Uwanja wa Taifa Dar es Salaam....Yanga wanaleta vurugu...

mzee wa njaa

JF-Expert Member
Jun 16, 2011
1,366
223
BREAKING NEWZ: Kutoka Uwanja wa Taifa. Mashabiki wa Ndala a.k.a Malapa wameenda kukaa jukwaa la Wekundu Simba Taifa kubwa na hawataki kutoka na wanaleta Vurugu huku wakiacha upande wao ukiwa tupu....Sasa ukisikia ugomvi ndio huo. Kwa hali hiyo wakifa watu wakulaumiwa ni nani? Makanyagio au Kandambili? TFF Mpo wanaanza wenyewe hao mgongo wazi.........In Zamalek We Trust...

Source: Macho yangu nashuhudia.
 
Hapo mie ndio natamani hizi timu zifutwe kabisa zibaki kwenye vitabu vya historia kama tanu na asp, ina maana yanya wakikaa kwenye huo upande ndio fujo? Au wakija simba ndio wataleta vurugu?
Ina maana sie tusio na timu tutapigwa pia tukikaa huko?, waache utoto
 
soccer la daslama hilo.....mabange tu!!
Ngoja nikaangalie IAAF indoor Grand Prix 2012 mimi....hizi bange waangalie hao hao walandukaji.
 
naona FFU wapelekwe uko bse simba watataka waje wakae apo walipozoea!
Kuna siku jamaa alikaa jukwaa la yanga bila kujua si ndala akapigwa bao jamaa kushangilia tuu kosa.
Walimshushia mvua ya kipigo mpaka akatoka.
Mazoea yana tabu sana
 
Unaumwa wewe,yaani unaandika kabisa in zamelek we trust? pumbafu.
 
Ndiyo unaweza kuona vipi wa Tanzania tuna matatizo ya kufahamu uzalendo na hiyo ni sababu tosha ya kushindwa kuendelea katika dunia hii, kwani haiwezi kuingia akilini eti Yanga ambayo ni timu yetu inawawakilisha wa tanzania, bado kuna wajinga wajinga eti wanajiita Simba eti wao hawawezi kuishangilia Yanga kwasababu ya utani ya jadi, jadi jadi ni aina mojawapo ya upumbavu tu, na nina maana hiyo hiyo kwa upande simba kama itakuwa hivyo, inabidi tufikie kipindi kuwa wamoja tunapowakilisha nchi yetu. Wakati nawakilisha haya mimi ni Simba tangu nilipojua kuna mpira wa miguu na timu za mpira katika dunia hii, lakini leo nitavaa jezi ya kijani kuiwakilisha Tanzania. Nione kama nitabadilika rangi.
 
Leo wimbo wa taifa utapigwa kwa heshma ya wawakilishi wetu, ambao ni yanga. Wewe utaimba wa Misri?
 
Kama wamekaa upande wetu chapeni tu hao, siku zote matoto matukutu hung'ang'ania kulala chumba cha wageni wakati chake kipo.
 
hata wakipasuana gemu lipo pale pale na wasubiri kichapo tu hao nasie azam tuzidi kuwatonesha zaidi hapo j5...
 
Leo wimbo wa taifa utapigwa kwa heshma ya wawakilishi wetu, ambao ni yanga. Wewe utaimba wa Misri?
Mnaanza kusahau juzi juzi tu hapa mmeshangilia TP Mazembe, Mkashangilia DC motema pembe, mkaja mkaizomea timu ya Taifa kwenye Cecafa eti ina wachezaji wengi wa Simba, leo inakuwaje mnakuwa wakali acheni watu washabikie Zamalek.
 
Leo wimbo wa taifa utapigwa kwa heshma ya wawakilishi wetu, ambao ni yanga. Wewe utaimba wa Misri?
Ni kwa heshima yao, sio yetu na mna bahati sijaenda uwanjani leo nilikuwa naongoza kuhesabu pasi za Zamalek.
 
Back
Top Bottom