Uwanja wa ndege kukodishwa Wachina

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Sioni sababu yoyote ya muhimu ya kuuendesha Uwanja wetu wa Kimataifa kwa ubia na kampuni toka China.

Posted Date::4/28/2008
Uwanja wa ndege kukodishwa Wachina
*Ni ule wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar
*Kuendeshwa kwa ubia na Kampuni ya Sonangol

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

KATIKA moja ya maamuzi mazito ambayo yanatarajiwa kufanywa tangu kuanza mageuzi ya Sera za Uchumi, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere sasa utaendeshwa kwa ubia.

Uchunguzi huo wa Mwananchi umebaini kwamba, serikali iko katika mazungumzo kwa muda mrefu kati yake na Kampuni ya China Sonangol ili iweze kukabidhiwa jukumu la kuuendesha uwanja huo kwa ubia.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, China Sonangol inatarajiwa kufanya magaeuzi makubwa katika uwanja huo, ikiwa ni pamoja na kujenga eneo jipya la kutua ndege ambalo litafahamika kama 'Terminal Three'.

Uwanja huo kwa sasa una sehemu mbili (Terminal One na Two), ambazo hutumika kwa ajili ya ndege hutua na kuondoka.

Katika mpango huo, Mwananchi imezidi kubaini kwamba, China Sonangol pia itakarabati katika kiwango cha juu eneo la Terminal One na Two, kutoka hali ya sasa.

Uchunguzi huo pia umebaini kampuni hiyo iwapo itakubaliwa katika mazungumzo yanayoendelea, itajenga Chumba kipya cha Wageni Maarufu (VIP) kutokana na kilichopo sasa kuwa kidogo na ambacho hakiendani na wakati.

Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk Makongoro Mahanga na Katibu Mkuu Omari Chambo, wote walipoulizwa walisema kwa kifupi hayo ni mazungumzo tu.

Dk Mahanga alisema hadi sasa hakuna makubaliano ambayo yamefikiwa katika suala hilo, kwani kilichopo ni mazungumzo.

Hata hivyo, Dk Mahanga ingawa hakukataa wala kuthibitisha kama kampuni hiyo itakubaliwa, alisisitiza kwamba uamuzi kama huo hata ukifanyika si mgeni kwani nchi nyingi duniani huendesha viwanja vya ndege kwa ubia.

"Sitaki kuzungumzia kitu ambacho hakipo kwani hayo ni mazungumzo tu, lakini hata kwa mfano mpango huo wa ubia si mpya kuna nchi nyingi duniani zinaendesha viwanja vya ndege kwa ubia," alisisitiza kwa kifupi.

Kwa upande wake Chambo, alisema suala hilo linaweza kupotoshwa, lakini akaahidi kutoa taarifa zaidi kwa gazeti hili.

"Msianze kupotosha jambo zuri likawa baya, nitafute nikupe taarifa zaidi kuhusu hilo," alisisitiza.

Wakati Dk Mahanga na Chambo, wakikataa kuzungumzia hilo kwa undani, uchunguzi huo umebaini zaidi kwamba China Sonangol, ndiyo ambayo pia iko katika mpango wa kuisaidia ATC kivifaa na kuboresha usafiri wa ndege kutoka nchini hadi Beijing.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo wa kina, Rais Jakaya Kikwete akiwa katika ziara yake nchini China wiki mbili zilizopita, suala hilo lilitiliwa mkazo zaidi.

Ziara hiyo ya Rais pia aliandamana na aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge.

Mwananchi imebaini kwamba, eneo ambalo linaangaliwa kujengwa VIP mpya ni karibu na Dahaco.

Katika uchunguzi wake huo, Mwananchi imebaini kwamba ubia huo utakuwa katika kiasi ambacho kinaweza kuwa asilimia 50 kwa 50, ingawa mjadala kuhusu hilo bado.

Uwezekano huo unatokana na Kampuni hiyo ya Kichina kutarajiwa kutoa kiasi kikubwa cha fedha za uwekezaji, ambazo zitafanya nayo iwe na nguvu kubwa katika maamuzi ndani ya menejimenti.

Taarifa hizo za kiuchunguzi zinaonyesha kwamba, tayari Kampuni ya China Sonangol, imeonyesha nia ya kukubali kulipia deni la kati ya Sh 9 hadi 10 bilioni, kutoka kwa wananchi wa eneo la Kipawa lililo karibu na uwanja huo wanaodai fedha za kuhamishwa kwa ajili ya kupisha upanuzi huo.

Hata hivyo, suala hilo liko katika hatua za mwanzo na inaelezwa kwamba, bado halijafakikishwa katika Baraza la Mawaziri kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi na wala kujadiliwa na Kamati ya Bunge ya Miundombinu.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, Mohamed Misanga, alisema hana taarifa yoyote kuhusiana na suala hilo na anachojua ni kwamba, uwanja huo unaendeshwa kama kawaida wala hajui mpango wa ubia.

"Kamati haina hiyo taarifa, ninachoamini na kuendelea kuamini ni kwamba, uwanja unaendeshwa kama kawaida," alisisitiza Misanga.

Iwapo uwanja huo utaendeshwa kwa ubia itakuwa ni moja ya hatua kubwa kutokana na unyeti wake kwa usalama wa nchi, kwani ni moja ya eneo muhimu kwa maadui wa ndani na nje kuweza kuihujumu nchi.
 
Nashangaa siku zote walikuwa wanangoja nini

BTW

walitakiwa wajenge uwanja mpya wa KISASA...sijui wanasubiri nini

Kama wanazo pesa za kupigana vita COMOTRO i am sure pesa za uwanja mpya zitakwepo tuu
 
MwK, mimi nadhani ni katika wale tunaokubali kuwa Tz ni kichwa cha mwendawazimu.... Unajua hii issue ya Mwalimu Nyerere Int'l Airport nadhani handling yake ipo na mikingamo mingi sana..... Sasa leo wanakuja na issue ya waChina kuiendesha... Sina tatizo lakini nataka kujua, ni study gani imefanyika ikapelekea serikali kufikiria hata kuibinafsisha.... Nasema hivyo kutokana na mambo mawili makubwa:
1. Serikali imeshatangaza uamuzi wa kujenga uwanja mpya wa ndege maeneo ya Kilwa road, nadhani ni Kisiju or something (I stand to be corrected but iliongelewa sana mwaka jana)....

2. Serikali kwa wakati huo huo inasema inafanaya mip[ango ya kuwalipa wananchi wa jirani na MNIA ili kuruhusu upanuzi wa uwanja wetu.....

Sasa leo tunaambiwa mChina atauendesha sasa nipo completelly lost sababu sijui wapi ni wapi manake inakuwa ngumu kuangalia pande zote ukizingatia ni pesa za mwananchi wa chini ndizo zinatumika instead ya kuleta maendeleo!!!

WanaJambo wenzangu, naomba mnieleweshe manake hii hai make sense into my small head kabisaaa!!!

Naomba kuwakilisha!!!
 
Nashangaa siku zote walikuwa wanangoja nini

BTW

walitakiwa wajenge uwanja mpya wa KISASA...sijui wanasubiri nini

Kama wanazo pesa za kupigana vita COMOTRO i am sure pesa za uwanja mpya zitakwepo tuu

Kwa mtindo huu wa kuwa na pesa za comoro, pia hainishawishi kubinafsisha, tunge miliki wenyewe na kama ni shida ya uongozi ndio tungetafuta nje. SINA IMANI TENA NA UBINAFSISHAJI
 
Hali ya Uwanja wetu unatia aibu mno kwa sasa! Ukiendeshwa na kampuni yenye sifa zinazostahili na mikataba hiyo ikilinda maslahi ya taifa, nina neno moja tu la kuongeza RUHSA!
 
hata kama ni kubinfsisha wakuu ina maana ule utaratibu wa kutangaza tenda haupo tena? Au mChina ameamua kutusaidia kama tulivyosaidiwa na Mshauri wetu kule TRL??

Uendeshaji wa uwanja wa ndege nao unatushinda eti tuubinafsishe, give me a break mmeshaangalia kule KIA kukoje wakulu??!!?

Naomba kuwakilisha!!!
 
MwK, mimi nadhani ni katika wale tunaokubali kuwa Tz ni kichwa cha mwendawazimu.... Unajua hii issue ya Mwalimu Nyerere Int'l Airport nadhani handling yake ipo na mikingamo mingi sana..... Sasa leo wanakuja na issue ya waChina kuiendesha... Sina tatizo lakini nataka kujua, ni study gani imefanyika ikapelekea serikali kufikiria hata kuibinafsisha.... Nasema hivyo kutokana na mambo mawili makubwa:
1. Serikali imeshatangaza uamuzi wa kujenga uwanja mpya wa ndege maeneo ya Kilwa road, nadhani ni Kisiju or something (I stand to be corrected but iliongelewa sana mwaka jana)....

2. Serikali kwa wakati huo huo inasema inafanaya mip[ango ya kuwalipa wananchi wa jirani na MNIA ili kuruhusu upanuzi wa uwanja wetu.....

Sasa leo tunaambiwa mChina atauendesha sasa nipo completelly lost sababu sijui wapi ni wapi manake inakuwa ngumu kuangalia pande zote ukizingatia ni pesa za mwananchi wa chini ndizo zinatumika instead ya kuleta maendeleo!!!

WanaJambo wenzangu, naomba mnieleweshe manake hii hai make sense into my small head kabisaaa!!!

Naomba kuwakilisha!!!

