Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere na Huduma mbovu za Mtandao na huduma

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
518
1,000
Kwa mwezi Sasa nimepita Uwanja wa ndege wa Dar kwenda na kurudi, siku ya kwanza nilikuta mrundikano wa watu nikasikia network imekata sijui mifumo mibovu. Ukiwasikiliza watendaji hasa waliovaa kirahia wanavyolalamikia mifumo ya uwanja ikiwemo TTCL nadhani ndo mtoa network utadhani siyo waaajiriwa na Kama ni waajiriwa basi wamechoka na bla bla za uongozi wa uwanja.

Waliovaa uniform ukiwauliza shida nini unaambiwa subiri tunarekebisha. That day nakumbuka Hali ilikuwa tete hata watu kuwahudumia kwenye mfumo hawakuhumiwa nikasema huu ndio uwanja wa kimataifa?

Kutokana na kero ile si Watanzania Wala wageni waliokuwa wanajadili positive, mfano raia mmoja wa China alisikika akisema China tunaelekea 5G Wakati Tanzania ndo kwanza wapo 2G. Hii kauli ilimaanisha tupo nyuma sana ya Dunia. Inakuwaje lango kuu lakuingia nchini likose huduma ya network?

Inakuwaje mfumo wa Askari wa Uhamiaji uache kufanya kazi? Kama waliovaa kirahia ambao wengi watakuwa kutoka usalama wanalalamika adharani kwenye makundi makundi inaamana Rais asikii hiki kilio? Kwanini makampuni ya tiketi yaliyopo hapohapo uwanjani network haisumbui?

Haiwezekani ikawa hujuma kufifisha utalii na usafiri wa anga nchini? Haya mamifumo ya kila siku imegoma maana nimepita Tena nakuta nyomi tatizo lilelile watu wamejipanga uhamiaji kwanini hao TTCL wasiwajibishwe au mkatumia mifumo Kama ya mashirika ya ndege? Wao wanapata wapi internet ambayo mtu wa Uhamiaji anayeingiza taarifa anakosa?

Ebu fuatilieni hili tatizo mnatengeneza image mbaya kwa wageni kukaa kwenye mstari lakini pia mkiendelea mtawavutia wahalifu kupita kwenye mipaka Kama hii

Mnakera kwakukosa vipaombele
 

Auz

JF-Expert Member
Apr 6, 2016
9,795
2,000
"Wananchi wanahitaji maji, barabara na zahanati"
Kwa kukosekana internet uwanja wa ndege, kunawezesha maji, barabara na zahanati viwafikie wananchi? Vitapatikana vipi bila ya pesa za wageni (kigeni)?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom