Uwanja wa Uhuru | Vodacom Premier League (VPL), Simba SC dhidi ya Singida United

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu kuwania Taji la Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kupigwa leo Jumatano ya March 11, 2020 ambapo Mabingwa wa Nchi, Simba SC, ambao ni vinara wa VPL, wakiwa na alama 68 kwa michezo 27 wanapambana na Singida United ambao wanashika nafasi ya 20 kwa alama 12 wakiwa wamecheza michezo 27 ya VPL.

Simba SC kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid waliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0, Je Singida United anaweza kuichelewesha Simba kwenye safari ya kuwania ubingwa wa VPL? Tusubiri dakika 90 za mchezo kuamua

Kumbuka mchezo huu wa VPL ni kuanzia saa 10:00 za jioni. Usikose Ukaambiwa

IMG_20200311_151543_785.jpeg

Update:

============================

Mabingwa watetezi Simba SC, leo Jumatano ya march 11, 2020 wameweza kuibuka na ushindi mnono kwa kuigaragaza Singida United kwa mabao 8 -0 kwenye mfululizo wa VPL

Simba SC, wakicheza kwa kutawala mchezo, walianza kuandika bao dakika za mwanzo tu ya mchezo kupitia kwa Meddie Kagere 2' 26' 41' 71.

Mabao mengine yakiwekwa kimiani na Deo Kanda mawili dakika ya 13' 18 huku Nahodha John Bocco akifunga bao moja dakika 19' na Sharaf Shiboub akifunga moja naye dakika 61 za mchezo.

Kwa matokeo haya Simba imefikisha alama 71 kwa michezo 28 na kuendelea kusafisha njia kuelekea kutwaa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo.

VPL, FT: Simba SC 8 -0 Singida Utd
 
Back
Top Bottom