Morani, nafikiri matatizo tuliyonayo pia yanatokana na kutokuwepo kwa mipango mizuri ndio maana tunaona mipango inayokinzana katika jambo moja au uvivu wa kufikiri na kurukia mambo bila kufanyika utafiti kwanza (inawezekana yote mawili yana chimbuko moja).

Juu ya maswali yako, sorry sina jibu.
 
hata kama ni kubinfsisha wakuu ina maana ule utaratibu wa kutangaza tenda haupo tena? Au mChina ameamua kutusaidia kama tulivyosaidiwa na Mshauri wetu kule TRL??

Uendeshaji wa uwanja wa ndege nao unatushinda eti tuubinafsishe, give me a break mmeshaangalia kule KIA kukoje wakulu??!!?

Naomba kuwakilisha!!!

Sijui mambo ya ndani lakini KIA panaonekana pana hadhi inayotakiwa, ni uhaba wa ndege zinazotua hapo ukilinganisha na viwanja kama hivyo nje ya TZ
 
hata kama ni kubinfsisha wakuu ina maana ule utaratibu wa kutangaza tenda haupo tena?

Ni vyema tenda ikatangazwa na upembuzi ukafanyika wa kina. Mleta hoja atuongoze katika hili.

Uendeshaji wa uwanja wa ndege nao unatushinda eti tuubinafsishe

Uendeshaji wa uwanja wa ndege umetushinda, lets face it. Sababu za kushindwa huko zinaweza zisiwepo au zikawa nyingi lakini hazibadili ukweli TUMESHINDWA!

give me a break mmeshaangalia kule KIA kukoje wakulu??!!?

Kunasikitisha sana! Maslahi ya taifa hayakulindwa, bila shaka, kampuni haina uwezo na/au mkataba unamlinda huyo anayeendesha uwanja husika.
 
Hiyo ni PPP/PFI na ni nzuri ila utekelezaji wake kwa TZ ni mbovu. Wangetangaza tender ili angalau kupata watu wa maana.
 
Guys i think this is quite right, kwakweli ni aibu mno kuona viwanja vya ndege vingi ulimwenguni kwa sasa vikiwa vya kisasa zaidi, kuanzia na ASIA,America,Europe na mwishowe ni huku kwetu!

Kwa afrika ya mashariki, Entebbe waliufanyia marekebisho wa kwao na kujenga termina nyingine mpya ambayo walau kidogo inapendeza na ni mwaka jana alipokuja malkia wa Uingereza na Brown kwenye commonwealth head of states meeting lakini pia nenda kaangalie Jomo Kenyatta sio sawa na wakwetu kabisa kinachosikitisha wakati mwingine ukiwa umekaa kwenye lounge umeme unakatika na ni adha kubwa kweli.
Nimetoka jana Lagos - Mohamed Mutalla airport na kwakweli jamaa wameubadilisha pia, nilikuwa huko last year!
Ninachojaribu kusema ni kuwa, there are alot of changes that our african airports are trying to do at the moment including having new premises and runways! Tanzania tunahitaji kwa hali na mali, moja kwa utalii wa nje na ndani, biashara na mengineyo yatakayo ajiri watanzania wengi mno.
Si mbaya kupata mwekezaji ambaye ataufanya uwe wa kisasa zaidi, airport nyingi tu zimefanyiwa ubinafsishaji tunachohitaji kutoka kwa viongozi wetu ni kuhakikisha mageuzi haya yanafanyika yakituacha na kitu badala ya hohehahe.
I trust JF, tuseme ubinafsishaji upite ila ufisadi kwenye hii project usiwepo kwa level yoyote ile!
Aviation industry is a driving force to boosting our tourism industry if is managed with professionals and honesty!
 
Tutasalimika ? Hawa jamaa si waaminifu kabisa .Kwa wakiuchukua huo uwanja wataurudisha lini ? Mbona nimeanza kuogopa ? Kama kweli issue ni kuiga what others does mbona hatuigi kwa haraka kuwapeleka mahakamani akina Chenge na watu wa EPA ?Jamani nisaidieni .
 
Tutasalimika ? Hawa jamaa si waaminifu kabisa.Kwa wakiuchukua huo uwanja wataurudisha lini ? Mbona nimeanza kuogopa ?

Hawa jamaa ndio the new super power hawana huruma au ethics zozote tofauti na wengine wakin'gana hawatoki


Kama kweli issue ni kuiga what others does mbona hatuigi kwa haraka kuwapeleka mahakamani akina Chenge na watu wa EPA ?Jamani nisaidieni

Akina Chenge na EPA tutsikia tu kwenye bomba it may take decade kuwafikisha mahakamani...we iba leo mbuzi next day uko segerea that is how systems work kwetu bongo...

Lakini usikate tamaa mapambano yanaendelea ili vitukuru wetu watakuja kuyaona mabadiliko tunayokemea sasa...hopefully
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom