Uchaguzi 2020 Uwasilishaji wa sera za CHADEMA umeshiba na ndio unaoleta kizaazaa Lumumba

Ridhwani Mbaraka

JF-Expert Member
Jun 18, 2017
440
1,000
Kuna tofauti kati ya fasihi Andishi na Simulizi. Sera za vyama zimeandikwa na kuchambuliwa kwenye vitabu. Ukiachilia mbali kwamba sio wote wanaweza kupata vitabu hivyo lakini pia sio wote wanaoweza kusoma wakaelewa.

Tundu LISU anatumia muda wake mwingi wa kampeni kunadi sera zake kwa njia ya UHALISIA " Realities " .Jambo hili linawakera sana CCM kwa sababu anachofanya ni kama mwalimu anavyofundisha darasani.

Anaanza kueleza tatizo kwa kulitaja ..Kwa mfano ugomvi wa wakulima na wafugaji. Baada ya hapo anaeleza chanzo cha tatizo hilo..Mfano" Ardhi kubwa kumilikiwa na viongozi wakubwa au kampuni kadhaa na hapa anawataja kwa majina.

Baada ya hapo anaeleza jinsi walivyopata ardhi hiyo,kama ni kwa minajili ya vyeo vyao au kuuziwa isivyo halali au halali. Pia hueleza faida au hasara ya watu hao kujimilikisha ardhi hiyo.

Mwisho anarudi kwenye suluhisho kwa mujibu wa SERA za Chadema au kwa mujibu wa sheria za nchi ili kuonyesha UDHAIFU na kutowajibika kwa viongozi waliopo.

Huu ni uwasilishaji BORA kabisa wa SERA mpya na ambazo wananchi hawajazizoea au kuzielewa vizuri.

CCM na Tume (CCM) hawakutegemea kuona uwasilishaji huu. Walitamani awe anasoma kama ilivyoandikwa kwenye kitabu. Lakini pia walipenda waone uwasilishaji huo uwe kama alivyofanya Lowasa(2015) ,Dr Slaa(2010) au Freeman Mbowe (2005) ambao walikua wanazisema juu juu bila mifano hai inayowagusa wananchi wa eneo husika.

Hongera Tundu Lissu! shikilia hapohapo watu wanakuelewa sana na pia unawavuruga watu wa Lumumba. Hawana uwezo wa kujibu hoja zako,wanaishia kuandika "Magufuli 5 Tena".
 

Mzee Wa Republican

JF-Expert Member
Jul 20, 2013
952
500
Lkn pia walipenda waone uwasilishaji huo uwe kama alivyofanya Lowasa(2015) ,Dr Slaa(2010) au Freeman Mbowe (2005) ambao walikua wanazisema juu juu bila mifano hai inayowagusa wananchi wa eneo husika.
Katika hawa watatu uliowataja Dr Slaa alikuwa na uwasilishaji bora kabisa wa hoja na kwa kiasi fulani alifanikiwa kwenda deep hasa kwenye masuala ya chakula, maji na sera ya mambo ya nje.
Ila kwa sasa huyu Tundu Lissu anapiga vizuri sana tena kwa mazingira halisi zaidi kulingana na mahitaji ya kisiasa na kimkakati ya sasa.

Cheers to TL
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,551
2,000
Lissu anafundisha kama yuko darasani, tena kwa lugha nyepesi na relatable
... lugha inayotumiwa na Tundu Lissu inaeleweka mno . Halafu ajabu sijamsikia TL akichomekeachomekea vijimaneno vya English ili kuonesha usomi; yeye ni Kiswahili mwanzo mwisho tena kilichonyooka na chepesi hadi kwa wendawazimu! Na kukaa kote Ulaya 3 yrs hajapoteza ladha ya Kiswahili chake. Hiyo ndio sifa ya msomi.
 

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Apr 10, 2011
5,269
2,000
... lugha inayotumiwa na Tundu Lissu inaeleweka mno . Halafu ajabu sijamsikia TL akichomekeachomekea vijimaneno vya English ili kuonesha usomi; yeye ni Kiswahili mwanzo mwisho tena kilichonyooka na chepesi hadi kwa wendawazimu! Na kukaa kote Ulaya 3 yrs hajapoteza ladha ya Kiswahili chake. Hiyo ndio sifa ya msomi.
Jamaa anajua kujenga na kuzipanga hoja.... na ana facts na historia ya kutosha; jana namsikiliza Rujewa kuhusu tabu za wakulima na wafugaji na jinsi gani mashamba yaliyochukuliwa kwa wananchi na kupewa serikali leo hii wamepewa "wawekezaji" ambao wanwakodisha wananchi, lugha nyepesi na anagonga kweli kidonda chao. Ngoja tumsikia mzee wa hasira ataenda kusema nini huko. Yule Burushi anaweza kulazimishwa kurudisha mashamba 😁 😁 😁 😁 😁
 

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
11,747
2,000
Uchaguzi wa urais Chadema wanaweza kushinda - in fact it's theirs to lose but the following must be done first and foremost:

1. Umati wa wahudhuriaji wa mikutano wahamasishwe kupiga kura:
Hili sijaliona Lissu akilisisitiza kwenye speeches zake. inabidi awe akiwahamasisha watu wote wenye kadi wazinyooshe juu au ambaye kaacha home anyooshe kidole. hii itakuwa inawakumbusha wapigaji kura wajibu wao # 1.

2. Kuhakikisha kura zote zinahesabiwa katika vituo vya kupiga kura na kutumwa systematically kwenda kwenye tallying centre(s).

3. Kuhakikisha CREDIBLE representatives wanakuwa deployed wakati wote wa kuhesabu kura na wawe wanapiga picha kurasa zenye matokeo na kuziwasilisha haraka kunakostahili (refer # 2 hapo juu). MUHIMU SANA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom