Uwasilishaji wa Hitajio Katika Uandaaji wa Mchanganuo wa Mradi (Preparing a Need Statement)

Sep 11, 2020
9
8
1601055567777.png


Uwasilishaji wa Hitajio (Need Statement) ni kipengele MUHIMU sana katika uandaaji wa andiko la Mradi. Uwasilishaji wa Hitajio una malengo makuu mawili (2) ambayo ni:
  • Kuonyesha ni kwa namna gani TATIZO la mradi wako linarandana na matakwa/maslahi ya mfadhili (funder's interests/priorities). Maslahi/matakwa ya mfadhili hupatikana kwenye nyaraka ya Ombi la Uwasilishaji wa Miradi (Request for Proposals/Call for Proposals-RFP/CFP) au kwenye Taarifa ya Upatikanaji wa Ruzuku (Notice of Funding Availability-NOFA)
  • Kuonyesha TATIZO mahsusi (specific problem) ambalo mradi unaenda kushughulikia
Unapowasilisha HITAJIO la mradi wako; ni vyema kuhakikisha unajikita kwenye muongozo uliotolewa na mfadhili kupitia RFP. /NOFA kama nilivyoeleza hapo juu. Lakini pia hii miongozo huonyesha vigezo vya uombaji wa ruzuku (eligibility to apply), ni lazima uzingatie hili pia kabla ya kuanza mchakato wa uandaaji wa andiko.

Katika uandaaji wa HITAJIO la mradi (need statement), hakikisha unakuwa "specific". Kwa mfano unaweza ukasema "Kumekuwa na wimbi kubwa la vijana wanaojihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya Kwenye wilaya ya Kinondoni. Mradi utatoa elimu kwa vijana 200 na wadau wengine 50 juu ya athari za matumizi ya Dawa za Kulevya na njia za kuepukana nazo. Pia mradi utaanzisha "drug treatment clininic" mbili ambazo zitatoa huduma kwa vijana waliokwisha athirika na mtatumizi ya Dawa za Kulevya wilaya ya Kinondoni"

Hapa; tumekwisha eleza HITAJIO la mradi wetu, kwa maana nyingine tumekwishaonesha mradi wetu unaenda kufanya nini hasa? Hatua inayofuata sasa ni kuonyesha uthibitisho (proof) juu ya uwepo wa tatizo la matumizi ya Dawa za Kulevya kwenye wilaya ya Kinondoni. Uthibitisho juu ya uwepo wa tatizo huweza kuonyeshwa kupitia;
  • Takwimu za jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni zenye kuonyesha idadi ya watu waliokamatwa kutokana na kujihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya. Takwimu hizi hupaswa kuonyeshwa kwa njia ya "graph"
Baada ya kuonyesha uthibitisho wa matumizi ya Dawa za Kulevya katika wilaya ya Kinondoni, hatua inayofuata sasa ni kuonyesha kwamba ni kwa kiasi gani waathirika wakubwa ni vijana; ambao ndio walengwa wa kwanza wa mradi (primary stakeholders/beneficiaries). Hapa utapaswa kuonyesha;

  • Idadi ya vijana waliokamatwa kwa kujihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya. Ikiwa utakosa TAARIFA (data) juu ya idadi ya vijana waliokamatwa kwa kujihusisha na matumizi ya Dawa za Kulevya, basi utapaswa kuonyesha TAARIFA zako (data) ulizozipata kupitia "surveying" ulioifanya kwenye mitaa mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni iliyokuwa na lengo la kujua matumizi ya Dawa za Kulevya kwa vijana.
Wakati mwingine unaweza ukakosa TAKWIMU kutoka jeshi la POLISI, pia hata wewe mwenyewe ukakosa uwezo wa kufanya "surveying" ili kujua kivipi tatizo ni kubwa kwa vijana. Katika hali hii; unaweza kutumia uthibitisho wa;
  • Makala ya gazeti yenye kuonyesha matumizi ya Dawa za Kulevya kwa vijana wilaya ya Kinondoni.
  • Mahojiano na mtu muhimu katika jamii (Prominent Member) yakionyesha uwepo wa matumizi makubwa ya Dawa za Kulevya kwa vijana wilaya ya Kinondoni
  • Mahojiano na watendaji wa umma/serikali (Public Officials) kama vile walimu, Mamlaka zenye kuhusika na udhibi wa Dawa za Kulevya n.k
  • Wakati mwingine; unaweza kuonyesha uthibitisho kutoka wenye TOVUTI mbalimbali (websites) zilizobeba taarifa zenye kuonyesha kukithiri kwa matumizi ya Dawa za Kulevya kwa vijana wilaya ya Kinondoni.
Jambo jingine la kuzingatia, ni kuonyesha kwa kiasi gani matoke ya mradi wako yatachangia Taifa kiujumla kwenye mapambano dhidi ya matumizi ya Dawa za Kuelvya kwa kuonyesha takwimu za Kitaifa juu ya kukithiri kwa matumiza ya Dawa za Kulevya, pia kuonyesha uwiano kati ya malengo mahsusi katika sera za kisekta (sectoral policies), sera za kitaifa (National Strategies) n.k na lengo la mradi wako.

Ahsante

Blue Icon Consultancy (BIC)
Project Management, Strategic Management & Fundraising Management
Mobile: +255 719 518 367
Dar es Salaam
 
Back
Top Bottom