Uwanja wa ndege Mwanza wajaa maji tena, ndege zasimama kutua na kuruka

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,595
Waziri mkuu pia ashindwa kuondoka.

Pia abiria ambao flights zao zipo destined to Dar es salaam na Kilimanjaro, nao wamekwama. Run way haionekani baada ya uwanja wote kufunikwa na maji.

Tunasubiri maji yaondoke kwa hiari.

70c9jl.jpg
 
Updates.
Uongozi wa uwanja umeamua kuufunga uwanja kwa muda wa masaa sita, hali ambayo imepelekea route ya kwenda Bukoba kwa siku ya leo kuvunjwa kutokana na hali ya uwanja wa bukoba kutokuwa na taa katika njia ya kukimbilia ndege hivyo ndege kutoruhusiwa kutua usiku
 
Na itakuwa hivyo mpaka siku itokee ajali kubwa ndiyo utawasikia watu wanaoitwa serikali wakiamka!
 
ndo waliyoyataka hayo... fedha za kuufanyia ukarabati wa huo uwanja walishazila
 
ndo waliyoyataka hayo... fedha za kuufanyia ukarabati wa huo uwanja walishazila
"ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni"
Hii issue ni kweli nimetumiwa sms na mfanya kazi mwenzetu ambaye yuko hapo airport alikua anamsindikiza boss wetu.hata hivyo mida ya saa saba nilipishana na msafara wa waziri mkuu ukielekea Airport.Kinachonichekesha ni kuwa waziri mkuu yuko hapo nje airport sasa sijui atakaa hapo hadi saa ngapi.Nimeongea pia na mteja wangu mmoja Dar yeye ameniambia wameambiwa wataondoka saa mbili usiku pale JKNIA kuja mwanza.Namalizia kazi ofcn ,nadhani itabidi nielekee eneo la tukio nipate picha.Sijui wanoko kama wataniruhusu au watanipakipondo mbele ya mtoto wa mkulima.
Hivi Alshaabab hawako mwanza,maana jamaa atakuwepo muda mrefu tu!.
 
Na itakuwa hivyo mpaka siku itokee ajali kubwa ndiyo utawasikia watu wanaoitwa serikali wakiamka!


Kwa kweli tusiombe litokee.... Ila Wahenga walisema "dalili ya mvua ni mawingu...."
Sasa mie nashangaa hawa wahusika wanasubiri nini kurekebisha hicho kiwanja??
 
ndo waliyoyataka hayo... fedha za kuufanyia ukarabati wa huo uwanja walishazila


Hawa watu sijui wakoje... Hawajui kabisa kula na kipofu... Hivi kwani ni lazima kula 100%.....??
Kwanini wasifanyie kazi asilimia 60 halafu wale japo 40% japo si haki??
 
Kujaa maji kwa uwanja wa ndege mwanza mbona unajaa kilasiku,serikali inajua kukusanya pesa tu ila kujenga mitaro mikubwa ili uwanja uwe unaweza kuhimili maporoko yamaji hawawezi,hii nimara ya4 ktk kipindi chamwezi 1 uwanja unafungwa kwakujaa maji,hawatofanya matengenezo yamitaro mikubwa mpk ije ndege iuwe watu kwa mamia kwa ajali ndio utaskia wanafanya ukarabati,kweli hii nchi ya majuha.
 
Hawa watu sijui wakoje... Hawajui kabisa kula na kipofu... Hivi kwani ni lazima kula 100%.....??
Kwanini wasifanyie kazi asilimia 60 halafu wale japo 40% japo si haki??
Mi wala siwalaumu wao... najilaumu mimi mwenyewe kwa kutokuwa na moyo wa kuwawajibisha wezi hawa
 
Waziri mkuu ndiyo ameingia dar hivi punde toka Mwanza baada ya maji kupungua na ndege kuruhusiwa kuruka,
hivyo abiria wengine nao wameshaanza ku check in ready to fly to their destinations.
 
me naombea yakae hata wiki tatu hivi,labda itawapa fundisho namna ya kuthibiti maji hayo,hapo kuna dalili ya kuleta maafa siku zijazo.
 
Hali ilivyokuwa katika uwanja wa ndege wa Mwanza.
dYTakgAAAABJRU5ErkJggg==

Wakitoka kuangalia hali ilivyo na kupewa taarifa ya kuahirishwa kwa safari
 
Zikiwa zimebaki siku 3 kuadhimisha miaka hamsini ya uhuru Hivi ndivyo hali ilivyokuwa jana uwanja wa ndege mwanza. inayoonekana ni ndege ya serikali na waziri mkuu alikuwa ndani ya ndege lakini ilishindikana kuondoka kutokana na uwanja huo kuwa mkondo wa maji.

Copy of IMG_0049.jpg Copy of IMG_0053.jpg Copy of IMG_0052.jpg
 
Back
Top Bottom