampeni kunadi sera zake kwa njia ya UHALISIA " Realities " .Jambo hili linawakera sana CCM kwa sababu anachofanya ni kama mwalimu anavyofundisha darasani.
Anaanza kueleza tatizo kwa kulitaja ..Kwa mfano ugomvi wa wakulima na wafugaji. Baada ya hapo anaeleza chanzo cha tatizo hilo..Mfano" Ardhi kubwa kumilikiwa na viongozi wakubwa au kampuni kadhaa na hapa anawataja kwa majina.
Baada ya hapo anaeleza jinsi walivyopata ardhi hiyo,kama ni kwa minajili ya vyeo vyao au kuuziwa isivyo halali au halali. Pia hueleza faida au hasara ya watu hao kujimilikisha ardhi hiyo.
Mwisho anarudi kwenye suluhisho kwa mujibu wa SERA za Chadema au kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuonyesha UDHAIFU na kutowajibika kwa viongozi waliopo.
Huu ni uwasilishaji BORA kabisa wa SERA mpya na ambazo wananchi hawajazizoea au kuzielewa vizuri.
CCM na Tume (CCM) hawakutegemea kuona uwasilishaji huu. Walitamani awe anasoma kama ilivyoandikwa kwenye kitabu. Lakini pia walipenda waone uwasilishaji huo uwe kama alivyofanya Lowasa(2015) ,Dr Slaa(2010) au Freeman Mbowe (2005) ambao walikua wanazisema juu juu bila mifano hai inayowagusa wananchi wa eneo husika.
Hongera Tundu Lissu! shikilia hapohapo watu wanakuelewa sana na pia unawavuruga watu wa Lumumba. Hawana uwezo wa kujibu hoja zako,wanaishia kuandika "Magufuli 5 Tena".