Uwanja wa Uhuru umefurika sana!, watu Washindwa kuaga. Watakiwa kujipanga barabarani kuelekea Uwanja wa ndege ili waweze kupunga mkono

Mungu ni mwenye Ukuu sana na kazi yake haina makosa. Kila binadamu akiwemo Magufuli si wakamilifu.
Wangapi walidhihaki, yuko wapi Mungu wake aliyekuwa anamtaja kila siku!
Kwa machozi na umati huu, Mungu wake amemuinua mbele ya macho ya Dunia nzima. Wote tunashangaa, nani kawaambia watu hawa waje kwa wingi huu na walie vile!
 
Ili kuwatendea haki Wakazi wa Dar es salaam tunaomba kamati ya mazishi ya hayati Magufuli muongeze walau siku moja ili zoezi hili liitimishwe kesho.

Uwanja umefurika na nje misururu ni mirefu sana.

Maendeleo hayana vyama!
View attachment 1730918
Huo ndy mfano wa safari ya mwisho ya mtu mwema hapa duniani.

Taswira ya safari njema ya mbinguni inaanza kuonekana hapa hapa duniani hata kabla ya kuzikwa kaburini..

Magufuli ni mfano wa mtu mwema.


Nenda rais wa wanyonge

Nenda mtu mwema

Nenda my true leader of all times

Hakika umeumaliza mwendo kwa heshima kubwa..
 
Hivi ni kwa nini wachukua picha za video hawachukui sehemu ambayo na sisi tunaoomboleza tukiwa nyumbani tunaweza kuona sura ya Mh. Kwa dakika za mwisho? Au wanakatazwa? Au ndio maadili ya kazi yanawataka hivyo!? Ningetamani waonyeshe kama ilivyokuwaga kwa Hayati Baba Wa Taifa!
Wangeonesha watu wasingeenda uwanjani kama hivi
 
Ili kuwatendea haki Wakazi wa Dar es salaam tunaomba kamati ya mazishi ya hayati Magufuli muongeze walau siku moja ili zoezi hili liitimishwe kesho.

Uwanja umefurika na nje misururu ni mirefu sana.

Maendeleo hayana vyama!
View attachment 1730918
Mwanza itakuwa zaidi ya pale, wageni wamejaa kila mahali, ilitakiwa waupe mkoa wa mwz cku mbili.Kuna Wananchi wengine wanaona hawatapata nafasi ya kumuaga hapa Mwanza wametangulia Chato.
 
kwa Maoni yangu siku mbili Zaid ziongezwe, hata mkoa wa Mwanza waweke siku mbili, mazishi yawe siku ya JUMAPILI.
Mwanza wageni wanamiminika Sana kwa Sasa kwa ajili ya usalama, kamati ya mazishi iongeze siku ya kumuaga angalau siku mbili kwa jiji la Mwanza. Kwa Dar pekee Kuna watu wametoka mikoa ya jirani, Tanga, Pwan, Lindi, Mtwara n.k. Mwanza itakuwa zaidi ya hapo
Kuongeza siku ni jambo moja na kuchukua tahadhari za kiafya ni jambo lingine
 
Back
Top Bottom