Uwanja wa Taifa | Dar Derby, Vodacom Premier League (VPL) Yanga SC yaibamiza Simba SC kwa goli 1 - 0 ; Morrison akata mzizi wa fitina

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
20,408
2,000
Hello Tanzania na kando ya Tanzania

Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Vodacom Premier League (VPL), kuendelea kutimua vumbi leo Jumapili ya March 8, 2020 kwa kuwakutanisha watani wa Jani katika jiji la Dar es salaam, ambapo Yanga African SC, Wananchi wa Jangwani wanawakaribisha Simba SC, Wekundu wa Msimbazi, Mabingwa wa Nchi, kwenye Uwanja wa Taifa.

Mchezo huu unatarajiwa kuwa mgumu na mkali kwa muda wote wa dakika 90 kutokana na kuwa mchezo muhimu kwa kila timu huku Yanga SC yenye alama 47 kwa michezo 24 wakihitaji alama tatu muhimu katika mchezo wa leo dhidi ya Simba SC vinara wa Ligi wenye alama 68 wakiwa na michezo 26, ambao ushindi kwao ni kutaka kujiimarisha zaidi kileleni na hatimaye ubingwa.

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga SC Luc Eymael, amesema wamejipanga kuwakabili wapinzani wao Simba SC huku akiongeza kuwa ana uzoefu na derby kama hizi.

"Nina uzoefu wa kutosha wa mechi kama hizi (Derby) tangu nafundisha Sudan, DRC Congo na Kenya hivyo mchezo huu ili upate matokeo ni mazuri ni kuandaa mbinu na si kuangalia rekodi au matokeo ya nyuma", amesema Eymael

Kwa upande wake Kocha wa Simba SC, Sven Vanderbroeck, amesema amekiandaa kikosi chake kuchukua alama tatu ili mwisho wa msimu kushinda ubingwa.

"Tunacheza mchezo huu kama si mchezo wa Ligi kwa sababu kila mmoja anajua tumewaacha kwa alama kadhaa, tutaucheza kama mchezo wa kweli wa wapinzani hivyo tumejiandaa kuchukua alama tatu na tusonge mbele ili mwisho wa msimu tushinde ubingwa", amesema Vanderbroeck

Kwenye mzunguko wa kwanza wa VPL, timu hizi zilitoka sare ya mabao 2-2 Je awamu hii ya lala salama itakuwaje? Safari ya dakika 90 kuamua.

Kumbuka mchezo ni kuanzia majira ya saa 11:00 jioni.
Karibuni sana Jopo la WanaJF, Kuongoza Jahazi Sambamba Nami Nahodha Ghazwat, Tunakuambia Usibonyeze Kitufe, USIKOSE UKAHADITHIWA.

============

Takwimu Yanga na Simba VPL, 2019/2020.

Simba SC |
Nafasi 1
Alama 68
Ushindi 22
Sare 2
Vipigo 2
Magoli ya kufunga 55
Magoli ya kufungwa 14
Clean Sheets 15

Yanga SC |
Nafasi 4
Alama 47
Ushindi 13
Sare 8
Vipogo 3
Magoli ya kufunga 29
Magoli ya kufungwa 18
Clean Sheets 12

====================

UPDATE;

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Ahmad Ahmad, atakwepo uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo wa VPL, Derby ya Yanga African na Simba SC

Rais huyo wa CAF, ambaye amealikwa na Shirikisho la mpira wa miguu nchini Tanzania (TFF), kwa ziara ya siku tatu, na atakutana na viongozi wa Serikali na Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, kuzumgumzia maendeleo ya soka na ndiye atakuwa mgeni rasmi kwenye huo wa watani wa Jadi ambao utapigwa leo Jumapili ya March 8, 2020.

IMG_20200308_002126_629.jpeg
IMG_20200308_002215_381.jpeg
IMG_20200307_235619_628.jpeg
[/B]​
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom